Nov 30, 2018
Kama Unataka Kuwa Tajiri, Anza Kufanya Biashara Hizi Kwanza.
Katika
dunia ya sasa zipo biashara nyingi ambazo mtu anaweza akachagua mojawapo na kuifanya,
na kwa kuchagua huko biashara hiyo inaweza ikampa mtu huyo mafanikio
makubwa na hadi kuweza kufikia utajiri mkubwa.
Hata
hivyo pamoja na wingi huo wa biashara, kwa mujibu wa tafiti ambazo zimefanywa
hivi karibuni zinaonyesha zipo biashara ambazo ukizifanya zinaweza zikakufanya
ukawa tajiri kwa haraka sana au zikakurahisishia njia ya wewe kwenda kwenye
ubilionea wako.
Biashara
hizi si mpya sana masikioni mwako unazijua, hapa nakukumbusha ili uweze kuzingatia
kwa jicho la tofauti na pia kuzifanya kwa namna ya tofauti. Kwa kufanya biashara
hizo kwa utofauti, utakuwa umemudu kuweza kupiga hatua ya kufikia mafanikio
yako.
Biashara
hizo ni zipi? Zifuatazo ni aina za biashara ambazo ukizifanya zitakupa mafanikio
makubwa na yenye tija kwenye maisha yako.
1.
Usafiri.
Moja
ya biashara ambayo inaaminika hasa kwa bara la afrika ikiwa utaifanya kwa
utulivu na ukafata misingi yake ni biashara ya usafiri. Hapa unaweza ukawa na
kampuni yako ya kusafirishia abiria kutoka sehemu moja na kwenda nyingine.
Kwa
sasa hitaji la usafiri bado ni kubwa, kama si mjini hata kijijini. Watu wanataka
kusafiri kila siku na kwa bahati mbaya wengi hawana uwezo huo wa kumiliki
vyombo vya usafiri. Hii ni mojawapo ya biashara ya kuifikiria kuifanya kama
unaweza, kwani itakupa mafanikio sana.
2.
Afya.
Kama
pia utajikita na kufanya biashara inayohususha mambo ya afya, basi upo
uwezekano mkubwa zaidi wa wewe kufanikiwa sana. Huduma za afya katika maeneo
mengi bado hazijafikiwa kisawasawa na zinahitajika kweli.
Hivyo
kwa kufanya biashara hii, kama ukifungua hospitali au zahati au duka la dawa, utapata
pesa na hapo pia utakuwa imeisaidia jamii. Kikubwa kubali kuzunguka kuangalia
ni wapi ambapo ukifanya huduma au biashara hii wewe itakulipa.
3.
Chakula.
Hakuna
mtu asiyekula, hiyo ikiwa na maana ukianzisha biashara ya vyakula na ukaifanya
kwa ufanisi mkubwa utafanikiwa. Hapa unaweza ukauza chakula, lakini si maanishi
uje na picha ile ya mama ntilie ‘pasee.’
Ukiamua
kuja na biashara ya kuuza chakula ifanye kwa ukisasa zaidi. Zipo sehemu bado nyingi
zinazohitaji huduma hii ya chakula safi, mazingira safi, lakini hawaipati kwa
uhakika kwahiyo unatakiwa ujue jinsi ya kuanza ili uanze kupiga pesa.
4. Viwanda
vidogo vidogo.
Huwezi
kuendelelea sana kama utaendelea kuwa mlanguzi
wa biashara za watu wengine. Changamsha akili na anza mchakato wa kuweka viwanda
vidogo vidogo ambavyo vitasaidia wewe kuweza kukupa kipato kikubwa.
Uzuri
wakuwa na kiwanda kidogo wewe ndio unakuwa mzalishaji wa kwanza kwa hiyo ni
lazima utapata faida kubwa sana. Hapa unaweza ukatengeneza kiwanda chako cha
kutengeneza juisi au unga wa sembe na lishe, uamuzi ni wako.
Kwa
kuhitimisha, hizi ni baadhi ya biashara chache tu, ambazo unaweza ukazifanya na
zikakupa mafanikio makubwa. Uamuzi ni wako uanze na biashara ipi.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 29, 2018
Kanuni Za Kujua Kusudio La Kuumbwa Kwako.
Kila
mwanadamu ameumbwa na kusudio lake hapa dunia. Pia itakuwa ni dhambi kubwa kama
upo hapa dunia pasipo kutambua hilo
kusudio lako. Watu wengi wanashindwa kufanya vizuri katika yale wayafanyayo hii
ni kwa sababu watu hao wanafanya vitu ambavyo sio vyao bali ni vya watu wengine.
Watu
wengi tunaishi kwa kuigaiga mambo ya watu wengine, yaani utakuta mtu fulani
anafanya jambo fulani kisha mtu mwingine naye anaanza kufanya jambo hilo ,
kitendo hiki ni kujipoteza wewe mwenyewe pasipo wewe kujua.
