Mar 21, 2018
Huna Sababu Ya Kuendelea Kukosa Pesa, Kama Utapata Maarifa Haya.
Siri na muujiza wote wa mafanikio makubwa upo kwenye
maandishi. Wasomaji wazuri wa vitabu wanaelewa hili vizuri kwamba kwenye maandishi
ndio kuna siri nyingi za mafanikio ambazo watu wengi hawazijui.
Ukiwaangalia watu wengi, wanataka sana kuona
wakifanikiwa, lakini watu hao hao tena hawako tayari kupata maarifa ya
kuwasaidia. Hiyo inakuwa ni sawa na mtu anayetaka kusafiri kwa gari tena wakati
huohuo mtu huyo hataki kuweka mafuta.
Kama ndio kufanikiwa kwa namna hiyo hakupo,
mafanikio makubwa na ya kweli yanakuja kama una maarifa bora ambayo unayatumia
kila wakati kuweza kusaidia kufikia mafanikio hayo. Maarifa hayo hayapatikani
popote zaidi ya kujifunza.
Kuna wakati nimekuwa nikueleza faida za kujifunza,
ingawa bado kuna watu wanakuwa hawaelewi hili, lakini nikikazia hapa moja ya
faida kubwa ya kujifunza pia ni kupata maarifa ambayo yatakusaidia kifedha ukae
vizuri kama utajikita katika hilo eneo.
Kwa lugha nyingine huna sababu ya kuendelea
kuishiwa au kukosa pesa kila wakati kama kuna aina ya maarifa fulani ukiyapata.
Maarifa haya ya msingi ambayo yatakusaidia kwenye maswala ya pesa ndio
tunakwenda kujifunza hapa.
Kumbuka, huna sababu ya kuendelea kukosa pesa
kama utapata maarifa haya ya msingi. Ni jukumu langu ukifanyia kazi kile
utakachokwenda kujifunza uwe na uhakika utapiga hatua. Sasa twende pamoja
tuweze kujifunza.
1. Mtazamo
wa kimafanikio.
Kama wewe una mtazamo sahihi, mtazamo wa
kimafanikio ambao unakuwezesha si kuishi tu bali na kupata mafanikio ya ziada,
basi unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa na kuepuka na kuishiwa au kukosa pesa
kila wakati.
Kinachowaangusha wengi kwenye safari ya mafanikio
ni kwamba ni watu ambao hawana mitazamo ya kimafanikio, bali ni watu ambao wana
mitazamo ya kushindwa. Hiki ndicho kitu ambacho unatakiwa ujiulize una mtazamo
wa mafanikio au kushindwa?
Ukiona una mitazamo mingi sana ya kushindwa,
unatakiwa kubadilika mara moja na kutafuta namna utakavyoweza kujenga mtazamo
bora wa kukusaidia kufanikiwa. . Mitazamo una nafasi kubwa sana ya kubadilisha
maisha yako, hilo unatakiwa ujue.
2. Umiliki
wa muda kwa usahihi.
Watu wenye mafanikio wanajua vyema jinsi ya
kutunza muda wao vizuri na kupangilia kila kitu. Ni watu ambao hawaishi kwa
kubahatisha wanajua kwa uwazi muda ndio rasilimali ya kwanza kuitumia
kufanikiwa ikiwa hata huna kitu.
Hivyo hawako tayari kupoteza muda wa wengine na
hawako tayari pia kupotezea muda wao. Kwa maarifa haya huwasaidia sana kuweza
kufanya shughuli za ziada ambazo zinawaingizia kipato cha ziada.
Kwa muda kidogo wanaoupata hufanya jambo hili au
like la kuingiza kipato na mwisho wa siku hujikuta kupata pesa za kutosha. Hapa
ninataka kusema nini, ukijifunza juu ya kutunza muda ni nyenzo mojawapo muhimu
ya kukufanikisha.
3.
Mahusiano sahihi na watu.
Watu wenye mafanikio hawaishii tu kwenye kuwa na
mtazamo sahihi wa kimafanikio na kutunza muda wao vizuri. Ukiwafatilia utagundua
ni watu ambao wana mahusiano sahihi na watu. Kila wakati hutafuta watu sahihi
ambao wataenda pamoja.
Ni ukweli uliowazi unapokuwa na watu sahihi, si
rahisi sana wao kuweza kukuangusha. Hivi ndivyo watu wenye mafanikio wanavyojenga
mafanikio yao kwa kiasi kikubwa. Kwa sababu hii hata wewe ukifata maarifa haya
huna sababu ya kuendelea kuishiwa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.