Nov 20, 2015
Jinsi Ya Kutambua Kipaji Cha Mtoto Wako Na Kukiendeleza
Hujambo mpenzi msomaji
wa DIRA YA MAFANIKIO na karibu sana katika siku ya leo kwa ajili ya kujifunza. Leo
katika makala yetu tutajifunza namna unavyoweza kutambua kipaji cha mtoto wako na
kukiendeleza. Na tunapozungumzia kipaji huu
ni uwezo anaokuwa nao mtu wa kufanya jambo fulani bila hata kwenda kujifunza shuleni.
Najua unaelewa hili vizuri.
Mara nyingi mtu
huzaliwa na uwezo huo na anapokwenda shule inakuwa ni rahisi kuweza kuuendeleza
kipaji hicho na kufanya jambo hilo kwa ufanisi sana. Sasa wewe kama
mzazi unawezaje kutambua kipaji cha mwanao na kukiendeleza? Ili kupata majibu
hayo ya nini unachotakiwa kufanya fuatilia yafuatayo katika makala hii;-
Kama mtoto wako anaongea kupita kiasi; Kuna watoto ambao huongea
kwa spidi sana na huwa hawachoki kuongea. Watoto hawa huongea mpaka anapokwenda
kulala na wengine huwa wanaongea mpaka usingizini. Huwa na tabia ya
kusimulia visa mbalimbali au kukueleza mzazi yote yaliyotokea mchana pengine
wakati wewe umeenda kazini au kwenye shughuli zako.
KUZA KIPAJI CHA MTOTO WAKO. |
Kwa mfano unapokutana na mtoto wa aina hii, hiyo hapo ni
dalili nzuri sana kwa watoto hawa kama kipaji chao kitaendelezwa vizuri na
kutokana na mwenendo huo wanaweza kuwa wanasheria,
waandishi wa habari, wanasiasa pamoja na Mc wa majukwaani.
Jinsi ya kuwasaidia watoto wa aina hii;
1. Epuka kuwakatisha
tamaa kwa yale wanayoongea na kama yanakera mfundishe kuongea yanayofurahisha.
2. Unaweza kumwambia akusimulie visa mbalimbali wakati wewe
ukimrekodi na baada usikilize pamoja nae. Hii humjengea kujiamini na
kuona kuwa anachofanya kinathaminiwa.
3. Msaidie pia aweze
kuwa msikilizaji mzuri kwa wewe kumsimulia wakati yeye akikusikiliza ana
kumwambia arudie ulichosema.
4. Mtengenezee tabia
ya kujiamini kwa kuepuka kumfokea au kumpiga mara kwa mara hususani kutokana na
kosa la yeye kuongea sana.
Asante sana mpenzi
msomaji wakati mwingine tutaangalia kipaji cha mtoto ambae kila jambo anataka
kulifanya yeye mwenyewe.
Makala hii imeandikwa na Deo Mukebezi Unaweza
kuwasilina naye kwa 0654627227
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.