Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, June 10, 2016

Utaacha Alama Gani Duniani Siku Ukifa?

No comments :
Lazima ujiulize ya kwamba ni alama gani utaicha chini ya jua kabla hajafa? Kimsingi tunaambiwa na vitabu vya dini ya  kwamba kila binadamu ni mavumbi na atarudi kuwa mavumbi, kauli hiyo inaashiria wazi hakuna atakayeishi milele katika ulimwengu wa mwili labda katika ulimwengu wa roho hii ina maana ya kwamba kila nafsi itaonja umaiti kwa wakati wake. Nisizungumze sana ila maana ibaki pale pale ya kwamba utaacha Alana gani siku ukifa?

Kama mara kadhaa nilivyowahi kuandika ya kwamba hakuna binadamu akiyeletwa duniani kuzurula hivyo ni wakati wako wa kujiuliza unataka ukubukwe kwa mambo yapi pindi ukifa. Je, unahisi jamii unayoishi nayo itazungumza nini juu yako. Chungunza kwa umakini harafu uone ni jinsi gani jamii yako itavyozungumza mstakabadhi wa maisha yako pale ambapo wewe utakuwa haupo.

Kila jambo ambalo unalifanya ni lazima liache alama ya milele, ambayo itafanya watu wakuzungumze wewe kwa mazuri iliyokuwa unayaishi. Hebu tamani leo kuwa , uwe ni mfano wa kuigwa kwa jamii nzima kwa mambo mazuri ambayo umeyafanya.

Tujififunze kitu kupitia hadithi hii;

Hapo za zamani za kale katika nchi ya mashariki ya mbali kulikuwako na mfalme aliyeitwa Muhigo. Mfalme Muhigo alikuwa ni mtu ambaye aliwahiza watu kufanya kazi kwa juhudi. Mara kadhaa mfalme Muhigo aliwasisitiza sana watu wake wazingatie sana muda kwani aliamini ya kwamba muda ni Mali.

Hata hivyo mfalme huyo kila alipokuwa akihitaji kuzungumza na watu wake alihakikisha kila mtu atakayehudhuria katika mkutano huo anaeleza ni mambo gani ambayo ameyatekeleza yeye binafsi ya kimaendeleo na jamii kwa ujumla.

Watu wengi walikuwa hawamuelewi hasa akifika katika kipengele hicho cha kuwauliza wameyafanya yapi ya kimaendeleo. Watu wengi walionekana kukerwa sana kwa kuwa mfalme alikuwa ni mfuatiliaji zaidi wa mambo ya kimaendeleo.

Licha ya mfalme Muhigo kuendelea kuwahamasisha watu wake, hata yeye alijihamasisha mwenyewe pamaja na kuwahamasisha wafanyakazi wake kufanya kazi kwa bidii sana. Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo utajiri wake unavyozidi kuongezeka. Na mara kadhaa watu walikuwa wakinong'ona na kusema ya kwamba mfalme ni mwizi anatumie pesa zao. Baadae kadri watu walivyozidi kuzungumza mfalme akaja kusikia habari zile, mfalme alisikitishwa sana kwa sababu habari zile hazikuwa na ukweli ndani yake.

Acha alama sahihi kwenye maisha yako, kabla hujafa.
Hivyo aliamua kuitisha mkutano tena na falme yake kisha kuwaambia ukweli kuhusu mali zake. Neno ambalo aliwaambia ni kwamba na fahamu ya kwamba hamjui kiundani mafanikio yangu yanatokana na juhudi zangu katika kilimo, hata hivyo nanyi mtawakuwa mashaidi ya kwamba kuwa mara kadhaa nimekuwa nikiwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kutumia muda vizuri, hivyo nataka kuwaambia tena ya kwamba KAMA MNATAKA MALI MTAZIPATA SHAMBANI.
Kabla ya kumaliza kuzungumza akaileza jamii ile jinsi ya kufanya kilimo bora. Tangu Siku hiyo kila mwanajamii ile alitekeza yale yaliyosemwa na kuamini Mali inapatikana shambani na matunda yake kila mmoja aliyaona. Hivyo maneno ya mfalme yakaigeuza jamii nzima hata wakawa wafanyabiashara wakubwa na Wakaweza kuzilisha falme mbalimbali kwa kile walichokizalisha.

