Mar 30, 2016
Chanzo Kikubwa Kinachokufanya Usitimize Ndoto Zako.
Kuna baadhi ya watu wanazitambua njaa zao na wengine hawazitambui njaa zao za mafanikio.
Njaa hizo za mafanikio zinatofautiana
baana ya mtu mmoja na mwingine. Nimesema ni baadhi ya watu wachache ndio watu
ambao wanajishughulisha usiku na mchana ili kuangalia ni mbinu zipi wanaweza
kuzitumia ili waweze kufanikiwa. Lakini
watu hao wenye njaa ya mafanikio, mambo yao wakati wa kuyasaka mafanikio huwa
ni mateso ya hapa na pale.
Watu hawa huzunguka huku na huko ili kupata
maisha bora. Watu hawa naweza nikawaona ni watu ambao huwa wana sura za huzuni
zaidi ila furaha huchukua kwa kiwango kidogo sana katika maisha yao. Wapo
baadhi ya watu kutokana na njaa walinazo kila kazi yeyote yupo tayari kuifanya.
Ila tatizo linakuja ni kwamba pindi apato fursa ya kufanya kazi wengi wao
wanapweteka na kutoonesha njaa walizokuwa nazo mwanzo pindi wapatapo nafasi ya
kufanya kazi. Hivyo katika makala ya leo nataka nikushirikishe kwa nini watu
hao huwa hivyo.
Hii ndio sababu kubwa kwa nini watu wengi
hawatumii nafasi walizozipata kwa asilimia mia moja;
Kuridhika
na walichonacho.
Tafiti zinaonesha ya kwamba asilimia kubwa ya
watu wakipata kile walichokuwa wanakihitaji hawakifanyi kwa asilimi mia moja.
Hii ni kutokana mtu anaona kitu hicho ameshakipata hivyo hana haja tena na
kuanza kuendelea kuongeza juhudi na ubunifu katika kitu au jambo fulani.
Kimsingi ni kwamba binadamu ni watu wa kulalamika sana nasema hivi nikiwa na maana
ya kwamba leo hii ukikutana na mtu ambaye hana ajira au hafanyi biashara ni mtu
wa kulalamika sana, na asilimia kubwa la kundi hili wengi wao husema nikija
kupata kazi au nikija kufanya biashara nitafanya vizuri ili kutumiza ndoto
zangu. Ila tazizo maneno hayo hugeuka dakika chache akilipata jambo hilo
hafanyi kama alivyoahidi mwanzoni wakati wa akilitafuta jambo hilo.
USIRIDHIKE SANA NA KILE UNACHOKIFANYA. |
Mfano leo hii tunaona baadhi ya wasanii wa
nyimbo wanapotea katika sanaa, hii mara
tu baada ya kutoa wimbo mmoja ambao utapendwa na watu wengi. Tatizo kubwa wengi wao huwa wanaridhika na
mapokeo ya wimbo huo na kupweteka na kujiona tayari wameshafanikiwa na mwisho wa siku hatuwasikii tena. Tatizo
lao kubwa ni kuridhika na walichokipata mwanzo. Pia wengi wanasahau kujipanga
upya na kuja kufanya vizuri katika kazi zake zote zinanazokuja.
Tupo baadhi ya wafanyabahara huwa tunaridhika
na kuona kile tunachokipata kama ni faida kubwa. Jambo la msingi na la
kuzingatia ni kwamba hicho ulichonanacho usiridhike nacho na kujiona wewe ni mkamilifu na kinatosha, la
hasha bali jione una mapungufu kwa kuzitambua njia mbalimbali za kuweza
kuongeza thamani katika biashara na kazi zingine unazofanya.
Tukumbuke ya kwamba ili kuyaona mafanikio katika
kila shughuli ambazo tunazifanya ni kwamba tujione ya kwamba vitu hivyo
vinatudai kwa maana ya kwamba tusiridhike na kuona vinatosha hapo vilipo. Leo
hii mtu aliyegundua ndege haridhiki na ndege amabayo ameigundua bali anafikiria
kitu kingine ambacho atakiongeza katika ndege ili kuongeza ubora au anafikiria
kitu kingine zaidi ya ndege.
Kama ndivyo hivyo hata wewe katika jambo
lolote ambalo unalifanya lazima ufikirie hivyo. Usiridhike na ulichonacho bali fikiria ni nini
unakihitaji zaidi ili kuongeza thamani katika jambo ambalo unalifanya. Kuwa mtu
ambaye ni mbunifu ambaye utatofautiana na wengine. Endapo utayafanya hayo kwa njia tofauti na
zile ambazo umezizoea utakuwa tofauti sana na watu wengine na ndoto zako
zitazidi kung’ara mara dufu.
Daima tukumbuke ya kwamba wewe ndiye mmiliki
wa mafanikio yako, hivyo una uwezo mkubwa wa kuyafanya mafanikio hayo yakuwe au
yafe. Kitu cha msingi ili kukuza biashara
au jambo lolote ni kuamua tu na
kuvifanya mambo kwa njia na tofauti ulizozioa .
Makala
imeandikwa na; Benson chonya
Simu;
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.