Mar 31, 2016
Hii Ndio Sababu Kubwa Ya Kushindwa Kufanikiwa Kwako.
Mafanikio makubwa huja kwa watu waliojiandaa. Kitu hicho ni baadhi ya watu wachache sana ambao hutambua. Watu wengi tunafikiri ya kuwa mafanikio tunayoyahitaji msingi wake mkubwa ni mtaji kwa maana ya kuwa na pesa kwa ajili ya kuanzisha biashara au jambo lolote.Kuwa na wazo hilo la kuwa na mtaji sio tatizo sana. Ila tatizo linakuja pale ambapo tunasahau ya kuwa kuna tatizo kubwa ambalo linafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto zao.
Jambo hilo ni WOGA BINAFSI hili ndilo tatizo kubwa ambalo watu wengi linawafanya washindwe kufikia ndoto Zao. Kuna usemi husema maisha ya mwanadamu yamethiriwa kwa kiasi kikubwa na woga.
Watu wengi wana woga wa uthubutu katika jambo fulani, mfano mtu leo hii anawaza katika akili yake kwamba hawezi kufanya jambo fulani. Akili yake ndivyo inavyowaza hii ni kutokana na woga alio nao katika nafsi yake.
Woga binafsi mara nyingine hujenga na jamii ya watu ambao wanakuzunguka. Mfano leo hii unataka kuanzisha biashara fulani kuna baadhi ya watu watakwambia hautaweza na wewe unaamini kweli hautaweza, hii ni kutokana umeshajenga woga binafsi kwa kuwa mtu fulani alikwambia hautaweza kufanya jambo fulani.
PUNGUZA WOGA ILI KUFANIKIWA. |
Wapo pia baadhi ya wazazi mara nyingi huwajengea
picha mbaya watoto zao na watoto hao kuamini kuwa hawewezi. Mfano mtoto wako
kila wakati anafeli katika masomo yake, badala ya mzazi kumuonesha njia za
kuweza kufaulu ila wewe unamkatisha tamaa. Mwisho wa siku mtoto huyo anajenga
woga binafsi, na kuamini yeye hawezi.
Ndugu Msomaji wa makala hii, inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa, hii ni kwa sababu kuna maneno ambayo uliambiwa na wazazi au ndugu wengine wanakuzunguka na leo hii bado unayakumbuka, mfano inawezekana uliambiwa wewe kichwa chako sio cha biashara na wewe ukayaamini maneno hayo.
Hivyo wakakwambia ujikite zaidi katika elimu yaani usome kwa bidii ili uje kuwa mtu fulani hapo baadae.
Kwa kuwa uliamini kuwa huwezi kufanya biashara na ukajikita katika zaidi katika elimu. Umemaliza chuo, ajira hakuna kwa kuwa ulishaambiwa huna kichwa cha biashara leo hii unaona maisha yazidi kuwa magumu na huna njia nyingine za kujiongeza ili uweze kufanikiwa.
Huwa ni ukweli usiofichika wala hauhitaji mifano kutoka ulaya watu wengi tunashindwa kufanikiwa hii ni kutokana na woga binafsi tulionao. Wito wangu kwako ni kwamba ili uweze kufanikiwa unahitaji kujiamini, tumia akili, nguvu na kuwa na mawazo bora ya kufikiri yatakayokufanya wewe kutoka katika hali uliyonayo kusonga mbele kuyasaka Mafanikio. Naomba kwa Leo niishie hapo.
Usisite kumshirikisha mwenzako naye ajifunze kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Imeandikwa; Benson chonya
dirayamafanikio@gmail.com
Ndugu Msomaji wa makala hii, inawezekana hata wewe unashindwa kufanikiwa, hii ni kwa sababu kuna maneno ambayo uliambiwa na wazazi au ndugu wengine wanakuzunguka na leo hii bado unayakumbuka, mfano inawezekana uliambiwa wewe kichwa chako sio cha biashara na wewe ukayaamini maneno hayo.