Hivyo zifuatazo ndizo kanuni za kujua
kusudio la kuumbwa kwako;-
1. Muombe mwenyezi Mungu.
Kwa
imani uliyonayo basi unashauriwa kutumia imani hiyo hiyo kuomba Mungu akujalie
ili uweze kufahamu kusudio lako uwepo wako katika sayari hii. Kwani ukweli ni
kwamba Mungu wetu ni mwema na ni muaminifu pia, hivyo tunaamini anatambua kila
mmoja wetu lengo lake ni nini hapa duniani.
2. Hakikisha unafanya kitu ambacho
unakipenda.
Miongoni
mwa mambo ambayo humsaidia mtu ili aweze kujua lengo lake na kuwepo hapa
duniani ni pamoja na kufanya mambo ambayo anayapenda.
Wengi
wetu tunashindwa kufanikiwa katika maisha hii ni kwa sababu tunafanya vitu
tusivyovipenda. Hivyo kila wakati unatakiwa kuhahakisha kila unachokifanya
unakipenda kutoka moyoni mwako.
Kama
unafanya jambo ambao hulipendi unashauri uachane na jambo hilo mara moja kwani
ni sawa na kupoteza muda tu, kwani unatakuwa unafanya ilimradi siku iendee tu.
3. Jitafute/wewe ni nani?
Unashauriwa
pia ili uweze kutambua uwezo ulionao ni pamoja na kuwekeza muda mwingi wa
kujitafuta wewe ni nani. Ninapozungumzia wewe ni nani hapa ni maana ya kwamba
ni lazima uwaze kuwa wewe upo vizuri katika kufanya jambo gani?
Mara
baada ya kupata majibu ya kwamba wewe upo vizuri katika jambo gani ndipo
unapotakiwa kuwekeza nguvu, muda, akili na pesa katika kulikeleza jambo hilo.
Kama
wewe ni mwanamitindo, mfanyabiashara, fundi au jambo lolote lile basi ni vyema
ukaweka mkazo wa kiutendaji katika mambo hayo na si vinginevyo.
Pia
ni ili uweze kujitambua wewe ni nani zinahitajika akili za ziada za kuweza
kujitambua madhaifu na uwezo ulionao katika utendaji wa jambo fulani.
Katika
madhaifu uliyonayo basi yafanyie kazi madhaifu hiyo ili weze kuondokana nayo
kabisa, ila katika uwezo ulionao basi unatakiwa kuongeza juhudi ili uweze
kufanya bora zaidi ya uwezo wako.
Hayo
ni baadhi ya ya mambo ya msingi unayopaswa kuzingatia katika kutambua kusudio
lako hapa dunia ili uweze kuishi maisha yenye furaha hatimaye kupata mafanikio
unayoyataraji.
Ndimi Afisa mipango: Benson Chonya.
bensonchonya23.gmail.com
Nov 28, 2018
Usiruhusu Sauti Hii Ikakufanya Ukashindwa Kufanikiwa.
Ni rahisi
sana kwenye maisha yako kusikia hasa pale tunapofatilia ndoto zako mtu
akakwambia kwa uwazi kabisa kwamba ndoto na mipango yako hiyo huwezi kutimiza
labda tafuta kitu kingine cha kufanya.
Wengi
tumesikia sauti hizi sana na tumekuwa makini nazo na hata kulaani wale wte
waliotuambia kwamba hatuwezi kufanya hivyo. Lakini je, ukijiuliza hizo ndizo
sauti unazotakiwa kuwa makini nazo sana tu peke yake.
Ni kweli
sauti hizo zina madhara kwetu, ingawa mbali na sauti za nje ambazo zinakwambia
huwezi hili au lile lakini kiukweli ndani yako unayo sauti ambayo mara nyingi
ni chanzo kikubwa cha wewe kushindwa kwa chochote kile.
Sina
shaka yoyote na wewe, najua umeshawahi kujiambia kwa kujiamini kwamba naweza
kufanya jambo hili na nitalifanikisha, wengi hujiambia sana hivi hasa linapokuja
swala la kuelekea kwenye kutimiza ndoto zao muhimu.
Hata
hivyo pamoja na kujiambia hivi huku wakiwa na uhakika kwamba watakwenda kufanya
vile walivyojiambia na kwamba inawezekana, lakini ndani mwao utashangaa inajitokeza
sauti inayokwambia huwezi.
Sauti
hii karibu kila mtu inampata. Sauti hii kwa wengi imewaambia sana hawawezi hata
kwa yale mambo ambayo walikuwa wanaweza. Inatokea sana hata kama umejiaminisha
unaweza, lakini sauti hiyo inakusisitizia huwezi.
