Mar 15, 2018
Mambo Kumi (10) Unayopaswa Kuyazingatia Katika Safari Yako Ya Mafanikio.
Yapo mambo ya msingi ambayo kila msaka mafanikio ni lazima ayafahamu katika safari yake ya mafanikio, na mambo hayo ya msingi yatamfanya mtu huyo aweze kuishi katika misingi hiyo ya mafanikio. Na mambo hayo ni:
1. Njia ya kuelekea kwenye mafanikio na
njia ya kushindwa katika kufikia mafanikio mara nyingi
zinafanana, hivyo ni vyema kila wakati ukajifunza kuchagua njia sahihi ya kukupeleka
kwenye mafanikio unayoyoyahitaji.
2. Mara zote ikumbukwe ya kwamba fursa
zote unazoziona na usiziona huwa hazitokei kama ajali bali hutengenezwa hivyo
jifunze kutengeneza fursa ili uweze kufikia katika kilele cha mafanikio yako.
3. Kutengeneza mafanikio pekee yake
haitoshi, bali jifunze pia kujitengenezea thamani kubwa katika jamii ambayo
inakuzunguka, Thamani hii ina manufaa sana kwako na jamii inayokuzunguka.
4. Kama hautakuwa tayari kupoteza au kupata
hasara katika jambo lolote unalolifanya sahau kabisa kuhusu mafanikio.
5. Kila wakati naomba utambue ya kwamba
mafanikio hujengwa na msingi kwa kutoka katika mazoea uliyoyazoea.
6. Mara zote achana na tabia ya kuzungumza
sana kuhusu malengo yako, bali unatakiwa kuyaweka malengo
hayo katika vitendo.
7. Hakuna siri za mafanikio isipokuwa na
maandalizi thabiti ya mafanikio hayo, kufanya kazi kwa bidii na
kujifunza kutokana na makosa unayopitia.
8. Kama kweli unataka mafanikio na ili
ufikie mafanikio hayo tambua unatakiwa kutokuwa mtu wa visinginzio hivyo epuka
visingizio kila wakati.
9. Mafanikio sio ufunguo wa furaha bali furaha
ndiyo ufunguo wa mafanikio, hivyo ili uweze kuitengeneza furaha hiyo unatakiwa
kupenda hasa kile unachokifanya.
10. Kushindwa katika jambo unalolifanya isiwe kigezo ya kwamba
huwezi kufanikiwa, bali unaposhindwa kama jambo fulani ndiyo fursa
pia mara zote kumbuka kuanguka mara nane ni fursa ya kuinuka mara
tisa.
Mpaka kufikia hapo
sina la ziada cha msingi ni kuyazingatia hayo ambayo nimekueleza siku ya leo.
Nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango, Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.