google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 16, 2016

Ifahamu Mipango Hii, Kabla Ya Kuanzisha Biashara.

No comments :
Malengo ni lazima yaende sambamba na mipango ili kuweza kutimiza ndoto zako kibiashara, hata hivyo huenda ukawa haujanielewa, ipo hivi, mipango ni mtiriko wa namna ya kuyafikia malengo.

Pia malengo ni lazima yaanze katika ngazi ya chini kabisa, hapa nikiwa na maana ni lazima uanze na malengo madogo madogo au watalaamu wa masuala ya mafanikio huita (baby step). 

Malengo ya kibiashara ni njia sahihi ya kufanikiwa kwako kibiashara, kuna baadhi ya watu wao hufanya mambo ambayo hayana mipango na mikakati ambayo itawasababisha kuweza kutimiza ndoto zao ambazo wamejipangia katika masuala mazima ya kibiashara.


Na kufanya hivyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, kwani kila siku utajiona ni mnyonge, huna faida za kuendelea kuishi, hufai hii ni kutoka na kutoiona faida yeyote katika biashara ambayo unaifanya.

Yafutayo ni maswali muhimu ambayo ni muhimu kujiuliza  katika upangaji wa malengo ya uanzishaji kibiashara.

1. Eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.

Kuanzisha biashara mpya ni sawa na kununua nguo mpya dukani, kama ndivyo hivyo huna budi kila uwapo dukani ni lazima uangalie nguo ambayo itakutosha vizuri, kwani kama itakuwa hakitoshi na ukainunua hautaitumia na mwisho wa siku utajilaamu hata kudiliki kusema biashara hii nimechezea pesa zangu na meneno mengine mengi kama hayo.

Kama ndivyo hivyo basi kama ilivyo kwa ununuaji wa nguo, basi hata katika biashara ni lazima ufikirie ni wapi ambapo unataka kufanya biashara hiyo, baada ya kufikiria kwa umakini katika kipengele hicho, jambo ambalo ni muhimu ambalo ni vyema ukalizingatia ni kwamba ni lazima uende eneo hilo kwa ajili ya kufanya utafiti wa kutosha. 

Nasisitiza sana suala hili la kufanya utafiti kwani endapo hautafanya utafiti wa kutosha na ukaanzisha biashara eneo hilo ni lazima utajikuta unaingia kwenye lile kundi watu walalamikaji ambao husema wana gundu, wamelogwa, hawana akili za kibiashara na maneno mengine mengi kama hayo.

Hivyo ili kuepuka na maneno hayo ni lazima utafiti wa kutosha kuhusu eneo kwa ajili ya kufanya biashara ni lazima ufanyike mapema na majibu yake yawe ya uhakika. 

Zijue vyema gharama za mradi wako, kabla haujauanzisha.
2. Gharama za mradi.

Sifa kubwa za mfanyabiashara ni kuendelea kujiuliza maswali kila wakati, kama ndivyo inawezekana kabisa una mpango wa kuanzisha biashara fulani hapo mbele lakini kutokana na kufanya vitu vingi kimazoea unajikuta unashindwa kufanya tathimini ya gharama husika  biashara hiyo ambayo unataraji kuifanya.

Kutokana na changamoto hii ya kutojua thamani ya mradi mzima hapa ndipo ambapo lile kundi kubwa la watu huibuka na kuhoji eti afisa mipango nina shilingi milioni moja je, naweza kufanya biashara gani?

Swali kama hili majibu yake yapo wazi kwamba mtu huyo hana mawazo sahihi ya biashara na pia hajui thamani ya biashara ambayo anaitaka kuifanya.


Lakini ukweli ni kwamba baada ya kupata wazo bora la biashara na baada ya kujua ni wapi ambapo utafanya biashara hivyo jambo tatu  ni lazima ujiulize je ni gharama gani ambazo zitatumika katika kuanzisha na kuendesha mradi mzima?

Kufanya tathimini ya mradi inakufanya ujue ni wapi ambapo unaelekea. Pia watalamu wa mambo ya kibiashara wanazidi kutukumbusha kwa kutuambia ya kwamba taswira tuliyonayo  ya mafanikio ya kibiashara hutupekeka pale tunapopataka.

3. Namna ya kupanua mipango ya kijasiriamali.

Katika hili mfanyabiashara yeyote ni lazima ujihohiji je, anawezaje kupanua mipango ya kijasiriamaili. Hapa nikiwa na maana ya kwamba upanuaji wa mipango ya kijasiliamali huenda sambamba na kujifunza vitu vipya ambavyo vitakufanya uweze kukua kibiashara.

Kujifunza mambo hayo utajifunza kupitia semina, makongamano, mikutano mbalimbali  pamoja na kusoma ambapo kimsingi utajifunza mambo yahusuyo biashara kwa ujumla. 

Pia katika hili marafiki sahihi ambao wanafanya biashara wana mchango mkubwa sana katika kufikia lengo lako. Pia kuna usemi ambao unasema unaweza ukachagua marafiki ila huwezi kuchagua ndugu, hivyo chagua marafiki sahihi.

Hivyo niweke nukta kwa kusema ya kwamba maisha haya ni mazuri endapo utaamua kuchagua kile kilicho chema kwako.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya,
0757 90 99 42,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.