Hivyo wakakwambia ujikite zaidi katika elimu yaani usome kwa bidii ili uje kuwa mtu fulani hapo baadae.
Kwa kuwa uliamini kuwa huwezi kufanya biashara na ukajikita katika zaidi katika elimu. Umemaliza chuo, ajira hakuna kwa kuwa ulishaambiwa huna kichwa cha biashara leo hii unaona maisha yazidi kuwa magumu na huna njia nyingine za kujiongeza ili uweze kufanikiwa.
Huwa ni ukweli usiofichika wala hauhitaji mifano kutoka ulaya watu wengi tunashindwa kufanikiwa hii ni kutokana na woga binafsi tulionao. Wito wangu kwako ni kwamba ili uweze kufanikiwa unahitaji kujiamini, tumia akili, nguvu na kuwa na mawazo bora ya kufikiri yatakayokufanya wewe kutoka katika hali uliyonayo kusonga mbele kuyasaka Mafanikio. Naomba kwa Leo niishie hapo.
Usisite kumshirikisha mwenzako naye ajifunze kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Imeandikwa; Benson chonya
dirayamafanikio@gmail.com
Mar 30, 2016
Chanzo Kikubwa Kinachokufanya Usitimize Ndoto Zako.
Kuna baadhi ya watu wanazitambua njaa zao na wengine hawazitambui njaa zao za mafanikio.
Njaa hizo za mafanikio zinatofautiana
baana ya mtu mmoja na mwingine. Nimesema ni baadhi ya watu wachache ndio watu
ambao wanajishughulisha usiku na mchana ili kuangalia ni mbinu zipi wanaweza
kuzitumia ili waweze kufanikiwa. Lakini
watu hao wenye njaa ya mafanikio, mambo yao wakati wa kuyasaka mafanikio huwa
ni mateso ya hapa na pale.
Watu hawa huzunguka huku na huko ili kupata
maisha bora. Watu hawa naweza nikawaona ni watu ambao huwa wana sura za huzuni
zaidi ila furaha huchukua kwa kiwango kidogo sana katika maisha yao. Wapo
baadhi ya watu kutokana na njaa walinazo kila kazi yeyote yupo tayari kuifanya.
Ila tatizo linakuja ni kwamba pindi apato fursa ya kufanya kazi wengi wao
wanapweteka na kutoonesha njaa walizokuwa nazo mwanzo pindi wapatapo nafasi ya
kufanya kazi. Hivyo katika makala ya leo nataka nikushirikishe kwa nini watu
hao huwa hivyo.
Hii ndio sababu kubwa kwa nini watu wengi
hawatumii nafasi walizozipata kwa asilimia mia moja;
Kuridhika
na walichonacho.
Tafiti zinaonesha ya kwamba asilimia kubwa ya
watu wakipata kile walichokuwa wanakihitaji hawakifanyi kwa asilimi mia moja.
Hii ni kutokana mtu anaona kitu hicho ameshakipata hivyo hana haja tena na
kuanza kuendelea kuongeza juhudi na ubunifu katika kitu au jambo fulani.
Kimsingi ni kwamba binadamu ni watu wa kulalamika sana nasema hivi nikiwa na maana
ya kwamba leo hii ukikutana na mtu ambaye hana ajira au hafanyi biashara ni mtu
wa kulalamika sana, na asilimia kubwa la kundi hili wengi wao husema nikija
kupata kazi au nikija kufanya biashara nitafanya vizuri ili kutumiza ndoto
zangu. Ila tazizo maneno hayo hugeuka dakika chache akilipata jambo hilo
hafanyi kama alivyoahidi mwanzoni wakati wa akilitafuta jambo hilo.
