Mar 4, 2016
Mambo Matatu (3) Ya Kufanya Pale Unapoona Mipango Yako Haiendi Vizuri.
Katika
maisha ya kutafuta mafanikio, mara nyingi kila mtu hupenda sana mipango yake imuendee
vizuri kila siku. Lakini hata hivyo pamoja na nia hiyo, kiuhalisia bado kuna
wakati mambo yanakuwa hayaendi sawa kama inavyotarajiwa. Hapo ndipo changamoto
na kuanza kukata tamaa huanza kujitokeza kwa wengine.
Jambo
la msingi la kujiuliza je, unapokabiliana na changamoto ama kuona mipango yako
haiendi sawa kama ulivyopanga ni hatua zipi ambazo huwa unachukua? Kwa kawaida,
ni lazima uchukue hatua za kukusaidia kwenda mbele, na si kukurudisha nyuma. Kwa
kusoma makala haya utaelewa hatua za kuchukua pale mipango yako inapokwendea
hovyo.
1. Weka nguvu zako nyingi kubadili
hali hiyo.
Kuendelea
kuishi jana na huku ukiwa ukiwaza sana pale ulipokosea kwenye mipango yako haitakusaidia
sana. Kitu cha kufanya sasa ni kuweka nguvu zako zote kwa yale mambo
unayoyataka kuyabadilisha. Mambo ya jana au mipango ya jana iliyokuwa inaenda
vizuri haipo tena kilichobaki kwako ni historia tu na sasa unatakiwa kuibadili.
Tuchukulie
kwa mfano kwenye biashara yako ulikuwa
na wateja wengi sana ambao kwa sasa huna. Kiuhalisia hapa, ili uweze
kuwarudisha wateja hao kwako kwanza unatakiwa kujua tatizo ni nini lililosababisha
ukose wateja. Baada ya hapo weka nguvu zako nyingi kuibadili hali hiyo. Kama
utakuwa una mtafuta mchawi, badala ya kutafuta njia utakuwa unajipotezea muda.
PANGA MIPANGO YAKO UPYA TENA. |
2. Panga mipango yako upya tena.
Inapotokea
mipango yako haijaenda sawa hiyo isiwe ‘tiketi’
ya kukufanya ukaamua kuacha kila kitu. Hapo sasa ndipo unatakiwa kujipanga upya
na kupanga mipango yako upya tena. Kushindwa kwako isiwe hapo ndio mwisho. Kaa
chini na fikiri upya juu ya kupanga mipango yako upya tena na tena.
Hata
wale watu wenye mafanikio makubwa, hawakufanikiwa mara moja kama unavyofikiri.
Walishindwa kwa namna moja au nyingine, lakini kilichowasaidia walijipanga tena
hadi kufikia makubwa. Chochote ukifanyacho kama hakiendi sawa, jipange tena
kukifanya kwa upya. Hiyo itakuwa ni msaada mkubwa sana kwako.
3. Tafuta msaada wa kukutoa hapo
ulipo.
Ni
kweli unaweza ukawa kila ukiangalia mipango yako haiendi sawa kama ambavyo
unavyotaka iwe. Utakuta umejaribu hili na lile lakini wapi, unaona kama haisadii.
Kitu cha kufanya sasa inabidi ukubali na utafute msaada wa kukutoa hapo ulipo.
Msaada huu utaupata kwa wengine waliopitia hali kama yako.
Hapo
ulipo jaribu kuangalia au kufikiria ni nani unayeweza ukawa unamfahamu aliwahi
kupita kwenye wakati mgumu kama wako. Ukimpata mtu wa namna hiyo mfuate akupe
mikakati ya kipi cha kufanya. Acha kung’ang’ana mwenyewe sana kutafuta suluhu.
Jichanganye na wengine wakupe mawazo mapya ya kukusaidia.
Kwa
kifupi, hayo ndiyo mambo matatu unayoweza ukayafanya hasa pale unapohisi kwamba
mipango na malengo haiendi sawa.
Nikutakie
siku njema na uwe na mafanikio mema.
Ni
wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.