Mar 23, 2016
Siri 15 Za Kukabiliana Na Changamoto Za Soko Katika Biashara.
Watu wengi wanafanya biashara, kulima
au kuzalisha mali kwa lengo la kutafuta pesa na maisha mazuri. Lakini je, mteja
wetu tunaemzalishia ni nani? Na kile tunachokizalisha kinatupa soko la uhakika?
Mara nyingi soko ni tatizo kubwa sana kwa wazalishaji iwe wadogo au wakubwa. Na
hili ndilo tatizo kubwa linalosababisha kutokufanikiwa katika biashara au
shughuli zetu.
Soko ndio kila kitu katika biashara
yeyote ile. Bila soko hakuna biashara na bila biashara hakuna soko. Kama
nilivyosema hapo awali tatizo au changamoto kubwa aliyonayo mkulima,
mfugaji,mjasiriamali,mfanyabiashara mdogo na mfanya biashara mkubwa ni soko. Kwa
nini tatizo ni soko? Tulia mzee wa nyundo nikupe
uhondo leo.
Mara nyingi soko linakuwa ndio tatizo
na changamoto kubwa kwa watu wote
wanaofanya biashara kwa sababu kuu zifuatazo:
1.Kutegemea wateja wale wale
kwa wafanyabiashara wote.
2.Kuzalisha bidhaa zinazofanana kwa
wazalishaji wote kama ni mchele ni huo huo wa mbeya na morogoro unafanana
tofauti tunaitengeneza walaji tu ila bidhaa ni ileile.
3. Kutumia mbinu zilezile za kizamani
katika kuuza bidhaa hakuna uboreshwaji katika ufungaji au upangaji.
4. Soko ni tatizo kwa sababu watu
wengi hawana elimu ya biashara hukurupuka tu kwa kuambiwa na rafiki au kusikia
biashara fulani inalipa.
5.Watu wengi hawafanyi utafiti wa soko
la bidhaa wanazozalisha huamini nitawapata tu wateja madamu mzigo au mali
ninayo na hivyo kujikuta wakipata hasara na kufilisika.
FANYA UTAFITI WA SOKO KABLA HUJAFANYA BIASHARA |
6. Watu wengi hufuata mkumbo kwa
kufanya biashara kwa kuona jirani au rafiki yake kafanikiwa naye hujidumbukiza
bila kutafiti alianzaje? Hizo ndizo sababu za kwa nini soko ni changamoto au
tatizo katika biashara.
Ni kwa namna gani tunaweza kutatua
hizi changamoto za Soko?
Sasa twende pamoja nikupe siri 15 za
kukabiliana na changamoto au tatizo la soko katika bidhaa, huduma na mali
unazozalisha.
1. Lazima ufanye utafiti wa kutosha
juu ya uhakika wa soko la bidhaa zako au biashara nje na ndani kabla ya kuanza kuifanya biashara hiyo.
2. Ni lazima ujue uhitaji wa bidhaa au
huduma ya biashara yako ni ya msimu au ya muda wote.
3. Ni lazima ujue wateja wako ni wa
aina gani katika kipato chao, kipato cha juu, cha kati au cha chini kabisa ili
ikupe uhuru wa kupanga bei.
4. Ni lazima ujue ni muda gani
wanahitaji huduma yako.
5. Ni lazima ujue gharama za
uzalishaji, usafiri, na faida ama posho yako kabla ya kufanya biashara yako
vinginevyo utaambulia hasara.
6. Ni lazima uwe na taarifa sahihi
muda wote kuhusu soko kushuka au kupanda.
7. Ni lazima ujue uwezo wa
washindani wako kibiashara ili ujue namna ya kukabiliana nao kiushindani katika
soko.
8. Ni lazima uwe na lugha nzuri kwa
wateja wako
9. Ni lazima uwe mbunifu kwenye
biashara yako ili kuwavutia wateja wapya na wa zamani.
10. Ni lazima utengeneze network ya
watu wazuri wa kushirikiana nao katika biashara yako.
11. Ni lazima uzalishe bidhaa na
uuze bidhaa zenye ubora na sio bora bidhaa.
12. Ni lazima wakati mwingine
uzalishe bidhaa zako kwa ‘order’ usizalishe
ilimradi tu unaweza kuzalisha na kwenda kuweka sokoni ukimsubiri mteja ambaye
huna maagano naye kama atakuja ama laa.
13.Tengeneza utaratibu wa kumsogezea
huduma mteja wako ikiwezekana mpelekee hadi nyumbani kwake ili kumteka akili
yake na kumtoza gharama ya usumbufu kijanja bila yeye kujua.
14.Tengeneza utaratibu wa kuwa na
mawasiliano na wateja wako na kuwapigia simu kwa lengo la kuchukua ‘order’ za
siku inayofuata.
15. Wape motisha wateja wako ili
kuwavutia wadumu kwako na kukuletea wateja wengine.
Asante kwa kunifuatilia ubarikiwe
sana ni mimi mshirika wako katika mafanikio na siri za mafanikio Shariff
H.Kisuda alimaarufu mzee wa nyundo kali.
Karibu na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.