USIRIDHIKE SANA NA KILE UNACHOKIFANYA. |
Mfano leo hii tunaona baadhi ya wasanii wa
nyimbo wanapotea katika sanaa, hii mara
tu baada ya kutoa wimbo mmoja ambao utapendwa na watu wengi. Tatizo kubwa wengi wao huwa wanaridhika na
mapokeo ya wimbo huo na kupweteka na kujiona tayari wameshafanikiwa na mwisho wa siku hatuwasikii tena. Tatizo
lao kubwa ni kuridhika na walichokipata mwanzo. Pia wengi wanasahau kujipanga
upya na kuja kufanya vizuri katika kazi zake zote zinanazokuja.
Tupo baadhi ya wafanyabahara huwa tunaridhika
na kuona kile tunachokipata kama ni faida kubwa. Jambo la msingi na la
kuzingatia ni kwamba hicho ulichonanacho usiridhike nacho na kujiona wewe ni mkamilifu na kinatosha, la
hasha bali jione una mapungufu kwa kuzitambua njia mbalimbali za kuweza
kuongeza thamani katika biashara na kazi zingine unazofanya.
Tukumbuke ya kwamba ili kuyaona mafanikio katika
kila shughuli ambazo tunazifanya ni kwamba tujione ya kwamba vitu hivyo
vinatudai kwa maana ya kwamba tusiridhike na kuona vinatosha hapo vilipo. Leo
hii mtu aliyegundua ndege haridhiki na ndege amabayo ameigundua bali anafikiria
kitu kingine ambacho atakiongeza katika ndege ili kuongeza ubora au anafikiria
kitu kingine zaidi ya ndege.
Kama ndivyo hivyo hata wewe katika jambo
lolote ambalo unalifanya lazima ufikirie hivyo. Usiridhike na ulichonacho bali fikiria ni nini
unakihitaji zaidi ili kuongeza thamani katika jambo ambalo unalifanya. Kuwa mtu
ambaye ni mbunifu ambaye utatofautiana na wengine. Endapo utayafanya hayo kwa njia tofauti na
zile ambazo umezizoea utakuwa tofauti sana na watu wengine na ndoto zako
zitazidi kung’ara mara dufu.
Daima tukumbuke ya kwamba wewe ndiye mmiliki
wa mafanikio yako, hivyo una uwezo mkubwa wa kuyafanya mafanikio hayo yakuwe au
yafe. Kitu cha msingi ili kukuza biashara
au jambo lolote ni kuamua tu na
kuvifanya mambo kwa njia na tofauti ulizozioa .
Makala
imeandikwa na; Benson chonya
Simu;
0757-909942
Mar 29, 2016
Fursa Za Biashara Na Miradi Ambazo Unaweza Kuzifanya Kulingana Na Mtaji Ulionao.
Mara nyingi kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO tumekuwa tukikushirikisha mbinu mbalimbali
pamoja na fursa ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa. Lakini pamoja
na mbinu hizo ambazo waandishi wetu wamekuwa wakizitoa bado tumekuwa tukipokea simu
nyingi zinazouliza ‘Nifanye nini au
nifanye biashara gani’.
Kwa kujua umuhimu wa hilo, leo katika makala yetu ya leo, DIRA YA MAFANIKIO itakushirikisha aina tofauti tofauti ya miradi ambayo unaweza
kuifanya kulingana na eneo ulipo hasa kwa kuangalia urahisi wa utekelezaji
unaona kwako unafaa. Kwa kupitia makala haya, tunaamini utakuwa umejifunza kitu
na itakusaidia kukupa mwongozo wa kujua ni nini cha kufanya kitakachokupa
mafanikio makubwa.
Bila kukupotezea muda, twende pamoja kujifunza aina mbalimbali
ya miradi ambayo unaweza kuifanya kulingana na eneo ulipo.
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika halmashauri,
Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya elektroniki na
mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel,
Tally, Myob,
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo
za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe,
Kuku, Bata, na wengine.
