Mar 21, 2016
Mambo (5) Ya Kuyatazama Ili Kuongeza Thamani Katika Biashara.
Huenda ukawa anafanya biashara au unapenda
kufanya biashara lakini yapo baadhi ya mambo ya msingi ya kuyatazama kabla au wakati wa kufanya biashara. Tupo baadhi
yetu tunashindwa kufikia malengo yetu hasa katika kuwaza au tunapofanya
biashara. Leo katika makala haya nitakwenda kukueleza juu ya kujijengea misingi
ili kukuza na kuongeza uthamani wa
biashara.
Biashara yoyote ile endapo itafanywa kwa
misingi ambayo inafaa itakuwa na faida sana. Zipo baadhi ya biashara hazikui
kwa sababu ya kuzifanya biashara hizo
miaka yote kwa staili moja. Kama kweli unataka kukuza biashara yako ni lazima
utazame ni kwa jinsi gani unaweza kubadilisha mfumo wa kiutendaji ambao
utakufanya uweze kupata faida zaidi.
Biashara hata kama itakuwa ndogo au kubwa kiasi gani endapo utaifanya kwa
ubunifu na umakini wa hali ya juu utaongeza wateja zaidi.
Yafuatayo
ndio mambo ya msingi ya kuongeza uthamani wa biashara ili kuongeza wateja
zaidi;
1. ladha
na fasheni.
Kimsingi kuna baadhi ya watu huwa tunafanya
biashara tu bila kuangalia vitu kama
vile ladha au fasheni (mitindo
inayokwenda na wakati) . Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikupe mfano, kama wewe
unafanya biashara angalia wateja wako wanakula au wanakunywa kwa sababu ya
kukidhi mahitaji au kwa sababu wanaridhika na kile wanachokula au kunywa. Kama
wewe unafanya biashara nyingine kama vile, nguo, viatu, magari, vitu vya ujenzi
vitu vingine ni lazima uangalie vitu vinavyokwenda na wakati , kwani endapo
utafanya hivyo ndivyo vitavyokufanya uongeze wateja. Tukumbuke ya kuwa kadri
vitu vinavyokuwa vya fasheni ndivyo wateja wanavyozidi kuwa wengi.
WEKA LADHA NA FASHENI KWENYE BIASHARA YAKO. |
2. Kipato cha wateja.
Katika kutazama ni vipi unaweza kuongeza
uthamani wa biashara jambo la msingi ni kujua kipato cha wateja wako. Kama eneo ambalo unaishi wateja wako
wanaoishi ni watu wa kipato cha kawaida ni lazima ujue ya kuwa bidhaa na bei
lazima vilingane na wateja wako mfano huwezi kwenda kuanzisha biashara ya super
market kijijini. Pia tukumbuke ya kuwa kuna baadhi za bidhaa endapo bei
zitakuwa chini ndio huwa zinawateja wengi zaidi, halikadhalika kama wateja wako
ni watu wa kipato cha juu basi bidhaa na bei ya bidhaa zako ni lazima yakidhi
mahitaji ya watu hao kwa namna moja au nyingine.
3. Uhitaji wa bidhaa.
Katika biashara ni lazima uangalie uhitaji wa
bidhaa au huduma kwa wateja wako. Kanuni za kibiashara zinasema kwamba kama
bidhaa zina gharama ndogo za uuzaji na uhitaji
wa wateja hua mkubwa sana na kinyume chake inawezekana pia. Pia ni lazima usome
soko lako kwa maana ya kuangalia wateja wako wanahitaji nini, na ujalibu kuchua
mahitaji yao na kuwahudumia bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji yao.
4. Matangazo.
Matangazo kuhusiana na jinsi ya upatikanaji na
matumizi ya bidhaa au huduma husika. Ili kuwavutia wateja juu ya biashara yako
ni vyema kuitangaza bidhaa yako ili kuwafanya wateja waweze kuitambua biashara ambayo
unaifanya. Katika kuitambulisha bidhaa katika matangazo ni lazima uwe mbunifu
ili tangazo linapomfikia mtumiaji ahisi yeye ni sahemu ya biashara hiyo kwa
maana ya kwamba mtumiaji aseme bila bidhaa hawezi kuishi.
5. Hali ya hewa.
Biashara yeyote ni lazima ujue ni kipindi gani
bidhaa yako itauzika zaidi. Biashara zingine ni za msimu kwa mfano kama unauza
miamvuli najua utaifanya kwa nguvu zaidi kipindi cha mvua. Hivyo kwa kuwa wewe ndo unataka kuifanya biashara au umekwisha kuanza
biashara ni lazima uzingatie je biashara yako
itauzika zaidi msimu gani? Ukizingatia hayo, biashara yako itakuwa ni
yenye faida kubwa sana.
Kama unataka kufanya biashara au unafanya
biashara na unataka kupata faida kubwa ni lazima uzingatie hayo kwa namna moja
ama nyingine.
Tunakutakia mafanikio mema katika biashara
yako. Pia endelea kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia DIRA YAMAFANIKIO kwa kupata maarifa bora zaidi.
Makala hii imeandikwa na Afisa mipango na maendeleo Benson
Chonya
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.