Mar 17, 2016
Jinsi Ya Kuweka Vipaumbele Hadi Kufikia Malengo Yako.
Watu wengi sana duniani hawajui
umuhimu na thamani ya kitu kuweka vipaumbele katika maisha yao. Mwanasaikolojia
mmoja aliwahi kusema mtu yeyote anayeishi duniani akikosa Kipaumbele katika
maisha yake hawezi kuishi atakavyo yeye bali ataishi watakavyo watu wengine. Nami
nasema kama ukikosa kipaumbele katika maisha yako usubiri kuwa mtumwa katika
maisha yako yote.
Tunapozungumzia vipaumbele ni dira au
mwongozo unaomwongoza mtu katika kutekeleza malengo aliyojiwekea. Kama
tujuavyo kila binadamu ana malengo yake katika maisha. Haijalishi ni
madogo au makubwa ya muda mrefu au mfupi,mazuri au mabaya yote ni malengo.
Watu wengi tunashindwa kutimiza
malengo yetu si kwa sababu hatuna elimu, si kana kwamba hatufanyi juhudi na
hatuna moyo wa kufanya vitu vya maendeleo. Tumekosa kitu kimoja kidogo sana
ambacho ni KIPAUMBELE. Kwa nini nasema tumekosa kipaumbele? Ngoja nikupe mfano.
Mwaka juzi nilikuwa natoa semina chuo
kikuu cha Dar es salaam kuhusu Saikolojia ya namna ya kujitambua. Wakati naendelea na
mada nilijaribu kuwauliza wanafunzi wa chuo mwaka wa pili je ukimaliza chuo
utataka kufanya kazi gani itakayokulipa? au utataka kuwa nani ukimaliza chuo?
Majibu yaliyotoka utakubaliana na mimi
kuwa watu hawana vipaumbele katika maisha yao. Moja ya wanafunzi anayesomea
sheria alinijibu nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Bakheresa. Mwingine
anayesomea shahada ya udaktari alijibu mimi nataka nikimaliza chuo nataka
niwe Pilot au rubani wa ndege kwa kuwa urubani unalipa sana mwaka moja tu
nitakuwa tajiri. Mwingine akajibu mimi nikimaliza chuo nitafanya kazi yeyote
ntakayoona inalipa na inaweza kunitoa kimaisha fasta.
JIWEKEE VIPAUMBELE VYA KUWA MSHINDI. |
Hao ndio wasomi wetu.Swali ni je hapa
kuna mtu mwenye kipaumbele kitakacho mfikisha anapotaka? Jibu ni rahisi tu
Wanachuo hawa wamekosa kipaumbele katika kutimiza ndoto zao. Wanajaribu kugusa
kile kinachoweza kuwaletea mafanikio bila kujali ni kwa namna gani na kitaweza
kumugharimu kiasi gani. Kumbuka siku zote kutambua
na kuona ni vitu viwili tofauti.
Vipaumbele ni mwongozo ni hamasa
zitakazo kufanya ujihimu na ujibidishe katika kuhakikisha unatimiza malengo ya
ndoto zako. Vipaumbele vitakufanya usichoke kufanya kile unafanya kwa lengo la
kuitimiza ndoto zako. Ukiwa na vipaumbele ni ngumu sana kukata tamaa na ni
nguvu sana kufanya maamuzi tofauti na uliyokusudia. Ukiwa na vipaumbele
hutapoteza muda wako bure kwa vitu ambavyo kamwe havita kusaidia ktk kutimiza
ndoto zako. Alaaa kumbe! Kipaumbele ni kizuri sana mtu ukiwa nacho katika
maisha eti eee!! Ansante sana mzee wa nyundo kwa kunihabarisha hili.
Je nawezaje sasa kupanga vipaumbele
vyangu katika maisha yangu ili nitimize malengo na ndoto zangu katika maisha? Twende
pamoja mbona rahisi sana!
1. Kuwa na malengo katika maisha yako
unataka kuwa nani katika uhai wako au siku za usoni kwa mbeleni. Unataka uwe
mhandisi,injinia,daktari,mkulima au mfanyabiashara?
2.Unataka ufikie wapi kielimu chuo, kidato
cha sita au unataka upate mwanga tu kisha usomee ujasiriamali?
3.Kiafya unataka uwe na unene
kiasi gani au mwembana kiasi au mnene sana?
4.Kimaendeleo unataka umiliki vitu
gani vya kifahari Nyumba, magari au nini unataka kumiliki?
5.Kiimani unataka familia
yako,ndugu zako na jamii kwa ujumla ukitazamaje kuhusu Imani yako mtu
wa Mungu,mnyenyekevu au katili na jeuri asie na upendo na watu?
6. Kipesa unataka umiliki kiasi gani
cha pesa ili kufikia malengo na furaha ya maisha yako. Hizi ni baadhi tu ya
vipaumbele ambavyo unaeeza kujiwekea ktk maisha yako na vikakupa hamasa katika
kutekeleza majukumu yako na kutimiza malengo yako uliyojiwekea katika maisha
yako. Naomba kuishia hapa kwa leo nikutakie uwekaji mwema wa vipaumbele
vitakavyo kuongoza kutimiza malengo yako.
Nikutakie siku njema na endelea
kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki katika kusaka
mafanikio ya kweli,
Shariff H. Kisuda alimaarufu mzee wa nyundo kali,
Simu; 0715 079993,
Email; kisudasharrif@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.