Mar 18, 2016
Namna Unavyoweza Kuondoa Mawazo Hasi Katika Maisha Yako.
Mwanadamu
ni kiumbe ambaye amepewa uwezo mkubwa sana wa kufikiri. Na katika uwezo huo
huwa mara nyingi anakuwa ana mawazo chanya na mawazo hasi. Mimi na wewe kwa
namna moja au nyingine huwa ni watu wa kutumia mawazo haya, yawe chanya au hasi
lakini tunakuwa nayo.
Kila
siku tunavyoishi huwa tunakuwa na mawazo mengi sana kwani akili ya mwanadamu
huwaza kila dakika. Hebu fikiria sasa hivi na jaribu kuandika mawazo yako
ambayo unafikiria kwa takribani kila siku. Mangapi kati ya mawazo hayo huwa ni
hasi? Naweza kusema kwamba asilimia kubwa ya watu wengi, mawazo yao ni hasi.
Naamini utaniunga mkono katika hili.
Je,
unajua kwamba mawazo yetu yana nguvu kubwa sana ya ajabu na pia yana uwezo kwa
asilimia kubwa sana kubadili maisha yetu. Akili inaweza ikawa ni kitu kigumu sana
kukimiliki na kukitawala kama usipokuwa makini. Lakini unapoongeza umakini katika
kuitumia akili yako, itakusaidia kufanikisha mipango yako mingi iliyokwama.
Siku
zote ukitaka kuwa mchezaji mzuri ni lazima ufanye mazoezi sana. Hivyo basi hata
ukitaka ubongo wako kufikiri chanya ni lazima uufanyishe ubongo wako mazoezi
mengi sana ya kutosha. Hiyo itasaidia ubongo wako kufikiri kutoka hasi na kuanza
kufikiri chanya.
FANYA TAHAJUDI AU SALA KUTOA MAWAZO HASI. |
Kwanini
ni muhimu sana kuondoa mawazo hasi? Hiyo yote ni kwa sababu mawazo hasi ni
kizuizi kikubwa cha kufikia mafanikio yako. Kama ukitaka kuacha kufikiria
mawazo hasi kuna njia ambazo unaweza kuzitumia na ukaweza kufikia malengo yako.
Kwanza, soma vitu vya kukufanikisha.
Dunia
ya leo ina kelele nyingi sana ambazo ni hasi na hazina maana wala msaada sana
kwako. Ili uweze kutoka huko ni muhimu kwako kujilisha au kusoma vitu vya kukufanikisha.
Hapa unaweza ukasoma vitabu, majarida ya mafanikio au hata ukahudhuria semina.
Usikubali
kukaa kienyeji enyeji, poteza fedha zako kwenye kununua au kusoma vitabu
mitandaoni ambavyo vinaweza kukusaidia kukuongeza uwezo wako wa kufikiri
chanya. Kwa kujijengea mawazo chanya
itakupelekea wewe mwenyewe kufikia ndoto zako.
Pili, fanya tahajudi(Sala).
Wakati
mwingine mawazo hasi yanakuwa sio rahisi sana kuondoka mpaka ufanye tahajudi au
sala. Hili ni tendo ambalo unaweza ukawa unalifanya kila siku. ‘Kumediteti’
hakuhitaji nguvu kubwa sana, inaweza ikawa rahisi sana na ukafanikiwa kuondoa
mawazo hasi.
Unapoanza
kutaka kufanya tahajudi au ‘meditation’
funga macho yako, wakati huo huo unavuta pumzi taratibu huku ukiwa umetulia
kimya ukitafakari hali unayotaka ikutokee. Unapofanya hivi kwa muda utajikuta
unapata majibu na kufanikisha malengio kwa sababu unachukua muda kuuongoza
ubongo wako.
Tatu, andika mawazo mazuri.
Baada
ya kuhisi kuwa una mawazo chanya yanaanza kuleta mwamko wa mafanikio, unaweza
ukawa na kitabu cha kumbukumbu zako( Diary)
na ukaamua kuyaingiza yale mawazo unayayona ni mazuri na yanaweza kuleta
mabadiliko mara moja.
Zoezi
hili la kuandika mawazo mazuri litakusaidia sana kupunguza mawazo hasi katika
akili yako na kwa kuanzia hapo utaupa uwezo ubongo wako kuwaza mawazo chanya na
yenye mafanikio kwa upande wako.
Nne, usikate tamaa.
Hata
inapotokea unaona mawazo yako hasi kama hayatoki na bado yapo, jifunze
kutokukata tamaa mapema. Amini mawazo yako hayo yataanza kutoka polepole. Kitu
kikubwa uwe una nia ya kuamini kwamba ni lazima utakuwa una mawazo chanya muda
sio mrefu.
Ni
matumaini yangu ya kwamba utatumia njia hizo katika kukusaidia kukupa mawazo
chanya yenye manufaa kwako na kitaifa pia. Pia usisahau kumwomba Mungu
akusaidie.
Shukrani za pekee zimwendee Nickson Tarimo kwa kutushirikisha makala haya, kumbuka endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza zaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.