Kikawaida
sauti hii mara nyingi ipo sana ndani mwako. Unachotakiwa kufanya ili kuishinda
sauti hii ni kujiambia naweza nyingi sana hadi uweze kufanikiwa. Lakini ikiwa
utairuhusu sauti hii uwe na uhakika itakukwamisha na hutaweza kufika popote.
Sauti
hii wewe unayo na mwingine yoyote anayo ila kikubwa unachotakiwa kufanya ni
kujenga ule uwezo wa kupambana nayo hadi uishinde. Hebu angalia ndoto zako
umekuwa unazo nzuri kweli, lakini ukitaka kufanya kuna kitu kinakwambia huwezi.
Naamini
umeshawahi kukutana na kitu kama hiki sana na umekuwa hujui uchukue hatua gani.
Kwa vyovyote vile sauti hiyo inapotokea kwako ni lazima ujifunze kusema naweza
hata kama inakwambia huwezi vipi.
Ikiwa
hautaweza kuushinda sauti hii ni kweli usishangae hata yale malengo yako ambayo
ulikuwa ukiaamini kabisa kwamba utaweza kutimiza unaona nayo hayatimii kwa
sababu ya kuambiwa huwezi.
Kwa jinsi
unavyoisikia sauti hiyo ndani inayokwambia huwezi, inatakiwa uwe mwepesi sana
kusema naweza. Usije ukaambiwa huwezi na sauti inayotoka ndani mwako halafu ukabaki kimya, hapo ndipo utakuwa
unajipoteza.
Unatakiwa
kujenga maisha yako kwa kujimini sana kwa kijiambia unaweza mara nyingi
uwezavyo. Lakini usiishie kusema unaweza tu kwa mdomo huku hakikisha uwe
unachukua hatua pia.
Kwa kuchukua
hatua huku ukisema unaweza hakika amini utaweza kutimiza ile mipango
uliojiwekea. Badilisha mwelekeo wa maisha yako kwa kuiushinda sauti inayokuja
ndani yako ya kusema siwezi na kuwa naweza, hapo utafanikiwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 27, 2018
Kipato Kikubwa Kinatengenezwa Kwa Kufuata Hatua Hizi.
Katika nyakati za sasa, wakati ambapo dunia inakwenda kwa kasi na hali ya uchumi ikibadilika sana, ipo haja ya kila mtu kuweza kujifunza namna ya kuweza kutengeneza kipato kikubwa na cha kudumu.
Hiyo iko hivyo kwa sababu, bila kufanya hivyo,
utaachwa nyuma sana kimafanikio na utajikuta ukiwa ni mtu wa pale pale, miaka
na miaka. Una anzaje kujitengenezea kipato kikubwa wakati pengine mtaji wako ni
mdogo?
1. Anza na kidogo.
Katika harakati za kutengeneza kipato cha
kikubwa na cha kudumu ni vyema ukajifunza kuanza na kidogo. Anzia pale ulipo
ili kutafuta mafanikio yako. Chochote ambacho unaona kinakufaa kifanye, hata
bila kuona haya.
Watu waliofanikiwa si kwamba walianza na mambo
makubwa sana, hapana. Mara nyingi ni watu waliomua kukubali kukaa chini na
kuanza na kidogo kile walichonacho ili kufikia mafanikio yao.
Ni jukumu hilo hilo ambalo unaweza hata wewe
ukalichukua na kuanza na kidogo ulichonacho. Acha kusubiri sana mpaka kila kitu
kikamilike ndio uanze kufanya. Ukifanya hivyo, yaani kuendelea kusubiri utakuwa
unajichelewesha mwenyewe kufanikiwa.
2. Jenga fikra chanya.
Hautaweza kutengeneza kipato kikubwa na
kufanikiwa kama kila wakati fikra zako zipo hasi, hasa linapokuja suala
linalohusiana na mambo ya fedha. Ni lazima fikra zako ziwe chanya na kuamini
kwamba una uwezo wa kutengeneza pesa.
Acha kuendelea kung’ang’ania fikra mgando
ambazo hata hazikusadii kitu, zaidi zinakukwamisha sana kufanikiwa. Watu
waliofanikiwa kipesa na kutengeneza pesa nyingi, kila wakati huamini sana wao
ni watu wa pesa.
Kwa kuamini kila siku na kuendelea kufanyia
kazi yale wanayoyafanya bila kuchoka hujikuta wakiwa na pesa nyingi sana katika
maisha yao. Kama leo hii unataka kutengeneza kipato kikubwa, jenga fikra chanya
juu ya pesa na utafanikiwa.
3. Weka mipango imara.
Silaha pekee ya kuweza kufanikisha kujenga
kipato kikubwa na cha uhakika ni kwa wewe kuhakikisha unakuwa na mipango ya
kutengeneza kipato hicho. Ni muhimu sana kujiwekea mipango imara ili ikusaidie
kutimiza lengo lako.
