google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 11, 2015

Njia 4 Za Kuondoa Mfadhaiko Wa Mawazo.

No comments :
Mawazo ni jambo la kawaida kwa binadamu, huwa inategemea mawazo hayo ni ya namna gani. Wataalamu wa saikolojia wanasema kuna njia mbalimbali za kuweza kuondoa mfadhaiko wa mawazo ambazo ukiweza kuzitumia zitakuweka huru zaidi na kuweza kuishi maisha ya furaha ambayo unayahitaji katika maisha yako.

1.Kuwa na mawazo chanya.
Njia ya kuongea wewe mwenyewe ni moja ya suluhisho la kuweza kuondoa mfadhaiko wa mawazo. Kuna wakati inatokea unaongea mwenyewe kwa sauti au moyoni kuwa nitafanya hiki au kile. Mtazamo chanya utakusaidia sana kurudi katika hali yako ya kawaida na kuweza kabisa kujiweka sawa.


Hivyo unashauriwa kujifunza kubadilisha mawazo hasi kuwa chanya. Kwa mfano unaweza kujisemea nitafanya hivi au nitafanya vizuri zaidi ya hivi hata kama unaona mambo yanakwenda vibaya. Kwa kuwa na mtazamo chanya kutakusaidia sana wewe kutoa mfadhaiko katika maisha yako.


2. Tafuta unafuu.
Mara nyingi ukiwa na mfadhaiko wa mawazo hukufanya ujisikie vibaya, hivyo unatakiwa utafute kitu ambcho kutakuletea shinikizo la mawazo. Hivyo basi, unashauriwa kutumia muda usiopungua dakika 15 kwa kufanya vitu vifuatavyo kuwasilina na marafiki kwa kutuma meseji au kusoma vitabu, magazeti na majarida.

Vilevile sikiliza muziki, andika vitu ambavyo unatakiwa kufanya katika maisha yako. Kwa kufanya hivyo utakuwa unajitafutia unafuu wewe mwenyewe, hali itakayoweza kukufanya sasa uweze kujihisi kuondoka kabisa katika huo mfadhaiko wa kimawazo unaokutesa.


3. Tumia njia za dharura.
Kuhesabu moja hadi kumi, vuta pumzi kwa ndani kwa nguvu mara tatu au tano, jiondoe kabisa katika mfadhaiko huo kwa kusema moyoni nitafanya baadae, nenda katembee. Usiogope kusema samahani kama umekosea lakini pia weka kengele ya kukumbusha kwa dakika 10 kabla ya kujihadhari kuchelewa kuamka asubuhi.

Nyingine jiulize niyafanyaje matatizo makubwa  na kuyafanya kuwa madogo, jibu simu mara moja kwa siku, jibu barua pepe au barua, epuka kufanya vitu vingi sana kwa wakati mmoja. Kama ni kuendesha gari endesha kati kati ya barabara ambayo haina vurugu sana.


4. Kupumzika.
Kumpumzika ni zaidi ya kukaa na kuangalia kipindi katika runinga. Ili kuondoa mfadhaiko unaotakiwa kupumzika ufanye hii kitu ndani ya akili na mwili wako.  Wakati wa kupumzika kuna michezo mbalimbali kama yoga ambayo unaweza kuifanya na kutafakari kwa kina zaidi kile unachoona kinakupa mfadhaiko.

Katika hili tunaona watu wengi hulifanyia kazi na kufunza mfano kitendo cha kuvuta pumzi kwa ndani inaweza ikawa ni njia nzuri ya kuweza kujipumzisha hasa ukiwa nyumbani.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.