Mar 18, 2018
Ukishindwa Kuendana Na Kitu Hiki, Sio Rahisi Kwako Kuweza Kufanikiwa.
Kushindwa kwenye maisha wakati mwingine kunakuja si kwa sababu huna malengo au huchukui hatua, bali kuna wakati unashindwa kwa sababu ya kushindwa kuendana na mazingira yanayokuzunguka.
Kuna wakati
naweza nikasema unaweza ukashindwa kuendana na mazingira ya aina tofauti
tofauti kama vile mazingira ya ushindani katika biashara na mazingira
mengineyo ambayo yanakupa upinzani sana.
Kwa vyovyote vile ili uweze kujihakikishia ushindi wa mafanikio, unatakiwa uwe ni mtu wa kuendana na mazingira yanayokuzunguka yaani uwe na ule uwezo wa ‘ku- adapt.’ Hali yoyote unapokutana nayo ni lazima kwako ujue jinsi ya kuishinda.
Kwa vyovyote vile ili uweze kujihakikishia ushindi wa mafanikio, unatakiwa uwe ni mtu wa kuendana na mazingira yanayokuzunguka yaani uwe na ule uwezo wa ‘ku- adapt.’ Hali yoyote unapokutana nayo ni lazima kwako ujue jinsi ya kuishinda.
Vitu vyote
vinavyoshindwa kuendana na mazingira mara nyingi huwa vinashindwa sana au hata
kuweza kufa kabisa. Hili unaweza ukaliona kwa wanyama na hata mimea pia.
Viumbe hivyo hujitahidi sana kuendana na mazingira halisi.
Hata wewe unapokutana na
tukio au hali yoyote hata kama hali hiyo inaonekana ni ngumu sana kwako lakini
unatakiwa kujua jinsi ya kukabilina nayo hali hiyo. Ukishindwa kukabiliana na
hali hio utashindwwa tu huko mbeleni.
Kuelewa vizuri hili,
hebu angalia mimea ambayo inakua jangwani ni kitu gani ambacho hutokea? Ni kwamba
mimea hiyo huweza kumudu kuweza kuishi kwenye mazingira kwa kuweka mizizi
mirefu au kuwa na miiba sana.
Inabidi na wewe ujue,
unapokutana na kipindi kigumu kwenye maisha yako ujue namna ya kuweza kukabiliana
na hali hiyo na kuweza kuishinda. Kama utakuwa ni mtu wa kulia, nakuhakikishia
utaweza kushindwa kwa kila kitu.
Badilika kulingana na
mazingira unayokutana nayo. Usikubali kila wakati kuwa mtu yule yule ambaye
huna uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira unayokutana nayo. Kama unapitia
kipindi kigumu cha maisha komaa kweli hadi ushinde.
Nakukahakikishia utakuwa
mshindi katika maisha kama kila wakati wewe utakuwa ni mtu ambaye unaweza
kubadilika kulingana na mazingira yako au kuwa na ule uwezo wa kuendana
kulingana na hali halisi.
Kama hunielewi vizuri yaani
hapa, namaanisha unatakiwa uwe na uwezo wa kuishi popote na kufanya chochote kama
inatokea mazingira uliyopo yanakulazimisha wewe kuweza kufanya hivyo, hiyo
itakuwa na msaada mkubwa sana kwako.
Usilie au kuhuzunika kwa
sababu uchumi ni mbovu au unaona mambo siku hizi yamekuwa tofauti na zamani.
Unatakiwa kukazana na kuweka juhudi sana hadi kuweza kufanikiwa. Hiyo yote itafaa
kama utaendana na hali inayokuzunguka.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.