Kadri siku zinavyozidi kwenda mfalme Muhigo umri wake ulikuwa unaelekea jioni (uzeeni) hivyo maradhi mbalimbali yalikuwa yanamsumbua. Siku moja jioni wakati hali yake ikiwa bado ni pangusa nikaye (mbaya) aliwaita ndugu, familia yake yote, baadhi ya wanajamii na kuwaambia.

"Katika Maisha yangu niliwahimiza mfanye kazi kwa bidii na kujali muda sana kwani niliamimini ya kwamba muda ni mali, kwa mara ya kwanza ilikuwa ni ngumu kukubaliana na mimi ila nawashukuruni sana kwa kuwa sasa mmenielewa na mnafanyia kazi maneno yangu na matunda ninayoona, kwani tumeweza kulisha falme nyingi kupitia kilimo ambacho tunakifanya.

Pili ndugu zangu kwa sasa hali yangu ni mbaya na sina uhakika wa kupona hivyo nimewaita ili kuwafahamisha ya kwamba naomba maneno yangu ya kwamba kama unataka mali utaipata shambani muendeleni kuyafanyia kazi.

Lakini la mwisho naombeni kama nikifariki nawaomba sana mkinizika mikono yangu itokeze juu ya kaburi langu, baada ya kusema hayo kila mmoja alishanga! mtu mmoja akauliza kwanini mfalme unasema hivyo?

Mfalme akamjibu akasema"Mali zote nilizokuwa pindi nikifa nitaziacha hapa duniani hata hivyo mkifanya hivyo nilivyowaelekeza dunia nzima itajua ya kwamba mali zote za dunia hii hazina thamani tena mbele ya Mungu cha msingi ni kumuomba yeye atasaidie tu kuishi na watu vizuri.

Baada ya kusema hayo akarudia tena kusema" kama unaitaka mali utaipata shambani" baada ya kusema hayo akakata roho. Watu walilia sana na mwisho wakamzika kama alivyoamulu enzi za uhai wake. Mfalme Muhigo  maneno yake kwa watu wake yanaishi mpaka leo ni falme hiyo watu wote wamefanikiwa kimaisha.

TAFSIRI YA HADITHI HII NI;
Ewe Msomaji wa makala hii kama nilivyosema hapo awali ni lazima uiache alama katika sayari hii. Kwani umuhimu wa kufanya matendo bora kwa sasa ungali bado unatumia hewa hii ya oksijeni kutafanya uishi maisha bora na yenye furaha siku zote.
Alama pekee ya kukumbukwa daima ni kufanya mambo mazuri. Tukiachana mfalme Muhigo tuje tuwaangalie wahasisi mbalimbali wa taifa hili, kwa mfano mwl J.k. Nyerere kutoka na mambo analiyafanya enzi za uhai wake leo katuachia alama nyingi hadi inafika mahali vitu mbalimbali vinapewa majina yake. Kwa mfano kuna barabara, uwanja wa ndege, ukumbi na ndio maana mpaka hilo daraja jipya nalo limepewa jina lake.

Kitu Cha msingi  cha kuzingatia ni kwamba ishi vizuri na watu kwa kufanya vitu vyenye tija vitakavyofanya ukumbukwe daima, vinginevyo utasifiwa kwa baadhi ya mazuri ambayo unaliyafanya siku ya msiba wako ila baada ya siku mbili kila kitu kitasahulika na kubaki jina.

Mwisho nimalizie kwa kusema ni lazima ujue umekuja dunia kwa kusudio maalamu litimize kusudi hilo ili ukumbukwe daima. Pia ukumbuke kila binadamu ni mchungaji hivyo jiulize unachunga nini? Hakikisha kwenye uhai wako unaacha alama ya maisha yako.
Mwandishi ni afisa mipango; Benson Chonya
Simu; 0757-909942
Facebook; Benson Chonya
Barua pepe; 
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment