Mar 10, 2018
Kama Usipozijua Hali Hizi Vizuri, Utakuwa Mtu Wa Kuumizwa Sana Kwenye Maisha.
Katika maisha, zipo siku ambazo unakuwa umejawa na tabasamu na furaha tele, kutokana na mambo yako wewe kuweza kwenda vile kama unavyotaka. Halikadhalika, zipo siku ambazo zinakuwa za kilio na majonzi pengine kutokana na mambo kwenda hovyo.
Hali
hii ya kufurahi na kuona kila kitu sawasawa kwa sababu ya mambo yanatuendea
vizuri ipo na hali ya kuhuzunika wakati mambo yanakwenda vibaya pia ipo na
tunakutana nayo kwenye maisha. Kila mmoja wetu amewahi kukutana na hali hizi.
Kama
iko hivyo, unachotakiwa kujifunza ni hiki, wakati mambo yako yanakwendea vizuri,
furahi kwa wakati huo. Pia wakati mambo yako yanapokwendea vibaya jenga
uvumilivu, jikaze na amini wakati mzuri tena kwako unakuja.
Kosa
kubwa wanalolifanya watu wengi, ni pale hali za kushuka zinapotokea kwao, ukizingatia hali
hizi huambatana sana na maumivu makubwa, ni kule kujisahau na kuona kwamba
kama wameonewa au hawakustahili kabisa kupatwa na hali hizo.
Maisha yamejaa hali za kupanda na kushuka sana. Kama ikiwa bado hujabaini kwamba kuna kushuka na kupanda kwenye maisha kila wakati, basi kila unapokutana na matukio hasi, utakuwa ni mtu wa kuumizwa sana.
Maisha yamejaa hali za kupanda na kushuka sana. Kama ikiwa bado hujabaini kwamba kuna kushuka na kupanda kwenye maisha kila wakati, basi kila unapokutana na matukio hasi, utakuwa ni mtu wa kuumizwa sana.
Ukiangalia
chanzo cha watu wengi kuumia na kuteswa na maisha ni kwa sababu ya watu hawa
wao kujua maisha ni kupanda tu na hakuna kushuka. Watu hawa likitokea tukio dogo
tu la kushuka huwaumiza sana na kuwatoa nje ya mwelekeo wao.
Watu
wa namna hii kama ana biashara akipata hasara kidogo inamuuma sana na anaweza kuifunga.
Akikwaruzana na mpenzi wake pia inauma sana nakuona karibu kila kitu hakifai. Anasahau
kabisa kwamba maisha ni kupanda na kushuka.
Elewa ikiwa unataka kuishi katika dunia hii kwa amani na furaha, unatakiwa kujua
maisha ni kupanda na kushuka. Kwa hiyo inapotokea kupanda, wewe furahi, lakini
unapoona wakati wa kushuka jikaze na vumulia maumivu yote yanayoendana na
kushuka huko.
Kikubwa
unachotakiwa kukumbuka kwenye kushuka huko ambako kunaambatana na maumivu mengi
hakutaweza kukupata wewe moja kwa moja. Hata itokee umeumia na kulia vipi,
wakati wako wa kupanda utakuja pia.
Ikiwa
kungekuwa hakuna kushuka, basi kupada juu kusingekuwepo. Ikiwa kungekuwa hakuna
kupoteza, basi kufanikiwa na kushinda kusingekuwepo. Yote hayo yapo kiasili ili
kukupa nguvu na hamasa ya kuweza kuendelea mbele.
Hata
kama imefika wakati unaona giza totoro na hakuna tumaini lolote la maisha yako,
tambua kabisa asubuhi yenye nuru inakuja na hakuna ambaye atakuwa mtu wa kukuzuia,
hivyo usikatishwe na tamaa kwa hilo.
Haijalishi
ni kitu gani ambacho umekutana nacho kwenye maisha yako. Haijalishi siku yako
imekwenda vipi. Kikubwa unachotakiwa kujua zote hizo ni hali ambazo unatakiwa
kuzitambua ili uishi maisha ya ushindi na furaha.
Kila
wakati weka akilini kwamba maisha yana kupanda na kushuka. Hizo ni hali ambazo
zipo. Usiruhuu hata kidogo hali yoyote ikuumize kupitiliza. Jifunze kukabiliana
na kila hali kwa wakati wake ili usiweze kupoteza mwelekeo kwenye maisha yako.
Amua
leo kuwa mtawala bora wa hali hizi zote mbili. Ukiweza kuzitawala vizuri hali
hizi, basi maisha yako yatakuwa na furaha na amani nyingi na hautaweza kushi
kwa majuto ya kupitiliza kama wengine wanavyoishi hivyo.
Kila
kitu kinawezekana, tafakari na chukua hatua.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.