Kwa mfano, unaweza ukaweka mipango ya kuwekeza
vitega uchumi vya aina tofauti tofauti ambavyo vitakusaidia katika kutengeneza
kipato kikubwa. Ukishaweka mipango hiyo unaiweka kwenye utekelezaji.
Watu wenye mafanikio makubwa ndvyo ambavyo
hujiwekea mipango yao kwa staili hiyo karibu kila siku. Lakini hawaishii kuweka
mipango hiyo bali huchukua jukumu la kuifatilia kial siku. Hicho ndicho kitu
unachotakiwa kukifanya ili ufanikiwe pia.
4. Kuwa mvumilivu.
Kila mafanikio yanahitaji uvumulivu wa aina
fulani ili uweze kuyapata. Hakuna mafaniko ambayo unaweza eti ukayapata bila
kuvumilia. Kipo kipindi ambacho kwa vyovyote vile ni lazima usibiri.
Hivyo wakati umejiwekea mipango na mikakati
yako ya kukuwezesha kufanikiwa, tambua unatakiwa kuwa mpole kwa kukaa chini na
kusubiri mchakato wa mafanikio yako kuwezekana.
Kila mtu aliye na mafanikio leo hii ukimuuliza
ni lazima atakwamba alivumilia kwa namna fulani hivi na hakuyapata mafanikio
hayo mara moja. Ili nawe uweze kujenga kipato kikubwa unahitaji uvumilivu wa kutosha.
Jipe muda wa kuvumilia.
Kitu unachotakiwa ukijue mapema ili uweze
kutengeneza kipato kikubwa ni kwamba, kipato hicho huwa hakitengenezwi kwa
bahati mbaya. Mara nyingi huwa ipo misingi au hatua unazotakiwa uzifuate
kama ambavyo tulivyojadili kujadili.
Kumbuka zaidi ili uweze kutengeneza kipato
kikubwa, unahitaji kuanza na kidogo, kujenga fikra chanya juu ya pesa, kuweka
mipango imara na wewe kuwa mvumilivu. Ukiweza kuzingata mambo hayo. Hilo halina
shaka, tayari utakuwa na uhakika wa kutengeneza kipato kikubwa.
Endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Nov 24, 2018
Kwa Nini Hutakiwi Kuonyesha Udhaifu Wako Kwa Wengine?
Kila mmoja wetu ana udhaifu wa aina fulani. Kwa mfano, kuna wengine wana hasira, kuna wengine wana huruma, na kuna wengine hawawezi kuficha siri. Kila mmoja ukiangalia ana udhaifu wa aina fulani, hata wewe upo udhaifu ambao unao.
Pamoja
na kila mtu ana udhaiafu wake, lakini kitaalamu unashauriwa usijaribu kuuweka
udhaifu wako huo kwa watu wengine kwa sababu, ipo siku watu hao watakaojua udhaifu
wako watautumia udhaifu huo huo kuumiza wewe.
Hata
ikitokea mtu huyu ni wa karibu sana, usimwambie udhaifu wako wewe kaa nao. Ndio
maana hata kwenye biashara wengine wanashinda na kufanikiwa kwa sababu ya kujua
udhaifu wa upande wa pili uko wapi na kuufanyia kazi.
Si kwenye
biashara tu, hata kwenye vita, au kwenye mpira, wale wanaojua udhaifu wa
wengine vizuri hao ndio wanaoshinda. Kwa hiyo kuweka udhaifu wako nje ni sawa
na kuanza kujitangazia kwamba ni lazima utashindwa katika eneo fulani la maisha
yako.
Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.
Mfano mzuri wa kuweka udhaifu wako nje, tunauona kwenye maandiko matakatifu kwenye hadithi ya Samsoni na Delila. Unaona Samsoni aliweza kukamatwa na kuteswa na adui zake mara baada ya kusema udhaifu wake kwa mkewe.
Katika mfano huo, ingawa wengi tunajua lakini unaonyesha Samsoni siri ya nguvu zake nyingi ambazo alitumia kuulia Simba na kupiga maadui zake zilikuwa kwenye nywele. Alikuwa hatakiwi kukata nywele kwa namna yoyote ile na hiyo ilikuwa ni siri kwake ambayo hakutakiwa kusema kwa mtu.
Lakini
alipoulizwa na kubembelezwa sana ataje siri ya nguvu zake na mkewe, mwisho
akajikuta akiisema, aliamua kuweka udhaifu wake nje, na matokeo yake wakati
amelala aliweza kukatwa nywele na kukosa nguvu hizo alizokuwa nazo na matokeo
mabaya yalimkuta kwa sababu ya kuonyesha udhaifu wake nje.
