Mar 3, 2016
Faida Za Kujua Kile Unachokitaka Katika Maisha Yako.
Kimsingi
kila mwanadamu anapenda kuwa na maisha
mazuri siku zote, hakuna hata mmoja
ambaye anapenda kuishi katika maisha ambayo sio mazuri hata siku moja. Baadhi wa watu hawa
hasa ya wale ambao hawajafanikiwa
ukiwauliza kile ambacho wanakihitaji, wengi wao hutoa majibu ya ujumla
kwamba nataka kuwa mfanyabiashara, nataka kusoma , nataka kujenga nyumba na
vitu vingine vingi ambavyo mwanadamu huyu anataka kuwa au kuvifanya kwa hapo baadae.
Lakini
ukweli ni kwamba kusema hayo huwa tunakosea kwa sababu huwa tunayoongelea kwa
mapana sana, hapa namaanisha ya kwamba lengo lako la kesho lazima liwe
maalaumu. Kwa mfano usiseme unataka kuwa mbanyabishara na kuishia hapo tu, bali
ni lazima uainishe ni aina gani ya biahara unayotaka kuja kuifanya na utie nia
ya kweli juu ya biashara hiyo.
Kwa mfano unaweza kupanga malengo yako ya hapo
baadae unataka kuwa mfanyabiashara wa viatu, nguo za kiume, kike au viatu. Hata
kama unataka kujenga nyumba katika maono yako lazima ufikirie unataka nyumba ya aina gani? Iwe na vyumba
vingapi, aina gani ya madirisha unatamani yawe kwenye nyumba yako na vitu
vingine vingi.
Hizi
ndizo faida ya kujua kile unachokihitaji kwenye maisha yako.
1. Huongeza kujiamini.
Baada
ya kujua ni nini ambacho unachohitaji katika maisha yako. Itakusaidia sana
kuweza kujiamini kwa kuweka jitihada za dhati za kufikiri na za kiutendaji
katika jambo hilo. Mfano wewe ni mwanafunzi umejua ni
nini ambacho unakihitaji katika masomo yako. Ni matumaini yangu makubwa
utajenga uwezo mkubwa wa kujiamini na kufanya vizuri katika masomo yako ili aweze
kutimiza ndoto zako halikadhalika wafanyabiashara na watu wengineo. Kujiamini
ni siri kubwa kwa mtu yeyote msaka maendeleo. Baada kujua ni nini ambacho unakitaka kutakusaidia
sana kuweka mikakati na mipango ili kutimiza lengo.
UKIJUA UNACHOTAKA, UTAHAMASIKA KUTENDA. |
2. Kutokupoteza muda kwa mambo ambayo
hayana msaada.
Mtu
akijua anachokitaka mara nyingi huwa ni mtu ambaye anajali sana muda katika
kutekeleza mambo yake. Vitu ambavyo
kwake havina faida kwake huachana navyo.
Kama mpaka dakika hii unatumia nguvu nyingi kwa kitu ambacho hakina
manufaa kwako jaribu kukiacha kitu hicho na anza kufanya vitu ambavyo vitakuwa
na manufaa makubwa kwako. Kwenye vitu ambavyo ni kweli unavitaka jaribu kuwa
makini katika matumizi sahihi ya muda ili kuweza kupata matokeo mazuri juu ya jambo hilo.
Mara
kwa mara mtu ambaye anafanya vitu ambavyo anavipenda huangalia zaidi katika
masuala yatakayomletea faida tu. Ila mawazo na mitazamo ambayo haina faida
huachana nayo.
3. Huleta hamasa kubwa ya kiutendaji.
Ukifanya
kitu unachokipenda mara nyingi huleta matokeo makubwa sana. Mfano wanafunzi
wengi hawafanyi vizuri kimasomo kwa sababu wanasoma vitu ambavyo siyo chaguo lao.
Mtu anapenda kusoma masomo ya biashara lakini wanampangia akasome sayansi,
matokeo yake mtu huyu akifeli tunaanza kumlaumu kwamba hana akili kumbe tatizo ni kumchagulia vitu
asivyovitaka.
Halikadhalika
hata wafanyabiashara walio wengi,
biashara zao zinakufa hii ni kutokana wanafanya biashara ambazo sio
chaguo lao sahihi mwisho wa siku biashara hizo huzidumu. Moja ya kutaka kuona
mafanikio ya kibiashara, elimu na vitu vingine hakikisha ya kwamba unafanya
vile ambavyo kweli unavipenda kutoka moyoni mwako.
Kwa
kuwa mafanikio yapo mikononi mwako, fikiri kwa makini mambo ambayo unahisi ni
chaguo lako sahihi, na ukiyafanya kwa umakini wa hali ya juu utafanikiwa. Daima
kumbuka usemi huu wa ushindi siku zote ‘my
wish is my command.’
Asante
sana kwa kuendelea kufuatila makala kutoka katika mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, ombi langu kwako washirikishe wenzako kadri uwezavyo ili wajifunze
zaidi.
Makala hii imeandikwa na mtaalamu wa mipango na
maendeleo Benson chonya.
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.