Mar 8, 2016
Hizi Ndizo Sauti (3) Zinazochangia Kuleta Mafanikio Yako.
Mafanikio
unayoyahitaji kesho msingi wake mkubwa huanzia leo. Ukitaka kufanikiwa inawezekana
kabisa tena mara moja ndani ya sekunde kadhaa tu. Tupo baadhi yetu huwa
tunajikatisha sana tamaa wenyewe kwa kujisemea baadhi ya maneno kama vile hivi
nitaweza kweli? Maneno kama hayo yanakufanya uzidi kujiona wewe mnyonge na
huwezi kusonga mbele siku zote. Kuna mwalimu wangu mmoja wa dini aliwahi
kuniambia mdomo huumba kwa kile unachokisema ndicho kitakachokutokea, acha
kujisemea maneno yenye kukutasha tamaa bali jinenee maneno ya ushindi siku
zote.
Mara
nyingi umekuwa ukisikika zaidi kuliko kusikiliza. Tofauti kubwa iliyopo kati ya
kusikia na kusikiliza ni kama ifuatavyo, Kusikia ni kusikiliza kitu kwa juu juu
tu bila kutilia umakini kwa kile unachokisikiliza mfano unasikia gari inatoa mngurumo,
mtu atasikia sauti hii ile lakini hata
sikiliza. Ila kusikiliza ni kuwa makini kwa kile ambacho unasikiliza na
kukielewa mfano mtu akiamua kweli
kusikiliza taarifa ya habari atakuwa makini na kuilewa na kinyume chake
inawezekana pia.
Zifutazo ndizo sauti tatu
zinazochangia mtu aweze kufanikiwa;
1. Sauti za watu tofauti tofauti.
Hizi
ni zile aina na sauti ambazo umekuwa ukisikiliza kutoka kwa watu mbalimbali
ambao wanakuzunguaka. Hizi ni sauti za watu zenye kukutia moyo ili uweze
kuongeza juhudi kwa jambo unalolitaka ili uweze kufanikiwa. Wapo baadhi ya watu
utawasikia wanasema ukijitahidi kufanya vitu fulani mfano katika masomo,
biashara, kilimo na vitu vingine vingi utaweza kufanikiwa . Sauti hizi mtu
huambiwa ili kumuongezea hamasa kwa kila jambo analofanya ili aweze kutimiza
ndoto zako. Sauti hizi unaweza kusikia kutoka kwa watu waliofanikiwa hata
wasiofanikiwa pia. Sauti hizi unaweza ukasikia katika semina na sehemu
zinginezo. Swali la kujiuliza ni kwamba mafanikio yako yameletwa kwa njia
hii au yataletwa kwa njia hii ya kuwasikiliza watu?
KUWA MAKINI NA KUSIKILIZA SAUTI ZINAZOKUZUNGUKA. |
2. Sauti za historia mabalimbali.
Ni
aina nyingine za sauti ambayo inachangia kwa kiwango fulani mtu aweze kufanikiwa.
Sauti hizi za historia ni zile sauti ambazo tunasikia kutoka kwa watu
mbalimbali ambao bado wanaishi au hatupo nao tena kwa kusikia historia kwa baadhi ya mambo ambayo
waliyafanya na bado wanayafanya ili
waweze kufanikiwa zaidi. Sauti hizi za historia tunazisikia kutoka kwa matajiri
wakubwa kama vile wakina Bill Gate na wengineo wengi. Sauti na historia zao
zinatufanya tuone ni jinsi gani walianza na leo hii wameweza kufanikiwa na kuwa
matajiri wakubwa. Historia zao zinatufanya tujione na sisi tunaweza na siku
moja tutakuwa au tutakuwa zaidi ya wao.
3. Isikilize sauti yako.
Hii
ndiyo sauti kubwa kuliko sauti zote.
Sauti hii ni nyembamba sana ambayo ipo ndani ya moyo wa mtu . Watu
wachache ambao wanaitambua sauti hii, Sauti hii humfanya mtu yeyote aweze
kufanikiwa mara moja endapo utaamua kusikiza sauti yake. Endapo utaamua kujitambua na kusikiza sauti
hii ndio siku ambayo umaskini utakuwa umeupiga teke. Ngoja niendelee kukupa
madini juu ya sauti hii, Kila mtu amekuwa na sauti hii nyembamba lakini
anashindwa kuitumia hii ni kutoka na mfumo wa maisha ya kwamba huwezi kufanya
kitu chochote mpaka mtu fulani aamue juu
ya maisha yako.
Ni
watu wangapi leo wanafanya kazi kutokana na kusikiliza sauti za watu wengine
kuliko kuzisikiliza sauti zao? Usinipe jibu. Ni watu wangapi leo hii
wanajilaumu kwa kufanya kazi kwa ambazo hawazipendi hii ni kutokana walisikiza
sauti za watu wengine? Ukichunguza kwa makini utagundua ni wachache mno
wanaofanya kazi kwa upendo. Lakini ndugu msomaji wa makala haya kiukweli sijui nikueleza vipi ili ujue sauti yako ndio
ushindi wako ? Lakini tambua ya kuwa siku
ambayo utaamua kuisikilza sauti nyembamba ambavyo inatoka moyoni mwako ndio siku ambayo
utafanikiwa. Tukumbuke bahati huja kwa waliojitayarisha.
Asante
kwa kuendelea kufuatilia makala haya ya dira ya mafanikio
Makala
hii imeandikwa na afisa mipango na maendeleo; Benson Chonya
Simu;
0757-909942
E-mail.
Bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.