Mar 5, 2018
Maisha Uliyonayo Yako Hivyo Kwa Sababu Hii Kubwa.
Jiangalie hapo ulipo, jiangalie nini ulichonacho na nini ambacho huna, ukijiangalia hapo ulipo na hali uliyonayo, basi ni matokeo ya kitu kimoja tu, ambacho si kingine bali vipaumbele ambavyo uliviweka wakati wa nyuma.
Vile
vipaumbele ambavyo ulikuwa umeviweka kwenye maisha yako kwa siku za nyuma, hivyo
ndivyo vimekufikisha hapo ulipo mpaka sasa. Ukiangalia mambo uliyokuwa ukiyazingatia,
ndio yamekupa matokeo hayo.
Hakuna
ambacho umekipata kwa bahati mbaya, kila kitu umekipata kwa sababu ya vipaumbele
vyako. Huhitaji kubisha au kushangaa ni kitendo cha wewe kuchunguza kidogo tu
na utagundua ni kweli vipaumbele vyako ndivyo vilikufikisha hapo.
Kwa hiyo
uwe una hali mbaya kiuchumi, au uwe na maisha yeyote yale uliyonayo. Maisha hayo
yametengenezwa na kitu kimoja tu ambacho ni vipaumbele vyako na sio kitu
kingine chochote kile ambacho pengine unakifikiri.
Kama
unajiona una maisha magumu na huridhiki nayo hata kidogo, kitu cha kwanza cha kuanza
nacho ni kwa wewe kukazana kubadili vipaumbele vyako. Unapokazana kubadili
vipaumbele vyako ndipo unatengeza mafanikio yako hapo.
Inawezekana
vipaumbele ulivyokuwa navyo, ndivyo vimekufanya ukawa na maisha magumu sana. Sasa
tatizo la watu wengi hawajui kufatilia vipaumbele vya maisha yao na wanaona
maisha yao magumu tu pasipo hata kuelewa chanzo ni nini.
Jikague
mwenyewe na ujiangalie vipaumbele vyako viko sahihi? Kama unaona vipaumbele vyako
viko sahihi, basi kazana sana kufatilia vipaumbele hivyo mpaka viweze kukusaidia
kuweza kufanikiwa na kufika mbali kimafanikio.
Watu
wengi ukiangalia maisha yao yanakwama kwa sababu ni watu ambao wana vipaumbele
ambavyo haviwasaidii kuweza kufikia ndoto zao za kimafanikio hata kidogo. Kwa kifupi
vipaumbele vyao vinawadondosha.
Hakikisha
vipaumbe ambavyo unajiwekea vinakwenda kubadilisha maisha yako na maisha yako
sio lazima yabadilike sasa hivi ghafla, ni kwa kidogo kidogo itafika muda maisha yako
yataweza kubadilika na kuwa bora zaidi.
Unatakiwa
kujiuliza kila wakati je, vipaumbele vyangu hivi vinanisaidia kufikia mafanikio
yangu? Au vipaumbele vyangu hivi havieleweki? Ukijua hivyo tafuta vipaumbele
ambavyo viko sahihi na vyenye manufaa kwako.
Usikubali
kuwa miongoni mwa watu ambao wanaharibu maisha yao kwa sababu ya kukosa vipaumbele
vya msingi. Kuwa miongoni mwa watu ambao watatengeneza maisha ya mafanikio kwa
sababu ya kujenga vipaumbele sahihi.
Nikutakie
siku njema na wakati mwema katika kutekeleza vipaumbele vyako ili vikusaidie
kufikia malengo yako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.