Mar 30, 2018
Jikumbushe Kila Mara Mambo Haya Ili Yakupe Hamasa Ya Kufanikiwa.
Najua hapo ulipo, kwa chochote kile unachokifanya, lengo lako kubwa ni kuhitaji maisha mazuri na bora. Kuna maisha ambayo najua unayatamani, maisha hayo unataka kuyafikia na pengine una kiu nayo sana.
Hata
hivyo kabla hujafikia mahali ukayatamani sana maisha hayo unayoyataka, hebu
jiulize, kwa jinsi maisha yako unavyoyaendesha na kwa jinsi unavyoendesha
maisha yako kwa kila siku je, jinsi hiyo inakurushu kuyapata maisha hayo?
Ni wajibu
wako kujikagau na kujiangalia wewe mwenyewe hatua kwa hatua kwa jinsi
unavyoishi maisha yako. Kama kuna kitu unaona hakijakaa sawa na unaendelea nacho
ujue kitu hicho kitakunyima kuweza kufanikiwa.
Mwenendo
wa wewe jinsi unavyoishi siku moja tu, unaweza ukatoa picha kamili ya kwamba
unafanikiwa au hufanikiwi bila kujali ni kitu gani ambacho unakifanya. Mara nyingi
nasema kwenye kufanikiwa hakuna uchawi ni kanuni na sheria tu.
Unaweza
ukajiuliza mwenyewe kama kweli unataka mafanikio hasa, je, ni kweli mafanikio
hayo utayapata kwa jinsi unavyopoteza muda hovyo. Jiulize wewe mwenyewe na
usimwambie mtu yeyote, lakini ujipe majibu sahihi pia.
Tena
jiulize, kama unataka mafanikio ni kweli mafanikio hayo utayapa kwa wewe
kuendelea kuwa mzembe na wala huweki juhudi zinazotakiwa? Je, ni rahisi kuyapata
mafanikio hayo ambayo unayataka?
Na tena
jiulize ama kweli unataka mafanikio, je mafanikio hayo utayapa kwa mwendo huo
ambao unao ambao unaishi kiholela na hutaki kujifunza mambo mapya na hata kujichanganya
na watu wengine?
Ongeza
tena swali lingine hapo, kama unataka kweli mafanikio, je, mafanikio hayo
utayapata kweli kwa jinsi unavyotapanya pesa zako huko na huko na kushindwa
hata kujiwekea akiba ambayo itakusaidia?
Hutakiwi
haya maswali ujiulize huku watu wengine wakisikia, unatakiwa kujiuliza wewe na
kuangalia kule unakokwenda na pale ulipo ni nini unachokifanya, hatua zipi
unazozichukua na zinakupeleka kwenya mafanikio au la.
Ili kufafanikiwa
na kufikia mafanikio siku zote unatakiwa sana wewe kuwa makini kwa kila hatua.
Unatakiwa kuwa makini kwa kuangalia mwenendo wako. Watu wengi wanapotea kwenye
safari ya mafanikio kwa sababu si watu makini na wanakuwa wapo wapo tu.
Amua
kuwa ‘siriazi’ kufatuta mafanikio
yako na kuamua kuachana na kila aina ya uzembe ambao umekuwa ukikukwamisha hata
wakati mwingine pasipo wewe kuweza kujua. Tupilia mbali uzembe huo na
jikumbushe misingi ya mafanikio jinsi ilivyo.
Kila
hatua unayoipiga,ujue kabisa ni kitu gani ambacho unakifanya, kuwa makini na
kila hatua, hiyo itakuwa ni njia bora na ya pekee sana kuweza kukusaidia kuweza
kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa uyatakao.
Ukipoteza
umakini kwenye maisha yako na ukasahau kujikumbusha mambo ya kukusaidia
kufanikiwa, basi hicho ni chanzo kikubwa sana cha wewe kuweza kuanza kupotea na
kushindwa kuweza kufanikiwa. Unataka kufanikiwa usipoteze umakini.
Usikubali
kushindwa, usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio eti kwa sababu ya
kuendesha maisha yako kiholela. Kuwa makini na kila kinachokuzunguka katika
kuhakikisha unafikia mafanikio pasipo kizuizi kikubwa sana.
Kila
wakati jenga utaratibu wa kujikumbusha na kuangalia jinsi unavyoishi, je, kwa
mwendo huo unaoishi, utakupa mafanikio au hautakupa mafanikio zaidi ya kuweza
kukuangusha wewe mwenyewe?
Fanyia kazi hiki
ulichojifunza leo kwa kuhakikisha kwamba, unajikumbusha yale maisha unayoishi
au matendo unayoyafanya kama matendo hayo yanakusaidia kukupeleka kwenye
mafanikio uyatakayo au yanakupeleka kwenye kushindwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.