UFUGAJI WA NYUKI KWA KISASA. |
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa
mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na
kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia
mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya
sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na
landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme,
duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery,
inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs,
Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy
TV, TNG, Digitech, Continental.
51.Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na
wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na
tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na
mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na
televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na
mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana
mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani
mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na
kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua.
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo.
Chukua hatua na PIGA KAZI mpaka ufikie mafanikio makubwa lakini
kama yote haya umeshindwa kupata la kufanya wewe utakuwa ushapotea, endelea na
utaratibu wako wa kuilaumu serikali.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio mkubwa na
endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Kwa maswali au ushauri unaweza kuwasilina nasi kwa dirayamafanikio@gmail.com au simu
kwenda 0713 0480 35, karibu sana.
Mar 28, 2016
Mambo Mawili (2) Yanayotukwamisha Kufikia Malengo Yetu.
Yapo mambo mengi ambayo umekuwa ukiyaona au
kuyasikia ambayo yanakufanya usonge mbele au kurudi nyuma katika safari yako
mafanikio. Jambo la msingi ni jinsi gani
ambavyo unachukulia mambo hayo katika
kuoziona fursa katika eneo lako unaloishi. Lakini katika makala ya leo tunakwenda kujikita
zaidi kwa kuangalia mambo ambayo yanatufanya tuzidi kuwa wanyonge na kuona
mafanikio ni ya watu wachache.
Yafuatayo
ni baadhi ya mambo yanayotukwamisha kufika malengo.
JAMBO
LA KWANZA.
Kusemwa
na watu juu ya jambo lako. Tunashindwa kufika malengo makubwa kwa sababu
, sisi wenyewe ni kikwazo katika baadhi ya mambo ambayo hayana msaada wowote wa kimafanikio
kwa watu wengine. Wapo baadhi ya watu wapo kwa ajili ya kuona watu wengine hawasogei mbele kimafanikio . Wao wamekuwa na maneno ya kuwakatisha watu
wengine tamaa kwa kuwaambia wahusika maneno ambayo hayawajengi bali
yanawarudisha nyuma. Mfano leo hii anamwambia mtu unataka kufanya biashara fulani,
mtu huyo atakwambia hataweza kufanya jambo hilo kwa kuwa hufanani na kitu hicho
unachotaka kufanya.
Wapo baadhi ya watu ukiwashirikisha mambo yako
wao huchukua hatua ya kuwashirikisha watu wengine na kuwambia fulani anataka kufunya jambo fulani. Lakini
jambo la msingi la kuzingatia ili kuona unapata faida katika jambo lako
unalofanya hakikisha maneno ya watu wanayokusema yanakupa hamasa za kiutendaji
na kuongeza juhudi ili kupata faida kubwa.
JIAMINI KWA KILE UNACHOKIFANYA. |
Mfano wewe ni mfanyabiashara watu wanakusema
wewe unafanya biashara kwa njia za ushirikina au maneno mengine yanayofanana na
hayo achana na maneno hayo bali songa mbele kwa kuziona fursa za jambo lolote
ili kupata faida kubwa. Watu wanapozidi kukusema wewe unazidi kufanikiwa zaidi.
JAMBO
LA PILI
Kusubiri
kuambiwa ufanye jambo fulani. Hili
ni jambo linalotukwamisha sana katika safari ya mafanikio. Watu wengine
tunapenda kufanya mambo ya kimafanikio kwa kuambiwa na mtu mwingine. Wengi tunasubiri
kuambiwa fanya hiki au fanya kile. Katika safari ya mafanikio ukisubiri kuwaambiwa na mtu fanya hiki au
fanya kile kwa upande wako mafanikio yatakuwa ni ndoto tu.
Mfano wewe ni mwanafunzi unasubiri mwalimu wako
mpaka akuambie kasome kitu fulani au wewe ni mfanyabiashara unasubiri mtu
akwambie boresha ofisi yako ili kuongeza wateja ila wewe kwa akili yako hata siku moja
hujawahi kujipa kazi za kufanya au kujiuliza ufanye nini ili kuboresha biashara.
