Mar 28, 2018
Usipoliangalia Jambo Hili Kwa Umakini Litakufanya Ushindwe Kufanikiwa.
Kati
ya kitu kimojawapo ambacho kitakupelekea wewe kuanguka kwenye maisha yako kama
usipokiangalia vizuri na kukijua jinsi ya kukabiliana nacho, ni kukatishwa tamaa. Usipokuwa
makini na kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile lazima ukwame.
Maisha
ya watu wengi yameishia kati na yamekuwa maisha ya ndoto na yale matumaini
makubwa waliyokuwa nao watu hao mwanzoni yamepotea kabisa, yote hiyo ni kwa
sababu ya kukatishwa tamaa iwe na wengine au wao wenyewe.
Inapifika
mahali kwenye maisha yako ukaona kabisa kwamba wewe ndio umekata tamaa, naomba
nikwambie kwamba wewe ndio basi tena kufanikiwa. Hutaweza kufanikiwa mpaka
urudi kwenye matumaini ya kuamini kwamba utafanikiwa tena.
Kukatishwa
tamaa kwa namna yoyote ile kunakupotezea sana nguvu zako ambazo ulikuwa
umejiandaa nazo kwa ajili ya kuchukua hatua. Kwa bahati mbaya kukatishwa tamaa
kwenyewe kunaweza kukawa kwa maneno tu, ambayo umeyasikia na hayana ukweli.
Ndipo
hapo ambapo unatakiwa ujiulize ni kwa jinsi gani maneno hayo yana nguvu au yana
ukweli na ule uhalisia. Kama una nia kweli ya kufanikiwa unayo, inatakiwa uzibe
masikio kabisa na usisikie kukatishwa tamaa kwa namna yoyote kukitokea kwako au
kwa wengine.
Ili uwe
mshindi wa mafanikio hutakiwi kuwa mtu wa kukata tamaa. Unatakiwa uwe mtu ambaye
una roho ngumu, lakini si roho ya kuwakomoa watu, bali ile roho ya kuamua
kutokatishwa tamaa na kitu chochote kile zaidi ya kutaka kuona ukifanikiwa.
Unapaswa
kuelewa, juhudi yoyote kwenye maisha yako iwe juhudi ya masomo, juhudi ya
kutaka kufikia mradi fulani au juhudi ya aina yoyote ambayo lengo lake ni
kukufanikisha, juhudi hiyo ni lazima huwa inakutana na kukatishwa na tamaa.
Utakuta
juhudi zako zinakatishwa tamaa na mazingira na kufika mahali unaona duu hakuna
kinachofanikiwa tena hapa. Pia wakati mwingine utakuta juhudi zako zinakatishwa
tamaa na wewe mwenyewe kutokana na mawazo yako au wale wote wanaokuzunguka.
Kitu
cha namna hii kinapokutokea si bahati mbaya, bali naweza nikasema kwamba unatakiwa
ujue juhudi yoyote ile kwa namna moja au nyingine upo muda wake utafika inakuwa
inatishwa tamaa na vitu vingi sana na kama usipokuwa makini utakwama.
Hata
hivyo unachotakiwa kuelewa hapa, huwezi kukwepa kwenye maisha yako kukatishwa
tamaa kwa namna yoyote ile. Kitu pekee ambacho unaweza kukifanya hasa pale
unapokatishwa tamaa je, unachukuliaje kukatishwa tamaa huko?
Fanya
kukatishwa tamaa kwako iwe sababu ya kujitoa zaidi mpaka kuona ndoto zako
zinatimia. Usikubali kuachia ndoto zako kirahisi eti kwa sababu umekatishwa tamaa.
Tumia kukatishwa tamaa kokote kule kunakokutokea kwako kwa faida.
Ukiwa
mwangalifu na ukajua jinsi ya kukabiliana na kukatishwa na tamaa, utaweza
kuzifikia ndoto zako, lakini usipojua vizuri jinsi ya kukabiliana na kukatishwa
tamaa, jambo hili litakusumbua sana na utashindwa kwenye maisha yako.
Je,
kukatishwa tamaa kwako unakuchukuliaje kwenye maisha yako, ni chanzo cha
kufanikiwa au kushindwa kabisa? Usisite kutoa maoni yako.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.