Mar 20, 2018
Nguvu Ya Mafanikio Katika Kushukuru.
Wakati jambo moja linapokwenda hovyo kwenye maisha yako, chukua muda kidogo kushukuru kwa mambo mengi ambayo yanakwenda sawa kwenye maisha yako. Si kila wakati mambo yote yatakaa sawa kabisa, kama utakavyo wewe.
Inapotokea jambo moja
limekaa hovyo au halijaenda sawa kama wewe unavyotaka, shukuru kwa yale mazuri
kwanza. Huna haja ya kulaumu wengine au kijialumu sana wewe kwamba kuna sehemu
ambayo ulikosea.
Wakati huu unapoona
jambo lako linakwenda vibaya, weka nguvu na mawazo yako yote kwa hatua ambazo
utachukua na zitakusaidia kurudisha mambo yako kukaa sawa. Usichukue
hatua za kukurudisha nyuma hata kidogo.
Kila wakati fikiri juu
ya kukazana kuchukua hatua za kusonga mbele huku ukishukuru kwa hayo matokeo
ambayo yatakufanya ujifunze. Kwa lugha nyingine kuwa mtu wa shukrani kwa yote yanayokutokea.
Ukumbuke, tukiwa kama
bindamu kuna wakati tunakuwa ni watu wa lawama sana kuweza kulaumu kwa kile ambacho
kinatutokea na kuona ni kitu kibaya sana. Hata hivyo pia tunakuwa ni watu wa
kusahau kabisa kwamba yapo mambo mazuri ambayo tunayapata pia.
Moja ya sifa ya
mafanikio ya kweli yanapatikana kama utakuwa mtu wa shukrani. Unapojijengea tabia
ya kuwa mtu wa shukrani, inakusaidia kuweza kufanikisha mambo mengi, hii ni tabia
ambayo unaweza kuwa nayo bila kujali wewe ni nani.
Haihitaji kuwa na pesa
au kuwa na uwezo wa kipekee ili kuwa na shukrani. Mtu yeyote anaweza kuwa na
shukrani na unapokuwa unashukuru unajipa uwezo na mamlaka ya kuweza kushinda
mambo mengi kwenye maisha yako.
Ukiwa ni mtu ambaye unaishi
tu maisha yako pasipo kushukuru, ni jambo la hatari sana kwako na itafika
wakati maisha yako yatakuwa katika wakati mgumu sana. Hata ukiwaangalia watu
ambao hawana shukrani katika maisha yao, mafanikio yanawasumbua pia.
Ipo nguvu ya shukrani katika
mafanikio. Unaposhukuru kwa Mungu, unaposhukuru kwa siku ya leo kuifikia hicho
ni kitu kizuri sana kwako. Unaweza ukajitazama wewe mwenyewe kama ni mtu wa
shukrani au si mtu wa shukrani.
Unatakiwa kujua kabla hujalaumu,
kabla hujalalamika, na kuwaona wengine ndio wabaya wako, kwanza tumia muda
kidogo kushukuru yale mazuri uliyonayo. Ipo nguvu ya kubadili hata hali yako
inayoonekana mbaya kuwa nzuri ikiwa utakuwa mtu wa kushukuru.
Fanyia kazi somo hili na
uwe na mafanikio mema wakati wote, anza leo kwa kushukuru baraka na mafanikio
uliyonayo maishani mwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.