Kimsingi kufanya hivi ni sawa na kumfunika nyoka kwenye tenga ili asitoke.
Ewe msomaji wa makala haya ili kuona
unafanikiwa kwa kiwango kikubwa hakikisha kwa kila jambo unalolifanya usisibiri
mtu fulani akwambie ufanye bali kuwa na
akili ya kujiongeza. Kufanya hivi kutakufanya kuongeza ufanisi wa kiutendaji na
kupata kile unachokihitaji.
Ansante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO na endelea
kuwashirikisha wengine kujifunza zaidi.
Simu;
0757-909942
Email ; Bensonchonya23@gmail.com
Mar 25, 2016
Hizi Ndizo Fikra Chanya Za Kukusaidia Kufanikiwa.
Mafanikio siku zote mbali
na kufanya kazi kwa bidii yanahitaji uwe na fikra au imani chanya ili uweze
kufanikiwa. Kwa kuendelea kuwa na fikra au imani sahihi inakupelekea kufikia mafanikio makubwa. Baadhi
ya imani unazotakiwa kuwa nazo ili kujijengea mafanikio ni kama hizi zifuatazo:-
1. Amini kwamba pamoja na
kushindwa kwako sana lakini una uwezo mkubwa wa kufanikiwa lakini ikiwa
utajaribu tena na tena kile unachokitaka kwenye maisha yako.
2. Amini kwamba unatakiwa
kufanya mambo yako kwa utofauti kama unataka kufika hatua fulani kimaisha. Acha
kuishi kimazoea sana utakwama.
3. Amini ndani yako unao uwezo
wa kufanya kitu chochote cha kukupa mafanikio ikiwa lakini utaamua iwe hivyo.
Ukichukua hatua hali yoyote utaibadilisha.
4. Amini kufanya kazi kwa
bidii ni njia pekee ya kukutoa kwenye umaskini. Kama unafikri natania angalia
watu wengi ambao wanafanya kazi sana lakini huku wakikubali kujifunza. Maisha yao
ni ya mafanikio makubwa.
5. Amini muda ulionao ndio
unaouwezo wa kukufanya ukawa maskini au tajiri. Itatokea hivyo kwako kwa
kupanga matumizi mazuri ya muda wako.
KUWA NA MAWAZO CHANYA. |
6. Amini kuwa mbali na
watu hasi ni njia mojawapo ya kukusaidia kufikia malengo yako.
7. Amini kwamba wewe ndiye
unayeyajibika kwa maisha yako. Kwa vyovyote vile maisha yako yalivyo wewe ndiyo
chanzo kikubwa cha kwanza hakuna wa kumlaumu.
8. Amini kuwa mshindani
mkubwa wa kwanza wa maisha yako ni wewe. Unatakiwa kuwa bora kuliko jana kila
siku.
9. Amini una uwezo mkubwa
wa kujifunza kitu chochote na ukaweza. Unaweza kujifunza mafanikio, biashara au
chochote kile unachokitaka.
10. Amini una uhuru wa
kuchagua maisha yako yawe vipi. Kama unataka maisha yako yawe ya mafanikio
makubwa huo ni uchaguzi wako au kama unataka maisha yako yawe ya kawaida pia
huo ni uamuzi wako.
Ansante kwa kujifunza na
endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
E-mail;
dirayamafanikio@gmail.com
Simu; 0713 04 80 35,
Mar 24, 2016
Vipindi Muhimu Anavyopitia Mwanadamu Katika Maisha.
Katalamu binadamu katika safari
ya ukuaji hupitia vipindi mbalimabali. Katika vipindi hivyo binadamu kwa muda
mwingine huwa na furaha,huzuni,wasiwasi na hofu pia. Pia ni hivi ndivyo vipindi
ambavyo humsaidia kujifunza mambo mabalimbali ikiwa pamoja na tabia na
mafanikio.
