Mar 12, 2018
Kama Ukifanya Mambo Hayo Na Yasipokupa Mafanikio, Hutaweza Kufanikiwa Tena.
Katika harakati za kutafuta mafanikio yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa uyajue ili yakusaidie kukua kimafanikio. Kutokujua mambo hayo ndiyo chanzo kikubwa cha watu wengi kuweza kushindwa katika maisha ya mafanikio.
Leo
katika makala haya, sitaki kukwambia mambo yote hayo, nataka nikwambie mambo
matatu tu, ambayo kama ukiyafanya na ukijipa muda wa kutosha ni lazima yatakupa
matokeo ya kuweza kubadilisha maisha yako.
1. Anza na kidogo.
Ili
kufanikiwa na kuweza kufanya mafanikio yako yakazidi kuonekana hata kama huna
kitu, unatakiwa kujifunza kuanza na
kidogo ulichonacho. Si lazima kuanza na makubwa sana, anza na kile kidogo ulichonacho.
Unapoanza
na kidogo kitu ambacho hutakiwi kusahau ni kuweka nguvu zako zote hapo na
kujituma kisawasawa hadi kuweza kufanikiwa. Hakuna mafanikio yanayoanza kwa
mara moja na kuwa makubwa, mafanikio yote yanaanza kwa kidogo kidogo.
Kwa
hiyo kama unafikiri mafanikio makubwa, usifikirie mara moja kufika tu kule
unakotaka kufika, anzia kwanza pale ulipo na kisha utakuwa unakua taratibu kwa
jinsi siku zinavyokwenda. Hutakiwi kuwa na haraka, anza na kidogo na uwe
mvumilivu.
Hili
ni jambo mojawapo muhimu sana kama ukilifanya na kweli ukaamua kuanza na
kidogo, nakuhakikishia ni lazima utafanikiwa. Kikubwa usife moyo kwa kuanza
kwako na kidogo, endelea kusonga mbele na utafanikiwa sana.
2. Endelea kufanya.
Inawezekana
umejipa moyo na umekubali kuanza na kidogo, lakini nikwambie ukweli hata hivyo
mambo hayataenda kwa urahisi kama unavyofikiri, huko njiani utakutana na changamoto
na vizuizi vya kila aina ambavyo vitakukatisha tamaa sana.
Katika
wakati ambao utakutana na changamoto, naomba nikwambie, huo si wakati wa wewe
kuweza kukata tamaa au wakati wa wewe kuweza kusimama, endelea kusonga mbele,
hapo ndipo siri ya mafanikio ilipo.
Ndio
maana watu wenye mafanikio wanafanikiwa kwa sababu ya kukubali kuendelea
kusonga mbele bila kujali wanakutana na changamoto za aina gani na ambazo
zinawasumbua kwenye maisha yao.
Hata
wewe usikubali kusimama, usikubali kutoa sababu, toa matokeo yatakayoweza kukusaidia
wewe kuweza kufanikiwa. Amua kuendelea mbele bila kujali una maisha ya aina
gani mbele yako. ukiamua hivyo utafanikiwa nakwambia.
3. Wajibika.
Ni
kweli umeamua kuanza na kidogo ulichonacho na pia umekubali kuendelea ingawa
unakutana na changamoto, sasa usiishie hapo tu kubali kuwajibika kwa asilimia
zote kwa hicho unachokifanya.
Badala
ya kulaumu au kulalalamika, wewe weka juhudi, tengeneza thamani itakayozalisha
mafanikio na weka nguvu zako zote za uzingativu kwa hicho unachokifanya ili
uweze kupata mafanikio makubwa na ya uhakika.
Maisha
yako hayawezi kubaki hapo yalipo, kama kweli umeamua kuwajibika, maana
hautakubali kushindwa ni lazima utawajibika kupigania maisha yako mpaka yakupe
mafanikio yale unayoyataka na itakuwa hivyo.
Wengi
ukiangalia wanashindwa kwenye maisha kwa sababu hawakubali kuwajibika,
kikitokea kitu kidogo tu juu ya maisha wanalalamika sana na kuona kila kitu
basi kimeshindikana au kimeharibika.
Nikuhakikishie
tu, kama huna kitu na ukifanya mambo haya kwa muda mrefu na yasipokupa
mafanikio, hutaweza kufanikiwa tena. Haya ni ambayo ukiyafanya kwa kumaanisha
yanazalisha matunda ya mafanikio yako.
Zingatia
mambo haya, na yafanyie kazi ili kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.