Mar 2, 2018
Acha Kusubiri Hali Ya Hatari, Badili Maisha Yako Sasa.
Antony
Burges alikuwa na umri wa miaka 40, kipindi ambacho daktari wake alimwambia
hawezi kupona tena ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua. Taarifa hiyo ya daktari ilisisitiza kwamba ni lazima Antony afe tena
ndani ya muda wa mwaka mmoja.
Kwa
Antony ilikuwa ni habari mbaya sana kwake na tena iliyomshtua. Kilichokuwa kikimsikitisha
Antony si kwa sababu anakwenda kufa, bali alisikitishwa na ujio wa kifo chake
huku akiwa hajatimiza kabisa ndoto zake.
Alichokuwa
akiwaza kila wakati inakuwaje anakwenda kufa wakati ndoto zake hazijatimia? Kutokana
na maswali hayo ndiyo yalimfanya arudi tena kwa daktari kuumuliza ni kweli
hawezi kabisa kupona ugonjwa huo wa kansa?
Lakini
katika hali ya kusikitisha Antony alipewa jibu lile lile na kuambiwa
isingewezekana kupona, ni lazima angekufa. Juhudi za madaktari bingwa ili
kuokoa maisha yake wakati akiumwa zilikuwa zimefika ukomo, ilikuwa ni lazima
afe.
Antony
alirudi nyumbani kwa masikitiko mkubwa na akiwaza kwamba sasa anakwenda kufa
kifo cha aibu. Anakwenda kufa akiwa maskini ambaye hajaweka historia yoyote,
hicho ndicho kilichomkera.
Acha kusubiri hali ya hatari, fanya kitu cha kubadili maisha yako kila siku. |
Akiwa
kwenye chumba chake anachoishi huku akiwa katika hali ya kukosa matumaini ya
kuishi, alikumbuka kitu na kuapa asingeweza kufa bila
kuacha kitu chochote cha kukumbukwa duniani.
Hapo
ndipo alipokumbuka kwamba anakipaji cha kuandika. Aliapa ni lazima afanye kitu
hata kama muda wa kuishi umekwisha. Ilikuwa ni lazima aandike ‘novel’ ambazo zitasomwa wakati akiwa amekufa.
Hicho ndicho kilichotokea.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja akiwa anasubiri kifo chake, Antony Burges aliweza
kuandika ‘novel’ tano, ambapo kitu
hichohicho alishindwa kukifanya katika maisha yake yote mpaka pale alipopigiwa kengele
ya kifo.
Ilikuwa
sio rahisi kukamilisha kazi hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, lakini
iliwezekana. Unajua ni kwa nini? ni kwa sababu kifo kilikuwa kinamsubiri, na ilikuwa
ni lazima akamilishe malengo yake kabla hajafa.
Hata
hivyo lakini, zikiwa zimebaki siku chache ili kipindi cha mwaka mmoja
kikamilike na afe kama daktari alivyodai alirudi hospital tena. Daktari aliyemkuta,
alimfanyia vipimo upya na alimwambia uwezekano wa kufa katika kipindi hicho cha
mwaka mmoja haupo tena.
Kwa
taafrifa hiyo mpya kutoka kwa daktari ilimpa Antony nguvu mpya, nuru mpya na
tumaini jipya la maisha. Antony kwa hasira za mafanikio aliamua sasa kuandika
vitabu vingine vingi kwa nguvu zaidi. Aliweza kuandika vitabu vingine zaidi ya
70, mara baada ya kupona kutoka kifo chake.
Aligundua
swala la kusubiri mpaka itokee hali ya hatari ndio ufanye kitu katika maisha
yako ni baya sana. Utakuta wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa
sababu ya kufanya mambo yao mpaka wasubiri taa nyekundu.
Wengi
wetu ukichunguza katika maisha bado tupo kama Antony wa zamani, ni watu ambao
utakuta tumeficha vipaji na uwezo mkubwa ndani yetu bila kuutumia. Utakuta tunakutakuja
kuutumia uwezo huo mpaka pale kengele ya hatari igonge vichwani mwetu.
Jiulize
ni mara ngapi hutaki kufanya mambo yako kwa wakati mpaka usukumwe? Kama unaishi
maisha ya kusukumwa sukumwa hadi hali mbaya zikutokee mafanikio yanakuwa magumu
sana kuonekana kwako.
Yapo
mambo kadhaa ambayo tunaweza kujifunza kupitia Antony Burges, miongoni mwa hayo
ni:-
Kwanza,
jifunze kutumia uwezo wako wote ulionao unapokwa hai. Acha kusubiri hali ya
hatari ndio uanze kutumia uwwezo wako kukufanikisha. Acha kusubiri watoto
wamefukuzwa shule ndio uanze harakati za kutafuta ada.
Kwa
muda na rasilimali yoyote uliyonyo itumie vizuri kwa wakati ili ikusaide kukupa
mfanikio unayoyataka kwenye maisha yako. Unao uwezo mkubwa sana, utumie wakati
wote kuleta mabadiliko katika maisha yako na ya wengine.
Pili,
hata siku moja usikatishwe tamaa na kitu chochote hata kama ni kifo. Katika mazingira
magumu ambayo Antony alikuwa ameshaambiwa ni lazima atakufa, lakini aliweza kufanya
kazi bila kufikiria hilo na kufanikisha ndoto yake.
Alichokuwa
akitaka kuona ni ndoto zake zinatimia ilikuwa haijalishi mazingira anayopita ni
ya aina gani. Alikuwa anajua kabisa siku zake za kuishi ni chache, lakini
ilikuwa ni lazima apigane mpaka mwisho.
Tatu,
wakati wote ukitaka kuwa mshindi katika kila eneo acha kusubiri hali ya hatari,
fanya sasa kutimiza ndoto zako. Pigania ndoto zako wako bado ukijana. Pigania ndoto
zako wakati bado una afya na nguvu za kutosha. Pigania ndoto zako mpaka tone la
mwisho.
Inapotokea
mazingira ya kukatisha tamaa, usikubali mazingira hayo yawe ndio eti sababu ya
wewe kushindwa. Ukisubiri kama Antony kutokufanya kitu utatakuwa unajichelewesha
mwenyewe kufikia mafanikio yako.
Kila
wakati kumbuka mafanikio yako yanawezekana, badili masiha yako kwa kuwa na
fikra sahihi.
Nikutakie
siku njema na anasante sana kwa kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Washirishi na wengine waweze
kupata maarifa haya bora.
Pia
napenda kukukaribisha rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi.
Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU,
kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713
04 80 35 ili uanganishwe.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.