Hebu twende pamoja kujua na
kujifunza Vipindi hivyo ni;
Umri
wa mwaka (0-18).
Katika kipindi hiki binadamu huwa
mtoto na anayependwa sana na wazazi wake, katika kipindi hiki mwanadamu anakua
katika kipindi cha kufundishwa vitu
kutoka kwa watu mbalimbali. Mfano mtoto mdogo katika hali kwa kila anachokifanya
kwake huona ni sawa eidha ni jema au baya.
Mzazi huchukua jukumu la
kemkekemea kama anafanya jambo baya na humpongeza pale anapofanya vizuri. Mfano
mtoto hupongezwa kumsaidia mzazi kufanya kazi, kuwaheshimu watu
wote, kufaulu katika masomo yake na mengineyo mengi. Kiujumla katika kipindi
hiki binadamu huwa ni tegemezi kwa jamii inayomzunguka.
Kipindi
cha umri kati miaka (19-35).
Katika kipindi hiki binadamu
huanza kujitambua yeye ni nani.Vilevile katika kipindi hiki ni kipindi ambacho
binadamu anaanza kupanga mipango mingi. Mfano katika kipindi hiki mtu huanza
kupanga mambo mbalimbali nataka katika maisha yangu kitu cha kwanza kuwa nacho
ni gari, mwingine utamsikia mimi nataka nianze kuwa na nyumba, wengine utasikia
nataka kuolewa na mtu mwenye pesa, wapo wengine utawasika nataka kuoa mwanamke
mzuri na mipango mingine mingi.
Katika kipindi hiki utawasikia wanasema ndio kipindi cha kula ujana wakiwa na
maana ya kwamba ni kipindi cha kwenda kumbi mbalimbali za burudani, pia ni
kipindi cha kupendeza, pia ni kipindi cha vijana wengi kujiingiza katika kuiga
mikumbo kutoka kwa watu mbalimbali hatimaye kujiingiza kwenye wizi,kuvuta
bangi,umalaya na mengineyo mengi. Utawasikia wengine wanakiita kipindi cha
tumia pesa ukuzoee.
VIPINDI VYOTE NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA. |
Dah yaani ni kipindi hiki kina
mambo mengi sana. Katika kipindi hiki tupo baadhi ya watu huwa bado wapo katika
kipindi cha utegemezi. Mfano mzuri ni wanafunzi wanasoma elimu za juu yaani
vyuo wao huamini ya kwamba hawawezi wenyewe kusimama na kujitengeneze njia
sahihi ya kujipatia kipato.Pia wanafunzi hawa kwa walio wengi huwa wanafikiri
maisha baada ya elimu zao ni kuajiriwa.
Lakini ndugu msomaji wa makala
hii lazima ufikiri zaidi kuajiriwa peke yake ili uweze kuona mafanikio makubwa
ndani yako. kitu kikubwa ni kuwa mbunifu.Wito wangu kwako ni kwamba endapo
utatumia vizuri kipindi hiki ukiwa na mtazamo chanya utapata mafanikio makubwa
sana.
Umri
kati miaka (36-45).
Ni aina nyingine ya vipindi
ambayo hupitia mwanadamu. katika kipindi hiki ni kipindi cha utekelezaji wa yale
uliyoyapanga katika kipindi ulichopita yaani cha miaka( 19-35). Katika kipindi
hiki ni kipindi ambacho kina majukumu
mengi ambayo yanamfanya mtu akose hata usingizi. Katika kipindi hiki mtu huwa
na majukumu mengi sana kwa mfano kujenga, kusomesha watoto,huenda ukawa tegemeo
katika familia yako.
