Mar 15, 2016
Yasiyowezekena Ndio Mlango Wa Mafanikio Yako.
Uhali gani mpenzi msomaji wa safu hii ya DIRA
YA MAFANIKIO? Ni matumani yangu makubwa unazidi kuelimika kwa kujifunza mambo
mbalimbali kupitia mtandao huu, pia
nakusihi kila utakochojifunza kupitia
mtandao huu ni vyema ukawashirikisha na watu wengine ili na wao waelimike
zaidi. Kama ilivyo ada yangu kuweza kukumbusha baadhi ya mambo ambayo
yatukufanya uzidi kusonga mbele kimafanikio kwa kila jambo unalolifanya ili
kuweza kutimiza ndoto zako.
Katika makala ya leo tutakwenda kujikita zaidi
kwa kutazama yale mambo ambayo tunayaangalia kwa jicho la kawaida na kuyaona
mambo hayo kwamba hayawezekani. Lakini katika makala ya leo nakusihi ya kwamba
kwa kila jambo ambalo unaona haliwekani jaribu kulitazama jambo kwa jicho la
tofauti, endapo utayatazama mambo ya kimafanikio kwa jicho la tofauti hakuna
jambo ambalo halitawezekana.
Kimsingi tulio wengi hatuamini katika kushinda
ila tunaamini katika kushindwa, kuna usemi mmoja huwa unatumika katika michezo
mbalimbali unasema ya kwamba ‘’asiyekubali
kushindwa siyo mshindani’’ vilevile hata katika safari ya mafanikio usemi huu
unahusika sana kwa sababu kuna baadhi ya watu hawapo katika upande wa kuamini
ya kwamba siku moja watakuwa zaidi ya Dongote au matajiri wengineo, swali la
kujiuliza ni kwamba hao matajiri wa leo,
kama na wao wasingekuwa fikra
chanya za kuwa matajiri zaidi ya matajiri walikuwepo kwa kipindi hicho
unafikiri leo hii wangekuwa hapo walipo leo hii?
Soma; Usipojiandaa Kwa Mabadiliko Haya, Hakuna Wa Kukusaidia Katika Maisha Yako.
Soma; Usipojiandaa Kwa Mabadiliko Haya, Hakuna Wa Kukusaidia Katika Maisha Yako.
Jambo jingine la msingi ni kwamba kama wewe ni
mwanafunzi mara nyingi umekuwa unafeli hasa
katika masomo yako hasa somo la hesabu , unafikiri kufaulu somo hilo
inawezekani au haiwezekani? Mwalimu wangu mmoja wa saikolojia aliwahi kutufundisha kuhusu mafanikio
alituambia ya kwamba katika safari yeyote ya mafanikio kila kitu kinawezekana, baada ya kusema hivyo nilibaki nimeduwaa huku
nikijiuliza anamanisha nini? Huku nikiendelea
kujiuliza, akasema ‘’ vitu
ambavyo haviwezekani ni kumuomba dereva wa bodaboda akupe tiketi au kumeza plasta huku ukitarajia
ikutibu kitonda kilichopo nje ya mwili’’. Hivo amini ya kwamba wewe kufaulu kimasomo
inawezekana endapo utaweka nia za kweli.
KILA KITU KINAWEZEKANA KWAKO |
Baada ya kipindi nilirudi nyumbani na
kuwaza ni kweli katika mafanikio kila
kitu kinawezekana? Nikaona jibu ni ndio
kila kitu kinawezekana. Nikajaribu
kumuangalia mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne ambaye amefeli masomo yake.
Wapo wengi hukata tamaa na kuamini maisha yao yameisha pale huku wakiwa
wanaamini ya kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha. Swali dogo la kujiuliza ni
kwamba hawa waliofeli ina maana ya kwamba elimu imeishindwa kufungua maisha
yao? Jibu ni kwamba sio kweli, ila
kufeli darasani sio kufeli maisha, jaribu kuangalia ni sehemu gani
unaweza ukafanya vizuri na ukawa mshindi pia.
Soma; Umuhimu Wa Mahusiano Bora Katika Mafanikio.
Soma; Umuhimu Wa Mahusiano Bora Katika Mafanikio.
Wapo baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo akili
zao zote wanazielekeza katika msingi ya kuajiliwa peke yake. Wanafunzi hao
hawaamini katika misingi ya kujiajiri wenyewe
pia na wao kuwajiri wengine. Katika hili nimebaini ya kwamba wanafunzi
wengi ni wavivu wa kufikiri wao wanaamini ya kwamba kama mtu amesomea ualimu
basi atakuwa mwalimu mpaka azeeke,
endapo utakuwa na dhana hii
mafanikio kwa upande wako yatakuwa magumu sana. Pia naomba nieleweka vizuri sio
kuajiriwa ni kubaya la hasha bali jaribu kuwa na vyanzo vingi vya mapato licha
ya kutegemea kuajiliwa peke yake .
Vilevile kuna baadhi za jamii ambazo ni za
wakulima na wafugaji wao wanaishi katika misingi ya imani potofu katika
shughuli zao, hivyo kuwapelekea hata kushidwa kuzalisha bidhaa kwa wingi huku
kufanya hivo wanaamini ya kuwa watalogwa. Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye
imani kama hizi jaribu kuachana na imani hizo mara moja na ufanya kazi kwa
bidii kwa malengo ili kutimiza ndoto zako. Wewe ni
miongoni mwa watu ambao wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya maisha yako na
ya watu wengine kwa sabaubu unaziona
fursa nyingi za kufanikiwa hivyo usiwe kama samaki
mwenye kiu ndani ya maji.
Mwandishi; Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.