Mar 22, 2018
Kama Utachagua Njia Hii Ya Mafanikio, Hutaweza Kufanikiwa.
Hakuna kitu rahisi kama kutokuamua kufanya kitu. Kusema inaweza ikawa rahisi kwamba nitafanya jambo hili, lakini kuchukua hatua inakuwa ngumu, hiyo yote inaonyesha kutokufanya kitu ni jambo rahisi sana ambalo kila mtu analiweza.
Mara
nyingi pia mambo rahisi hayawezi kukupa kitu bora. Kila unachotaka kukifanya
ukigundua kwamba kitu hicho ni rahisi na kinafanywa na kila mtu, ujue kabisa
kitu hicho si rahisi sana pia kutoa matokeo yale yaliyo bora.
Ni rahisi
sana kuwa na matumaini ya matokeo bora kwa kile unachokifanya, lakini uelewe
kabisa ili hayo matokeo uweze kuyapata unahitajika kwanza kuweka juhudi na
kufanya kazi kweli na si kutegemea rahisi.
Ukiona
una mawazo ya kupata mafanikio kwa urahisi sana, kila kitu unakitaka kwa
urahisi na unaamini hivyo kabisa, ujue kabisa kushindwa hutaweza kukwepa. Ili kufanikiwa
inatakiwa juhudi na si swala la urahisi kama unavyowaza.
Ni rahisi
sana kuwakosoa watu wengine kwa yale mambo wanayoyafanya, na ukijiangalia wewe hufanyi
kitu na mbaya zaidi huwezi kufanikisha jambo lolote lile kwa kuwakosoa watu
wengine wanaochukua hatua.
Ukitaka
upige hatua za kimafanikio, huhitaji kuwa mtu wa kukosoa sana wengine. Ukiona unaanza
kuwakosoa na wakati wewe huchukui hatua, unatakiwa kukaa kimya tu, kwani hakuna
unachokifanya na unataka kufanya rahisi tu kukosoa ambako si msaada kwako.
Mafanikio
ya kweli yanakuja na wale watu ambao kweli wameamua kuchukua hatua na si kuwa
wakaaji ambao hawachukui hatua ila kazi ni kukosoa. Nikwambie tu unaweza
ukawakosoa wengi, lakini yote hiyo haikusaidii kitu, unatakiwa kuchukua hatua.
Ikiwa
unataka kweli kufanikiwa unatakiwa kufuata na njia ngumu, njia ambayo si rahisi
lakini ambayo mwisho wa siku itakufanikisha. Kuchukua njia rahisi au kuamua
kufanya mambo rahisi rahisi ujue kabisa huko ndiko unapotea kimafanikio.
Fanya
maamuzi ya kutokuchagua njia rahisi ya mafanikio yako. Njia rahisi ya mafanikio
haina msaada na haiwezi kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa. Wengi wanapitia njia
hii na wanaishia kukwama sana na kutokuweza kufanikia kabisa.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.