Mar 9, 2016
Hizi Ndizo Siri Za Mafanikio Zilizojificha.
Asante
sana kwa kuendelea kufuatilia makala mbalimbali za mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Ni matumaini yangu unazidi kuelimika kwa namna
moja ama nyingine. Katika makala yetu ya leo nitakwenda kueleza kuhusu siri za
mafanikio zilizojificha ambazo wengi wetu huenda tukawa tunazijua au tukawa
hautuzifahamu pia.
Kimisingi
siri hizi ndizo zitakazokufanya wewe uweze kutoka hapo ulipo na kuzidi kusonga mbele kwa maana ya
kuwa na mafanikio zaidi. Mafanikio ninayaongelea hapa ni yale ya kila sekta
aifanyayo mwanadamu. Mafanikio ndio msingi mkubwa kwa kila mwanadamu. Watu wengi huwa tunapata nafasi mbalimbali za
kufanya kazi lakini wengi wetu tunashindwa kuzitumia nafasi hizo. Mfano leo hii umepata ajira mahali fulani
wengi wetu hufanya kazi ilimradi tu badala ya kuonyesha uzoefu na ubunifu zaidi ulionao.
Ngoja
nikusimulie kisa kimoja ili utambue siri hizo zilizojificha za
kimafanikio; Kuna mwindaji mmoja katika
kijiji fulani alikwenda kuwinda wanyama katika msitu ambao upo mbali na makazi
yake. Baada ya kuwinda kwa muda mrefu alizunguka sana huku na huko lakini hakupa
kitoweo kwa siku ile. Siku iliyofuata hakukataa tamaaa alikwenda tena msituni
kwa ajili ya zoezi la uwindaji. Alizunguka sana siku hiyo lakini hakupata
chochote, ilipofika majira ya saa nane mchana mwindaji yule kwa kuwa alikuwa
amechoka sana alimpasa apumzike katika msitu uleule ili akusanye nguvu za
kuendelea kuwinda.
Baada
ya muda mchache aliendelea tena na zoezi
kuwinda bila kukata tamaa lakini hukupata chochote. Aliendelea tu kuwinda na
kujisemea ndani ya moyo wake kwamba ‘naendelea kuwinda sikati tamaa kama
ilivyotekea jana. Ghafla wakati
akiendelea kuwaza hayo katika akila yake
alitazama chini na kuona mayai mawili ya
ndege aina kanga. Mwindaji yule alifurahi
sana kwa kuwa alikuwa amezunguka sana ,
aliamua kuchukua mayai yale mawili. Yai
moja akalishika upande wa mkono kulia na yai jingine akalishika upande wa mkono
kushoto.
IJUE SIRI YA MAFANIKIO YAKO. |
Badaa ya muda mfupi alianza kupanga mipango
juu ya mayai yale. Alianza kwa kusema
maneno haya mayai haya nitakwenda kuchanganya na mayai kuku wangu, mwisho wa
siku watazaliwa kanga wawili, kanga hao nao watazalina watakuwa wengi zaidi,
kwa baada ya miaka kama 20 nitakuwa mzalishaji mkubwa wa kanga katika kijiji
hichi na mkoa kwa ujumla, hivyo nitakuwa na wateja wengi sana, nitapata hela
nyingi sana, niatajenga nyumba nzuri na yenye kila kitu cha kisasa, nitanua
magari mengi kwa ajili kutembelea , nitanunua mifugo mingi kwa ajili ya kufuga
na kupanga mambo mengine mengi.
Kumbuka
ya kuwa wakati anapanga hayo mayai yalikuwa bado mikononi mwake. Baada ya muda
mchache baada ya kupanga mipango yake juu mayai, alijiona jinsi atakavyokuwa tajiri na
atakavyokuwa tofauti na wanakijiji wengine, furaha ilimzidi na kusahau kuwa
ameshika mayai mikononi mwake alipiga makofi na kusema Mwenyezi mungu nisaidie
baada ya kupiga makofi mayai yale mawili yalivunjiaka na ndoto zake zote zikawa
zimeishia pale. Furaha yake juu ya mipango
ya maisha ikamfanya ndoto zake ziishie pale.
Kisa hiki kinatufundisha baadhi ya
mambo yafutayo;
1.
Kuna uwezekano mkubwa sana furaha ikizidi sana inakufanya ushindwe kutimiza
malengo na ndoto ulizokuwanazo. Unaweza ukasema afisa muongo ila huo ndio
ukweli. Ni watu wangapi leo hii walikuwa na furaha sana siku ya sherehe
mbalimbali na leo hii ni vilema? Ukifuatilia
juu ya hilo utakuta ni wengi mno na wengi ndoto zao zimeishia hapo. Mtu anakuwa
na furaha iliyozidi mwisho wa siku anajipongeza kwa kunywa pombe matokeo yake
furaha inageuka na kuwa majuto. Ukiona
ya kuwa una furaha fanya kitu cha maendeleo kuliko kufanya mambo ambayo
yatakughalimu maisha yako yote.
2.
Kisa hiki pia kinafundisha kutokukata tamaa kwenye mambo mbalimbali. Siku sote zipo changamoto ambazo huwa
zinaingilia mambo yetu ya kimafaniko. Kama tulivyoona katika kisa hicho naamini
ya kuwa mwindaji ana nafasi nyingine ya kutazama ni vipi malengo yake yanaweza
kutimia kwa kuangalia fursa zingine zilizopo?
Daima
tukumbuke ya kuwa kwa kawaida binadamu wote tuna malengo na ndoto kubwa za kimafanikio ila tatizo ndoto hizo
huja kwa kuharibiwa na kitu kimoja tu. Hivyo ni vyema kuepuka na kitu hicho
ambacho kitakufanya usiweze kutimiza malengo yako. Kila siku tukumbuke ya kuwa
sio kila furaha ikizidi sana itakufanya ushindwe kusonga mbele.
Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.