Unatakiwa
kujua ni kitu kibaya na hatari kwako ni kujaribu kuuweka udhaifu wako nje na
kila mtu auone. Huko ni kujitakia hatari kubwa sana ambayo inaweza kukupoteza
wewe. Kama una udhaifu wa aina fulani kaa kimya, sio lazima useme.
Kikubwa
kwako na kitu cha kufanya ni kuufanyia kazi udhaifu wako na kuhakikisha unakuwa
bora. Lakini usijaribu kuweka udhaifu wako nje hata kwa rafiki, watoto au mtu
wa karibu unayemwamini kama mkeo. Ni kosa kubwa kama kweli ukiamua kuanika
udhaifu wako.
Amini usiamini ipo siku utaumizwa tu kwa wewe kuuweka udhaifu wako nje kama utafanya hivyo. Kwa hiyo dawa pekee ya kuweza kukwepa kuumizwa huko ni kukaa kimya na udhaifu wako na si kusema kwa kila mtu.
Achana
na tabia ile ya watu utakuta anasema aah, mimi nina hasira ujue. Watu ipo siku
watatumia hasira hizo hizo kukufanyia kitu ambacho wewe hujaamini. Kitu cha
msingi hapa ni kuhakikisha unafunga mdomo wako na kuweka moyoni mwako udhaifu
wako.
Neno la
mwisho kwangu nikukumbushe, usijaribu hata siku moja kuonyesha udhaifu wako kwa
wengine, watu hao watatumia udhaifu huo kama fursa ya kuweza kukuumiza wewe. Tafakari
hili na utagundua ukweli hasa wa hiki nikisemacho.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 23, 2018
Mbinu Za Kujitofautisha Kibiashara Hatimaye kupata Faida.
Babu yangu aliwahi kunisihi ya kwamba kufanya biashara na hatimaye kufanikiwa katika biashara hiyo kunahitaji juhudi za maksudi kutoka kwa mfanyabishara husika. Hii ni kwa sababu kufanya biashara ni kumsubiri mteja ambaye huna imani ya kwamba atakuja ama la.
Pia ulimwengu wa sasa kila kitu kinachonekana kwa macho
kimekuwa ni biashara na biashara hizi asilimia 99.9 ni biashara ambazo
zinafanana, hivyo ili uweze kuona unafanikiwa katika biashara hiyo ni lazima
uwaze juu ya kujitofautisha kibiashara hatimaye upate faida.
Swali linaweza kuja ni je najitofautishaje kibiashara? Wala
usipate tabu nipo hapa kwa ajili ya kukata kiu ya maswali yako kama ifutavyo:-
Ili uweze kuwa ni mtu wa tofauti katika biashara unayoifanya
unatakiwa kuhakikisha unajikita zaidi katika kuhakikisha unatangaza biashara
yako kwa kiwango cha hali ya juu na ya kipekee, kwani ukweli ulio bayana na
usiopingwa ni kwamba biashara nzuri na yenye kuleta faida kubwa chanzo chake ni
matangazo.
Jambo jingine linakalokusaidia kuwa ni mtu wa kitofauti katika
biashara yako ni kuhakikisha ya kwamba unaboresha zaidi katika kitengo cha
huduma kwa wateja. Mfanye mteja wako asikuchoke yaani kuanzia anapokuja mpaka
anapoondoka, awe ni mtu ambaye anajisikia furaha na amani muda wote na hii yote
itatokana na vile ambavyo utakavyompokea na kumuhudumia.
Pia jifunze kuweka mazingira ya ofisi yako katika muonekana
nadhifu na wenye kuvutia kila mteja anayepita au anayekuja, hii ni kuanzia
mapambo yako, upangaji wa vitu vyako vya kuuza na vile visivyo vya kuuza pia.
Mwisho kabisa kila wakati unatakiwa kukumbuka hakuna mteja
anayependa kucheleweshewa kupata huduma, hivyo jifunze kutoa huduma yako kwa
haraka na kwa wakati muafaka.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, kazi ibaki kuwa kwako katika
utekelezaji wa hayo niliyoyaeleza. Nikutakie siku njema na mafanikio ,ema, na
Mwenyezi Mungu akawe pamoja nawe katika utekelezaji wa majukumu Yako.
Ndimi Afisa Mipango
Benson Chonya.
0757-909942
Nov 21, 2018
Ongeza Umakini Sana Kwenye Maamuzi Haya Na Utafanikiwa.
Tafiti nyingi zinaonyesha binadamu anafanya maamuzi madogo madogo zaidi ya 300 kwa siku moja tu. Maamuzi anayoyafanya ikiwa ni pamoja na ale nini, avae nini, aende wapi, aongee na nani, aamke saa ngapi, afanye biashara gani, ni maamuzi madogo madogo lakini hadi yanafikia zaidi ya 300 kwa siku moja peke yake.
