Mar 31, 2018
Fursa Na Mipango Peke Yake Sio ‘Tiketi’ Ya Kukupa Mafanikio.
Kuna watu wanaofikiria, kwa kuwa wana mipango mizuri na kwa kuwa wana fursa nzuri basi hapo mafanikio ndio tayari. Kama una ndoto za namna hiyo hata wewe, nikwambie unajidanganya na bado haitoshi hiyo, ila unahitaji kitu cha ziada ili kufanikiwa.
Najua
unao uwezo wa kufanya kile unachokitaka, lakini uwezo huo bado hautoshi. Najua unayo
fursa ya kuweza kufanikiwa lakini fursa hiyo bado pia haitoshi. Pia najua unayo
mipango mizuri sana ya kukusaidia
kufanikiwa, lakini mipango hio pia haitoshi.
Ni nini
kinachotosha au nini sasa unachotakiwa kufanya ikiwa unayo mipango, uwezo na
fursa lakini tu haitoshi? Kinachotosha kwako ni wewe kuamua kuchukua hatua. Hata
kama una kila kitu kizuri cha kukufanikisha sana kama huchukui hatua ni sawa na bure.
Hatua
zinatakiwa ili uwezo ulionao ufanye kazi vizuri. Hatua zinatakiwa ili uweze
kutumia fursa zako vizuri na pia hatua zinatakiwa ili uweze kufanya mipango yako
vizuri. Kujidanganya kwako wewe una mipango halafu huchukui hatua ni kazi bure.
Hatua
ndogo ambazo utakazoamua kuchukua ni za maana kwako sana kuliko mipango mikubwa
uliyonayo ambayo huifanyii kazi. Kipi ambacho unasubiri, unatakiwa kuanza
kuchukua hatua sasa za kukupeleka kwenye ndoto zako hata kama ni kidogo sana.
Leo ni
siku ambayo unaweza ukaamua kutumia kila aina ya fursa iliyopo mbele yako kubadili
maisha yako. Leo ni siku ambayo unaweza ukaitumia mipango yako na uwezo wako wote
kukusaidia kufanikiwa.
Chochote
ulichonacho hakina maana, chochote ulichonacho hakiwezi kutosha kama hutaweza
kuchukua hatua. Kitu cha msingi kabisa ni kuchukua hatua za kubadilisha ndoto
zako. Hatua ndizo zitakazokupa kile ukitakacho.
Lakini
kitendo cha kuringa au kujidai eti kwa sababu wewe una mipango mizuri na
ukaishia kwenye mipango hiyo, nakwambia hiyo itakupelekea kwako itakuwa ni
ngumu sana kuweza kuchukua hatua za kimafanikio.
Washindi
katika mafanikio wanajua vizuri mafanikio makubwa yanakuja kwa wewe kuchukua hatua.
Hizo zote zingine zinaweza zikawa ni kelele, lakini kufanikiwa kwako kunatengenzwa
sana na wewe kuweza kuchukua hatua.
Huhitaji
kuendelea kuwa na matamanio ya ndoto zako wakati wote, unachotakiwa kukifanya
sasa ni kubadili matamanio hayo na kuwa ya kweli. Hiyo ukumbuke lakini haiwezi
kutokea mpaka uchukue hatua.
Yajaze
maisha yako hatua na itafika mahali utaona matunda ya kile unachokifanya, hata
kama kitu hicho ni kidogo sana. Hakuna kinachoshindikana kwenye kuchukua hatua.
Mafaniko na mabadiliko katika maisha ni lazima yaonekane.
Hatua
ndio kitu cha kitakachokufanya ufanikiwe. Kuwa na wazo, mipango na fursa hiyo
haitoshi kwamba ndio ‘tiketi’ ya
mafanikio. Unatakiwa kuchukua hatua, unatakiwa kufanya kazi ili uweze
kufanikiwa, lakini sio kusema umefanikiwa na kumbe bado.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.