Kwa kuwa katika kipindi hiki kina
mambo mengi ya utekelezaji ni vema kile unachokipanga katika kipindi cha
mipango yaani miaka (19-35) na utekelezaji uanza katika kipindi hicho. Nasema
hivi nikiwa na maana ya kwamba katika kipindi hiki cha miaka 36-45 watu wengi hujikuta wana mipango
mingi lakini ugumu unakuja katika utekelezaji.
Umri
kati ya miaka 46-na kuendelea
Hiki ni kipindi cha uzee ambacho
mara nyingi huiitwa ni kipindi cha masahihisho. Katika kipindi hiki baadhi ya
watu hupungua uwezo wa kufikiri hatimaye kuwa kama watoto. Pia Watu wengi hapa
hupatwa na magonjwa mbalimbali kama pressure,figo kufeli, kisukari na
mengineyo. Katika kipindi hiki watu hustaafu kazi zao. Katika kipindi hichi
watu wengi hupatwa na pressure kutokana na walishindwa kupanga na kutekeleza
mambo yao katika vipindi vya umri kati (19-35).
Mfano mtu alikuwa ni mfanyakazi
wa serikali na hajawahi kujenga nyumba yake ya kuishi wala hana usafiri vyote alivyokuwa anatumia
vilikuwa ni mali za ofisi. Inafika wakati wa kustafu anapata mafao yake ndo pale
anaanza kupanga mipango yake na kujikuta hela aliyopewa katika kiunua mgongo
imeisha kwa sababu mtu huyu anakuwa ana mipango mingi katika kipindi cha uzee
matokeo haelewi aanze na kipi katika
utekelezaji. Je, aanze na kununua gari? Je aanze na kufungua biashara? Je aanze
na kujenga nyumba? Matokeo yako mipango inakuwa mingi kuliko utekelezaji hatimaye
anapata pressure.
Wito wangu kwako kumbuka siku
zote kupanga ni kuchagua na kutenda ni
kuamua. Katika safari ya mafanikio kila linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe
kijana tambua ya kwamba muda wa kupanga na kutekeleza mambo yako ni sasa achana
na usemi eti kijana ni taifa la kesho kwa kuwa ukiushika usemi huo utakuwa unachelewa katika safari yako mafanikio.
DIRA YA MAFANIKIO inakutakia kila
jema katika safari yako ya mafanikio. Pia endelea kutembelea ukurasa huu kila siku ili ujifunze zaidi
kuhusu mbinu mbalimbali za mafanikio.
Imeandaliwa
na;
Afisa
mipango na maendeleo:Benson .O. Chonya,
Mawasiliano;
Simu;0757-909942/0652-015024
E-mail;bensonchonya23@gmail.com
Mar 23, 2016
Siri 15 Za Kukabiliana Na Changamoto Za Soko Katika Biashara.
Watu wengi wanafanya biashara, kulima
au kuzalisha mali kwa lengo la kutafuta pesa na maisha mazuri. Lakini je, mteja
wetu tunaemzalishia ni nani? Na kile tunachokizalisha kinatupa soko la uhakika?
Mara nyingi soko ni tatizo kubwa sana kwa wazalishaji iwe wadogo au wakubwa. Na
hili ndilo tatizo kubwa linalosababisha kutokufanikiwa katika biashara au
shughuli zetu.
Soko ndio kila kitu katika biashara
yeyote ile. Bila soko hakuna biashara na bila biashara hakuna soko. Kama
nilivyosema hapo awali tatizo au changamoto kubwa aliyonayo mkulima,
mfugaji,mjasiriamali,mfanyabiashara mdogo na mfanya biashara mkubwa ni soko. Kwa
nini tatizo ni soko? Tulia mzee wa nyundo nikupe
uhondo leo.
Mara nyingi soko linakuwa ndio tatizo
na changamoto kubwa kwa watu wote
wanaofanya biashara kwa sababu kuu zifuatazo:
1.Kutegemea wateja wale wale
kwa wafanyabiashara wote.
