Mar 8, 2018
Mafanikio Ya kweli Yanapatikana Hivi…
Hapo
ulipo najua unatafuta mafanikio ya aina fulani, lakini je ulishajiuliza mafanikio
hayo ukishayapata yatakuwa na msaada gani kwa wengine? Je, ni mafanikio ambayo
ukiyapata yatakuwa ya ubinafsi au yatakuwa ni baraka kwa wengine.
Hili
ni jambo la kawaida tu, lakini unapaswa kujiuliza na kulitilia maanani ili
kujua mafanikio yako unayoyatafuta unataka yawe msaada kwa wengine au unataka
yaweje? Ni wengi hawajiulizi jambo hili.
Lakini
kwa jinsi ilivyo, ili mafanikio yako yawe ya maana na yaweze kukusaidia sana
wewe, ni lazima mafanikio hayo yalete mabadiliko kwenye maisha ya wengine pia. Kwa
jinsi mafanikio yako yanakuwa msaada kwa wengine, na wewe kufanikiwa kwako
kunakua zaidi.
Hapa
nikiwa na maana kwamba kufanikiwa kwako wewe kuwasaidie na wengine kuweza
kupiga hatua za kimaisha. Hapa tena nikiwa na maana kwamba mafanikio yako wewe
yaweze kuleta mabadikio chanya kwa jamii.
Kama
unasema una mafanikio lakini wakati huo huo tukiangalia mafanikio hayo yanakufaidisha
wewe tu na hakuna msaada kwa wengine naweza nikasema hayo mafanikio yanaweza
kuwa ni batili.
Mafanikio
ya kweli yanaleta mabadiliko katika jamii na kuifanya jamii inayokuzunguka ifaidi.
Ukumbuke hapa simaanishi ugawe vitu hovyo au utoe msaada tu kila wakati, namaanisha
hakikisha mafaniko yako yawe ya msaada kwa wengine, hata kwa kuwasaidia watu
pia kutimiza malengo yao.
Ikiwa
utalenga sana kutafuta mafanikio kwa ajili yako tu na si kwa ajili ya wengine
pia, uwe na uhakika kuna wakati utafika utakutana na upinzani na hakuna mtu
ambaye ataweza kuja kukusaidia kwa sababu ya ubinafsi wako.
Unapokuwa
lakini unatafuta mafanikio huku akili yako imelenga kutafuta mafanikio ya ziada
na ambayo yatawasaidia na watu wengine pia kuweza kupiga hatua, basi fursa nyingi
zitafunguka kwa sababu ya kile unachokidhamiria
akilini mwako.
Hivi
ndivyo naweza kusema mafanikio ya kweli yanapatikana, yaani yanapatikana kwa
kuwa msaada kwa wengine. Huhitaji tu kuwa mbinafsi kwa kila kitu, hakikisha
msaada wako kwa wengine unaonekana.
Ifanye
jamii inayokuzunguka au watu wanaokuzunguka wajivunie mafanikio yako. Kuwa na
falsafa ya kwamba 'nikifanikiwa mimi, na wengine wamefanikiwa na pia kushindwa
kwangu mimi kuna wakawamisha na wengine pia.'
Ukiwaangaliwa
watu wenye mafanikio makubwa ni watu ambao mafanikio yao pia yanawanufaisha na
watu wanaowazunguka. Jaribu hata wewe kuchunguza kidogo hili utaliona kwa jinsi
lilivyo.
Ukiona
mtu anatafuta mafanikio lakini wakati huohuo ni mbinafsi sana, basi naweza
kusema mafanikio yake yana shaka kubwa ndani mwake. Watu wenye mafanikio ya
kweli, dalili ya kwanza ya mafanikio hayo ni kuwa msaada kwa wengine.
Najua
hapo ulipo umefanikiwa kwa kiasi fulani, sasa je, mafanikio uliyonayo ni msaada
na baraka kwa wengine? Sitaki unipe jibu lakini ukweli unaujua wewe. Weka
jitihada za kutafuta mafanikio ya kweli kwa kuwa msaada wa wengine na utafika
mbali.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.