Inaweza
ikakushangaza kidogo, lakini ukweli ndio huo hapo kwamba kwa siku unafanya
maamuzi zaidi ya 300. Hivyo na kwa sababu hiyo, unatakiwa kujiuliza maamuzi
hayo unayofanya ingawa wakati mwingine unaweza usiyaelewe sana ni ya aina gani?
yanakusaidia au yanakuharibu? ni muhimu sana kujiuliza swali hilo.
Kwa
mfano, kama kila siku unafanya maamuzi ya kula vyakula vya hovyo kama vile
vyenye mafuta, kiafya unategemea nini? Au kama kila siku unafanya maamuzi yasiyo
ya msingi kwa kutumia pesa zako hovyo unategemea kweli itafika wakati utafikia
ule uhuru wa kifedha? Maamuzi mabovu
kama hayo ni rahisi tu kukudondosha.
Ukiangalia
tokea muda una amka asubuhi hapo ndipo maamuzi yako yanapoanzia, najua utaamua
uamke unafuraha au huzuni, au utaamua
siku hiyo ufanye kazi kwa bidii sana au kwa ulegevu. Yapo mambo mengi sana
ambayo utaamua lakini yote yana matokeo kwenye maisha yetu bila kujali matokeo
hayo ni hasi au chanya.
Tambua,
ikiwa asilimia 90 ya maamuzi haya madogo madogo unayoyafanya kila siku hayapo
sahihi, basi hakuna ubishi lazima ushindwe kwenye maisha. Pia ikiwa maamuzi
haya madogo madogo unayoyafanya yapo sahihi kwa asilimia 90, ujue unao uhakika
wa mafanikio kabisa na hakuna ubishi.
Kazi
kubwa inabaki kwako maamuzi unayoyafanya ni ya aina gani? Ndio maana unatakiwa
usikurupuke, kichwa chako kinatakiwa kutulia na kujua maamuzi unayoyafanya
yanakupoteza kwenye njia ya mafanikio au yanakuweka kwenye njia halisi ya
kufanikiwa kwako.
Kama
nilivyotangulia kusema, huwezi kuwa na maamuzi ya hovyo ukategemea kufanikiwa.
Mafanikio yako yanategemea sana na maamuzi yako ya kila siku. Kwa lugha
nyingine kipimo sahihi cha mafanikio yako ya kesho kinatokana na maamuzi yako
ya kila siku unayoyafanya.
Kama
kila siku ukiwa makini na maamuzi yako, ni rahisi sana kujua wewe kama kweli
utafanikiwa au hautafanikiwa. Ukiongeza umakini kidogo na kujua sawasawa
maamuzi unayoyachukua kila siku, basi utaelewa nisemacho hapo, juu ya umuhimu
wa kuyaangalia maamuzi yako kila siku.
Mwisho
kabisa elewa hivi, kila maamuzi unayoyafanya yana matokeo kwenye maisha yako, eidha
matokeo mazuri au mabaya, inategemea tu
ni maamuzi gani ambayo umeyafanya. Hivyo kila siku ongeza umakini kwenye
maamuzi yako na hakikisha unafanya
maamuzi sahihi ili ujenge maisha yako ya mafanikio kwa usahihi pia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 20, 2018
Sababu Tano (5) Kwa Nini Unaogopa Sana Kushindwa.
Kati ya kitu ambacho watu wengi sana wanakiogopa ni kule kushindwa. Ukiwauliza watu hao kwa nini wanaogopa sana kushindwa kwenye kile kitu wanachataka kufanya, sana sana watakwambia sababu moja tu kwamba wanaogopa kupata hasara.
Watu
hawa wanakuwa hawana sababu zingine makini za kwa nini wao wanaogopa kushindwa,
na hali ambayo inawasababishia wao hata washindwe kuchukua hatua. Suala la
kuogopa kushindwa lipo kwa watu wengi sana, na unaweza ukawa miongoni mwao.
Hebu
tuulizane mimi na wewe, au nikuulize je, unajua hasa kwa nini watu wanaogopa
sana kushindwa, iwe kuogopa kushindwa kwenye mradi, kwenye masomo, au kwenye usaili,
lakini woga huo upo tena kwa sehemu kubwa tu, naamini unalijua hilo.
Sina
shaka unafikiri na kujiuliza aisee ni kweli watu tunaogopa kushindwa na una
hamu ya kutaka kujua sababu zake ni zipi hasa zinazofanya watu waogope sana
kushindwa. Tulia hapo hapo, nikupe sababu yakinifu za kwa nini watu wengi wanaogopa kushindwa.
1. Ufinyu
wa mawazo.
Watu
wanaogopa kushindwa kwa sababu ya ufinyu wa mawazo au akili zao zinakuwa kama vile zimefikia ukomo. Kivipi? Mtu anakuwa
anaogopa kushindwa kwa kuamini kwamba akishindwa ndio hana nafasi tena ya kujaribu, kwa hiyo hawezi kufanikiwa
hata iweje.
