Mar 7, 2016
Hiki Ndicho Chanzo Kikubwa Cha Kushindwa Kwako Katika Jambo Unalolifanya.
Siku
zote katika safari ya mafanikio, elewa ukweli huu kwamba hakuna tatizo lililo
kubwa ambalo linauwezo wa kukuzuia kufikia mafanikio yako unayoyataka. Hakuna rafiki atakayekuzuia
kwenye mafanikio. Hakuna uchumi mbovu utakaoweza kukuzuia kufanikiwa. Hakuna
hali mbaya yoyote kama kukosa wateja na hali nyinginezo eti ndiyo ikawa sababu
ya kukuzuia kufanikiwa.
Chochote
kile ambacho unaona ndiyo inaweza ikawa chanzo cha kushindwa kwako, tambua siyo
kweli. Mara nyingi huwa kipo kitu kimoja tu ambacho wengi hawakijui na ndicho kinapelekea
wewe ushindwe kwenye mambo yako mengi. Kitu hicho si kingine bali ni wewe
mwenyewe. Wewe ndiye chanzo kikubwa cha kushindwa kwako.
Unaweza
ukaona mambo mengine yaliyo nje yako ndiyo yanakuzui sana kufanikiwa lakini
kama nilivyoanza na kusema sio kweli. Wewe ndiye mtu pekee unajizuia kwa sehemu
kubwa kwenye mafanikio. Mambo mengine unayoyaona kama vile kuzuizi ni kweli
yapo lakini hayo yana mchango kwa asilimia ndogo sana za kukuzuia kufanikiwa.
Najua
unajiuliza maswali mengi sana kivipi? Sikiliza. Unajizuia kufikia kwenye
mafanikio yako kwenye mambo mengi unayoyafanya wewe. Kwa mfano unajizuia
kufikia mafanikio yako hasa pale
unapokata tamaa. Unajizuia kufikia kwenye mafanikio yako pia pale unaposhindwa
kuamini kwamba utafanikiwa. Wakati mwingine unajizuia kwenye mafanikio yako kwa
kushindwa kwako kuchukua maamuzi ya kukufanikisha.
WEWE NDIYE CHANZO CHA KILA KITU. |
Ukiangalia
kwa kina utagungua chanzo kikubwa cha kushindwa kwako kinaanza na wewe. Kumbuka
hauwezi kushindwa katika jambo lolote katika maisha yako mpaka wewe mwenyewe
uruhusu hali hiyo ya kushindwa itokee ndani yako. Jaribu kufikiria katika
maisha yako, jambo lolote lile ulilolishindwa , hukushindwa hivi hivi tu kwanza
ulianza kukubali kutoka ndani yako kwamba sasa hapa siwezi tena kufanikiwa
katika hili. Na kweli ilikuwa hivyo.
Kama
hujaelewa vizuri ninachokwambia hapa nitakupa mfano. Naamini umewahi kupita
shule na kuna wakati ulisoma somo la hesabu. Kama ulikuwa ukifanya vizuri,
hongera. Lakini kama ulikuwa ukishindwa kila mara somo hili unajua ni kitu gani
kilichokuwa kikitokea? Ni kwa sababu ulikuwa umeruhusu hali hiyo ya kushindwa hesabu
iwe kwako. Na uliruhusu hivi kwa sababu ya zile sifa ambazo kila mtu anasema
kwamba hesabu ni ngumu, basi na wewe ukajikuta unakubaliana na hali hiyo na
kusema hesabu ngumu ukakubali kwamba utashindwa na ukashindwa kweli.
Kwa
mantiki hiyo unaona kabisa hata katika mambo mengine ya kimaisha wengi wetu
wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya wao wenyewe na si vinginevyo. Unaweza ukasingizia sana hali yoyote kama
wazazi wangu hawakunisomesha au mimi
sina mtaji na pia nimezaliwa familia maskini, yote sawa. Lakini kikubwa kumbuka
wewe una mchango mkubwa wa kubadili maisha yako kwa zaidi asilimia themanini.
Unalo
jukumu la kujikumbusha kila siku kwamba wewe ndiye unayewajibika kwenye maisha
yako kwa kila kitu. Hivyo hutakiwi kukata tamaa, hutakiwi kujirudisha nyuma kwa
mitazamo yako. Pia hutakiwi kujirudisha nyuma kwa kuwanyooshea wengine vidole
kwamba ndiyo wamekufikisha hapo. Hiyo haitakusaidia sana zaidi ya kuchukua
hatua ya kubadilika na kuendelea mbele.
Ansante
kwa kusoma makala haya. Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia
DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Pia endelea kuwashirikisha wengine waweze
kujifunza kutokana na makala tunazotoa hapa.
Ni
wako rafiki katika kusaka mafanikio ya kweli,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.