Mar 1, 2016
Ukiyafanya Haya, Mafanikio Makubwa Yapo Upande Wako.
Kwa
muda mrefu umekuwa ukijiuliza ni vipi utapata mafanikio unayoyahitaji? Lakini jibu ni kwamba mafanikio unayo wewe
mwenyewe ila tatizo ni kwamba unakuwa ni mtu wa kusuasua kuanza mambo hayo ya
kusaka mafanikio.
Ngoja
nikukumbushe ya kwamba hakuna muda maalumu wa kuyasaka mafanikio. Utawasikia
watu wengine wanasema eti nikiwa au ukifika miaka 35 au 40 eti ndo utaanza
kuyasaka mafanikio kwa kuwa na nyumba, magari na mengineyo.
Hii
sio kweli kumbuka ya kwamba muda wa
mafanikio ni sasa na wewe ndio mwamuzi wa kuamua kuanza kuchangamkia fursa zilizopo ili uweze
kuwa miongoni mwa matajiri ambao utakuwa
unatajwa midomoni mwa watu, naamini
ya kuwa unaweza.
Wapo
baadhi ya matajiri wakubwa tunaowajua. Leo ukijaribu kusoma historia zao wengi
wameanza kuwa na mitaji midogo kabisa lakini leo hii ndio ambao wapo midomoni mwetu
na pengine tumekuwa tukishangaa sana mafanikio yao.
Kwa
sisi ambao bado hatujapata mafanikio, kwa muda mwingi tunakaa vijiweni tunawajadili
, kuwasifia na kuwapa sifa nyingi nzuri bila wao kutusikia hata kutujua majina
yetu, huku wao wakiingiza fedha na kuzidi kutajirika zaidi.
Kiuhalisia,
yapo baadhi ya mambo ambayo leo hii tukiyafanya , sisi wengine ambao hatuna siri hii ya utajiri, tukiijua vizuri tutakuwa kama wao. Sasa
twende pamoja kujifunza baadhi ya mambo ambayo leo hii ukiyafanya mafanikio
makubwa yatakuwa upande upande wako.
Jambo la kwanza; Tenga muda wa
kufikiri mambo yako.
Muda
ni jambo la msingi sana katika safari ya mafanikio. Kisaikolojia binadamu wote
ni sawa ila tunatofautina sana katika
matumizi ya muda. Ngoja nikupe mfano huu ili uweze kunielewa zaidi. Kwa siku kuna masaa 24. Masaa haya jinsi
anavyotumia masikini na tajiri ni tofauti kabisa. Tajiri masaa haya huyaona
hayotoshi kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya. Ndio maana hata baadhi ya
matajiri ukiwa hufanyi vizuri katika kazi zao utawasikia wanasema usinipotezee
muda maana kwao muda ni mali.
Lakini
masaa hayohayo kwa maskini huwa ni masaa mengi sana kwa sababu hana mambo mengi
ya kufanya hata kufikiria pia. Maskini huyohuyo akitaka kuamka asubuhi
utamsikia anauliza hivi jua limechomoza. Kwa maana ya kwamba yeye huongozwa kwa
kulitazama jua. Halikadhalika akiamka asubuhi utamsikia usiku wa leo ulikuwa
mrefu sana. Ewe msomaji wa makala haya
ukifanya hivyo mafanikio utayasikia kwa akina Bill Gate tu.
BADILI RATIBA YA KUFANYA MAMBO YAKO. |
Pia
kumbuka wazo zuri ambalo utalipata wakati umetenga muda wa kufikiria mambo
yako, lifikirie mwanzo hadi mwisho wa jambo hilo. Pia liwe ni jambo moja.
Liandike kwenye karatisi au mahali popote ambapo unahisi hatapasau kwa urahisi
yaani ikiwezekana iwe sehemu inayoonekana.
Andika
mikakati mizima ya utekelezaji wa jambo hilo. Kwa kuangalia zana ambazo
zitatumika kuangalia jambo hilo, pia jaribu kutazama changamoto ambazo unahisi
zitajitokeza juu ya jambo hilo pamoja na jinsi ya kukabiliana changamoto hizo
na jaribu kuona matokeo ya jambo hilo. Kwa ufupi lazima uone maono (Vision) ya
wazo lako.
Jambo la pili; badili ratiba ya kufanya
mambo yako.
Kuna
baadhi ya watu tunafanya vitu kimazoa sana hii inapelekea siku zote tunabaki vilevile huku tukilalamika ya kuwa maisha ni
magumu. Tukumbuke ya kwamba Kufanya vitu kimazoea kunamfanya mtu asiweze
kusongo mbele.
Watu
wengi ambao wanalamika juu ya maisha asilimia kubwa utagundua ya kwamba
wanafanya vitu kimazoea. Kama kweli
unapenda jambo fulani la kimafanikio, basi usilifanye kwa mazoea.
Fanya vitu tofauti na ulivyozoea utaona matokeo makubwa ya kimafanikio
yapo upande wako.
Kama
umezoea kuamuka saa mbili kamili asubuhi basi amka saa kumi na mbili asubuhi
ili uone mpaka saa mbili utakuwa umefanya nini, kama umezoea kufunga biashara
yako saa tatu usiku basi ongeza muda wa kufunga biashara yako hadi saa tano ili
uwone kama kuna mabadiliko. Kama wewe ni mvivu basi anza kuwa miongoni mwa watu
wanaofanya kazi kwa bidii.
Endapo
utafanya hayo yote kwa kuzingatia wewe ni msaka tonge mafanikio makubwa yapo
upande wako. Usikate tamaa katika kila jambo unalolifanya. Kuwa shupavu kama simba, maana simba akikosa nyama hawezi kula nyasi
atapambana huku na huko ili apate nyama.
Kama
una maswali , ushauri au mapendekezo usisite kuwasiliana na afisa maendeleo na
mipango, mwandishi wa makala haya Benson
Chonya. Usisite pia kumshirikisha
mwenzako ili aweze kujifunza pia.
Simu;
+255 (0) 652 015 024
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.