Ukiwa
una mawazo haya yanayoamini nafasi pekee ya hicho ukifanyacho ni moja tu na
haitajirudia kwako tena, basi utaogopa sana kushindwa. Hutaweza kufanya
biashara kwa usahihi au chochote kwa sababu utaogopa kama ukishindwa ndio
umepoteza na kupotea.
Maisha
hayana nafasi moja kama unavyofikiri. Ukishindwa leo, kuna nafasi ya kujaribu
tena na tena mpaka utafanikiwa. Ukiondoa ufinyu wa mawazo au ‘limited mind’ ya kuamini kwamba
ukishindwa ndio basi, hutaogopa kushindwa tena, upo?
2. Kutaka
kuonekana sahihi wakati wote.
Leo kila
mtu akifikiria kufanya jambo anataka kuwa sahihi sana mbele ya watu. Anataka kufanya
jambo lake huku akiwa amekamilika kwa asilimia mia moja. Mtu huyu anasahau
kabisa kwamba hata wale anaowaona wamekamilika walianza wakiwa hawajakamilika.
Kwa mawazo
hayo ni lazima, piga ua garagaza, mtu huyu ataogopa kushindwa. Kila wakati
akitaka kufanya jambo anakuwa anajiuliza je, nikishindwa itakuwaje, si nitachekwa
na watu na nitaonekana sifai.
Kwa hiyo
hapa na kwa kifupi, kinachowapoteza watu wengi na kuogopa kushindwa ni kwa sababu
ya kutaka kuanza kwa ukamili, ukiwa sawa kila kitu. Kwa sababu hiyo kuogopa
kushindwa huwezi kukwepa hata iweje, umeidaka hiyo?
3.
Athari mbaya tulizofundishwa shuleni.
Tokea
tukiwa shule au tukiwa wadogo tumefundishwa na kukaririshwa na kwa bahati mbaya
na sisi tukameza kama kasuku na kujua kwamba kushindwa ni kitu kibaya. Hakuna ambaye
kafundishwa kushindwa ni kitu kizuri.
Ili kukuhakikishia
kushindwa ni kitu kibaya, tena tukawekewa na viboko, ukizingua tu kwa kushindwa unacharazwa bakora zako ili
kesho usishindwe. Kwa hiyo kila wakati ulikuwa ukiwaza mmh nikishindwa tu,
kimenuka.
Sasa
nikuulize, je, uliyepitia mazingira kama haya utakwepa kuogopa kushindwa? Hapa ni
lazima utaogopa kushindwa tu na utakuwa unaona kushindwa ni kosa kubwa sana. Hivyo
utafanya kila linawezekana usishindwe, kumbe ndio umepotea, umeiona hiyo?
4.
Kuhofia kuchekwa.
Eti unaogopa
kushindwa kwa sababu ya kuogopa kuchekwa, unasema daah, hivi nikishindwa watu
watasema nini, si watanicheka sana na itakuwaje. Kwa sababu hii tu, aloo,
lazima uogope kushindwa na hutaweza kuchukua hatua.
Unajua
kila mtu anataka kuonekana simba, anataka kuonekana anafanikiwa kwenye jamii,
sasa kwa mawazo hayo mtu anataka mambo yake yaonekane yamewaka hakuna kushindwa,
hapo ndipo hofu inapoanza kuzalishwa sasa.
Kwa mtu
mwenye mawazo kama hayo ya kuogopa kuchekwa, wee, utamwambia nini, badala ya
kuweka nguvu zake kwenye kuchukua hatua, yeye anakomaa na kuogopa kushindwa kwa
kile anachotaka kukifanya, hatari hiyo umeisoma eeh?
5.
Kutokujiamini.
Sababu
nyingine ya kiufundi ya kuogopa kwetu
kushindwa ni kwa sababu hatujiamini. Hauamini kwamba eti unaweza ukatoka kwenye
kushindwa hadi kufanikiwa. Haumini kama ndani yako unao uwezo mkubwa wa
kukusaidia kufanikiwa.
Kama
hujiamini kuogopa kushindwa kunakuhusu sana tu na tena sana. Kama huamini uwezo
wako, basi hiyo kwako itakuwa ni sababu ya msingi sana itakayokufanya uogope sana
kushindwa kwa chochote kile, unachotaka kukifanya.
Kwa kujifunza
sababu hizi zinakufanya uogope kushindwa naamini zimekuondolea hofu kwa kiasi,
lakini elewa hivi, huwezi kufanikiwa pasipo kushindwa, kwani kushindwa ni sehemu ya
mafanikio. Hivyo usiogope sana kushindwa, bali kushindwa huko kufanye kuwa
ngazi ya mafanikio yako. Na piga marufuku kuogopa kushindwa maishani mwako
kabisa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 18, 2018
Mambo Kumi Utakayofaidika Nayo Kupitia Kujifunza Kila Siku …
Watu wanao anguka sana kwenye maisha na hawafiki mbali ni wale watu ambao hawajifunzi iwe kwa kusoma vitabu au kujifunza kwa wengine. Ipo faida kubwa sana ya kujifunza ambayo wengi hawaijui na kuchukulia mambo kwa kawaida tu.
