Mar 27, 2018
Njia Sahihi Za Kubana Matumizi Yako Ya Pesa Kwa Faida.
Katika safari ya kufikia uhuru wa kifedha, zipo njia ambazo unaweza ukatumia na zikakusadia sana katika kutunza pesa zako na pesa hizo zikakusaidia pia katika uwekezaji. Wengi wanapoteza sana pesa zao pasipo ya sababu za msingi.
Ni muhimu
sana kama unataka kufika mbali kiuchumi ukabana matumizi yako ili pesa zako
zikusaidie kuwekeza. Ni njia zipi ambazo unaweza kutumia katika kubana matumizi
yako na ikakusaidia sana?
Zifuatazo Ni Njia Sahihi Za Kubana
Matumizi Yako Ya Pesa.
1. Tengeneza
bajeti katika matumizi yako na uifatilie. Bajeti hiyo utakayoitengeneza ndiyo
iwe mwongozo wako, usitumie pesa nje ya bajeti hiyo.
2. Tambua
matumizi yako ya lazima na muhimu ni yapi. Yapo matumizi ambayo ni ya lazima
sana, na yapo ambayo si lazima unatakiwa kuyajua.
3. Matumizi
yako yasizidi kipato chako. Hakikisha unafanya kila linalowezekana matumizi
yako yasiwe makubwa kuliko kipato chako.
4.
Fanya matumizi yako, baada ya kuweka akiba. Kila wakati jizoeze kuweka akiba na
kisha ndio uanze kufana matumizi yako.
5.
Usifanye vitu kwa lengo la kutafuta sifa, kama kununua vitu vya gharama, fanya
vitu kulingana na uwezo wako.
6. Fahamu
faida na sababu za kila jambo ambalo unalolifanya. Usifanye jambo lolote kwa
hasara. Kila jambo unalolifanya lifanye ukijua faida zake hasa ni zipi.
7.
Ishi karibu na eneo lako la kazi au biashara. Kuishi mbali na eneo lako la kazi
nako huko ni kupoteza pesa zako ambazo hazikutakiwa kupotea.
8.
Badala ya kwenda kula hotelini nunua vitu upike nyumbani. Tafuta muda na kisha
pika mwenyewe, vinginevyo utakuwa unapoteza muda wako bure.
9.
Usiazime vitu hovyo vya watu , jitahidi ununue vyako. Kuna wakati vitu vya
kuazima vinaweza vikawa ni chanzo cha wewe kutozwa pesa kama vikipotea.
10.
Sio lazima kila mtu anayeomba msaada ni lazima apatiwe. Kujifanya wewe kila
anayeomba msaada unampatia basi utakuwa unapoteza sana pesa zako pia
11.
Nunua mahitaji yako kwa jumla badala ya rejareja. Kununua mahitaji yako kwa
jumla inakusaidia sana kuokoa pesa zako ambazo kama ungenunua kwa reja reja.
12.
Nunua mahali ambapo unaweza ukapunguziwa bei. Usiamue tu kununua vitu kila
sehemu, nunua eneo ambalo unaweza ukapata punguzo.
13.
Katika nyumba unayoishi hakikisha unazima taa, feni, redio au Tv, usiviache
vikiwa wazi kama havitumiki. Kila wakti angalia vitu hivyo kama havina matumizi
zima.
14. Mvua
ikinyesha kinga maji ili uokoe gharama zisizo za lazima za maji. Hakuna haja ya
kununua maji, kama maji ya bure yapo.
15.
Pika chakula kwa idadi ya watu na usitupe chakula kinachobakia huo utakuwa ni
uharibifu. Ukipika chakula kwa mahesabu hakitaharibika.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA SHARIFF KISUDA
WA DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.