google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 14, 2016

Fikra Chanya Ni Chachu Ya Mafanikio.

No comments :
Ikiwa hali yangu haipo vizuri ila hali hiyo hainizui kuleta kusudio langu kwa wabantu wenzangu. Nimejaribu kutafakari kwa kina hivi ni kwanini mpaka leo nchi na jamii yetu bado ni maskini? Nikawaza kwa kina ili kujua nini tatizo?

Endapo pia ningekuwa darasani mwalimu angeniuliza swali kama hilo, majibu ambayo ningempa ni kwamba, sababu ya yetu kuwa maskini ni "because of poor leadership" ikiwa inamanisha kwa sisi ni maskini kwa sababu ya uongozi mbaya uliopo. Hayo ni majibu ya wengi na yakufaulu mtihani tu. Ila kwa uhalisia ukweli haupo hivyo kwa asilimia mia moja.

Lakini akili yangu sikutaka kuiruhusu iwaze juu ya majibu ya wengi. Nikagundua ya kwamba matatizo ya umaskini  tuliyonayo yanasabishwa kwa asilimia kubwa ni uwezo mdogo tulionao wa KUFIKIRI. Uwezo mdogo wa kufikiri ndio unaotufanya tuwe maskini mpaka leo hii na kutufanya pia kuwa ni miongoni mwa nchi ambayo inashika nafasi kumi mbovu kutoka mwisho ambayo watu wake hawana furaha kabisa.

Tunasema Tanzania ni nchi ya Amani huo ni kweli ukilinganisha na nchi ambazo hazina amani, ila cha ajabu licha ya kuwa na Amani ni nchi inayoshika nafasi ya 149 kati ya nchi 157 ambayo watu wake hawana furaha kwa bara la afrika.

Chachu ya mafanikio, inaanza na fikra zako chanya.
Usishangae huo ndio ukweli, kama unataka kubisha hebu tujiulize kitu kidogo, hivi ni watanzania wangapi wanaishi kwa FURAHA juu ya maisha yao na jamii kwa ujumla? Usinipe jibu, je unafikiri watu wangapi wanafurahia maisha haya tunayoishi kwa asilimia 100? Ukichunguza kwa umakini jambo hili majibu yake bila shaka yanahuzunisha sana.

Hata hivyo kutokuziruhusu fikra zetu kiziruhusu kuwaza vitu vipya kunatufanya wengi wetu kuwaza katika misingi ya aina moja. Mfano mzuri hebu chunguza kwa umakini uandishi wa maelezo binafsi (c.v) kwa asilimia kubwa utakuta nyingi zinafanana. Angalia biashara nyingi ambazo zinaendeshwa hapa nchini utakuta nyingi zinafanana. Unajua ni kwanini ni kwasababu uwezo wa kufikiri vitu vipya haupo.

Tuachane na hayo ili nisije kupoteza kusudio langu kwa siku ya leo? Ni hivi hapa kwetu Tanzania pana kila sababu ya kuwa zaidi ya nchi jirani ya ‘South Afrika’ ila tatizo bado tumezifunga fikra zetu, tumekuwa tukiishi miaka nenda miaka rudi maisha ambayo yapo katika mfumo wa ‘copy na paste’ (c&p), mfumo wa kuiga vitu kutoka nchi zingine, jambo hili sio baya naomba nieleweka ila kufanya hivyo kunatufanya tushindwe kuwa wabunifu wa vitu vyetu vya ndani.

Hata huo ubunifu wa vitu vyetu uliopo hauungwi mkono kwa asilimia zote, sijajua kwanini jambo hili ila huenda tatizo tunavithamini zaidi vitu vya nje. Watu wengi wamezoea kufanya vitu kutokana na mazoea sana, wakati wakisahau kufanya hivyo ni kuyumbisha bongo katika kazi ya kufikiri mambo chanya.

Upo usemi katika harakati zangu za pekuapekua nilikutana nao na wenyewe unasema "KAZI NGUMU KULIKO ZOTE NI KAZI YA KUFIKIRIA". Tafadhari rudia kusoma maneno hayo maana hayo endapo utayaendekeza ndio yanatofanya tuzidi kuwa maskini miaka nenda miaka rudi.

Uwezo wa kufikiri unazidi kupungua kila kukicha kwa wabantu wengi huku tukiendelea kufarahia ubunifu wa mataifa mengine kama China, Japan, marekani na mataifa mengine ambayo ubunifu wa vitu vyao unatokana na kazi ya kufikiri mawazo chanya kila siku.


Hivyo naamini ya kwamba kama kweli tunataka kusonga mbele kimafanikio ni wakati muafaka wa kuziruhusu akili zetu kuweza kutafakari mawazo chanya ambayo yatakwenda kubadili maisha yetu na wengine kwa ujumla. Ifike mahali tuwe wazalishaji sana kuliko kuwa watumiaji wa huduma au bidhaa kutoka nje ya nchi.

Ni matumaini yangu makubwa ya kwamba hii inawezakana endapo tutaweka vipaumbele vya mambo ambayo tunataka tanzania iweze kutambulika tukiachilia mbali uwepo wa vivutio tu. Nimesema hivyo huku nikiamini tunaweza.

Tujiulize yule ambaye aligundua Umeme wa maji, gesi na sola yeye alitafakari na nani? Bila shaka majibu unakuwa nayo, bila shaka kama nilivyowahi kuandika mara kadhaa dunia inahitaji majibu ya changamoto tulizonazo ambazo zinatuongezea uwezo wa kufikiri.

Nimalizie kwa kukuachia maswali ambayo unatakiwa kujiuliza siku ya leo;

1. Fikiri juu ya muda ulionao, je ni masaa mangapi yana faida kwako na ni masaa managapi hayana faida kwako?

2. Fikiri kuhusu mazingira uliyopo. Je kuna fursa ngapi zinapatikana hapo na unachukua hatua gani?

3. Fikiri kwa umakini kuhusu wewe. Je unataka kuwa nani kwa hapo baadae na sehemu gani?

4. Fikiri juu ya matatizo. Je ni unahisi una majibu ya changomoto zinazokuzunguka au wewe ni chanzo cha matatizo hayo?

5. Fikiri juu ya mawazo chanya. Je unawaza nini kila siku na unachukua hautua kwa kiasi gani? Je mawazo yako ni chanya au hasi?

Ukitafakari juu ya hayo utakupa mwangaza kwamba inataka kuelekea wapi juu ya maisha yako na taifa kwa ujumla. Maisha ya kufikiri mawazo chanya ndiyo yakupayo furaha ya moyo na mafanikio ya kweli. Kwani kwa kila jambo ambalo unalifanya linahitaji ubunifu ili kuwa kitofauti.

Mwandishi ni;  Afisa mipango Benson Chonya.
Simu: 0757 90 99 42
E-mail; 
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.