2.Kuzalisha bidhaa zinazofanana kwa
wazalishaji wote kama ni mchele ni huo huo wa mbeya na morogoro unafanana
tofauti tunaitengeneza walaji tu ila bidhaa ni ileile.
3. Kutumia mbinu zilezile za kizamani
katika kuuza bidhaa hakuna uboreshwaji katika ufungaji au upangaji.
4. Soko ni tatizo kwa sababu watu
wengi hawana elimu ya biashara hukurupuka tu kwa kuambiwa na rafiki au kusikia
biashara fulani inalipa.
5.Watu wengi hawafanyi utafiti wa soko
la bidhaa wanazozalisha huamini nitawapata tu wateja madamu mzigo au mali
ninayo na hivyo kujikuta wakipata hasara na kufilisika.
FANYA UTAFITI WA SOKO KABLA HUJAFANYA BIASHARA |
6. Watu wengi hufuata mkumbo kwa
kufanya biashara kwa kuona jirani au rafiki yake kafanikiwa naye hujidumbukiza
bila kutafiti alianzaje? Hizo ndizo sababu za kwa nini soko ni changamoto au
tatizo katika biashara.
Ni kwa namna gani tunaweza kutatua
hizi changamoto za Soko?
Sasa twende pamoja nikupe siri 15 za
kukabiliana na changamoto au tatizo la soko katika bidhaa, huduma na mali
unazozalisha.
1. Lazima ufanye utafiti wa kutosha
juu ya uhakika wa soko la bidhaa zako au biashara nje na ndani kabla ya kuanza kuifanya biashara hiyo.
2. Ni lazima ujue uhitaji wa bidhaa au
huduma ya biashara yako ni ya msimu au ya muda wote.
3. Ni lazima ujue wateja wako ni wa
aina gani katika kipato chao, kipato cha juu, cha kati au cha chini kabisa ili
ikupe uhuru wa kupanga bei.
4. Ni lazima ujue ni muda gani
wanahitaji huduma yako.
5. Ni lazima ujue gharama za
uzalishaji, usafiri, na faida ama posho yako kabla ya kufanya biashara yako
vinginevyo utaambulia hasara.
6. Ni lazima uwe na taarifa sahihi
muda wote kuhusu soko kushuka au kupanda.
7. Ni lazima ujue uwezo wa
washindani wako kibiashara ili ujue namna ya kukabiliana nao kiushindani katika
soko.
8. Ni lazima uwe na lugha nzuri kwa
wateja wako
9. Ni lazima uwe mbunifu kwenye
biashara yako ili kuwavutia wateja wapya na wa zamani.
10. Ni lazima utengeneze network ya
watu wazuri wa kushirikiana nao katika biashara yako.
11. Ni lazima uzalishe bidhaa na
uuze bidhaa zenye ubora na sio bora bidhaa.
12. Ni lazima wakati mwingine
uzalishe bidhaa zako kwa ‘order’ usizalishe
ilimradi tu unaweza kuzalisha na kwenda kuweka sokoni ukimsubiri mteja ambaye
huna maagano naye kama atakuja ama laa.
13.Tengeneza utaratibu wa kumsogezea
huduma mteja wako ikiwezekana mpelekee hadi nyumbani kwake ili kumteka akili
yake na kumtoza gharama ya usumbufu kijanja bila yeye kujua.
14.Tengeneza utaratibu wa kuwa na
mawasiliano na wateja wako na kuwapigia simu kwa lengo la kuchukua ‘order’ za
siku inayofuata.
15. Wape motisha wateja wako ili
kuwavutia wadumu kwako na kukuletea wateja wengine.
Asante kwa kunifuatilia ubarikiwe
sana ni mimi mshirika wako katika mafanikio na siri za mafanikio Shariff
H.Kisuda alimaarufu mzee wa nyundo kali.
Karibu na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)