Labda
nikwambie hivi, ikiwa husomi vitabu ni kweli unaweza ukafanikiwa, lakini
hutaweza kufikia mafanikio yale ya juu sana. Utaishia tu kwenye haya mafanikio
ya kawaida. Sasa je, faida za kusoma vitabu ni zipi?
Hapa
kwenye makala haya nimekuwekea faida kumi na kwa kifupi tu ambazo unaweza
ukazipitia na kuchukua hatua.
1.
Ukisoma vitabu, utakuwa unakua kila siku kimafanikio angalau kwa asilimia moja
tu, kuliko ambavyo ungekaa bila
kujifunza kupitia vitabu.
2.
Ukiamua kusoma vitabu, itakusaidia kuvunja baadhi ya tabia zako mbaya na
zinakupeleka wewe ushindwe, na kutengeneza tabia zaidi za kimafanikio.
3.
Vitabu vinakuepusha na kukwepa kufanya makosa , ambayo watu wengi wanayafanya
karibu kila siku kwenye safari zao za mafanikio.
4.
Kupitia kusoma vitabu, vinakupa hamasa na nguvu ya kusonga mbele zaidi hata
pale ambapo kuna wakati unajiona unakosa hamasa, vitabu vinakupa nguvu hiyo.
5.
Pia faida nyingine ya vitabu, vinakupa uwezo zaidi wa wewe kuweza kujiamini na
kuona kwamba kumbe unaweza kufanya kitu kwenye maisha yako .
6.
Vitabu vinasaidia kukutengenezea mfumo mpya wa maisha na ambao hata hukuwa nao,
yaani unakuwa unajishangaa unakuwa mpya kila siku iitwapo leo.
7.
Kujisomea vitabu pia inasaidia wewe kuweza kutengeneza mazingira ya wazi ambayo
yatakusaidia sana kuweza kufanikiwa tofauti na ambavyo kama hujisomei kabisa.
8.
Vitabu vinakusaidia wewe kuweza kufanya mabadiliko madogo madogo na kila siku,
ambapo mwisho wa siku unashangaa unafika mbali sana kimafanikio.
9. Vitabu
vinakupa msukumo wa kurudi kwenye njia kuu hasa pale unapokuwa umetoka kwenye
njia kuu hii ni mojawapo ya faida kubwa sana kuijua.
10.
Na muhimu zaidi, vitabu vinakufanya wewe unakuwa mtu wa kuchukua hatua zaidi
kila siku. Kama ulikiwa unashindwa kuchukua hatua vitabu vinakusukuma kufanya
hivyo.
Kwa
uchache hizi ni faida ambazo wewe utakazopata kupitia kujisomea, unasubiri nini
tena? Washa moto zaidi wa kujisomea.…
.
.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa
vifaranga wa kuku aina ya KUROILER,
SASSO, KIENYEJI ASILIA na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao
kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na
wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 17, 2018
Kila Wakati Zitumie Kanuni Hizi Muhimu Kwa Ajili Ya Mafanikio Yako.
Leo nitaomba
nichukue walau dakika chache ili niweze kukumbusha kanuni sita za kukupa
mafanikio unayoyahitaji. Hizi ni kanuni ambazo ukizitumia na kuzifanyia kazi ni
lazima zikupe matokeo makubwa kwa ajili ya mafanikio yako.
Wengi wanaozitumia
kanuni hizo zinawasaidia sana kupiga hatua na kuwafanikisha. Kila wakati jaribu
kuzitumia kanuni hizi kwa ajili ya manufaa yako na ya wengine pia. Usitoke hapo
ulipo twende pamoja katika somo letu la leo tujifunze kanuni hizi;-
1. Kanuni ya 1; Chukua hatua
stahiki.
Miongoni
mwa vitu vitakuvyofanya uzidi kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa ni pamoja na
kuendelea kuchukua hatua stahiki kwa hicho unachokifanya au kile unachotaka
kufanya. Kushindwa kuchukua hatua huko ni kuchagua kujiangusha wewe mwenyewe.
2. Kanuni ya 2;Tumia siku yako
vizuri na kwa uhakika.
Mafanikio
siku zote ni matokeo ya vile unavyoitumia siku yako vyema, hivyo ulivyo leo ni
matokeo ya hatua ulizozichukua siku ya jana. Hivyo jifunze kuitumia leo yako
vyema ili uishe kesho yako yenye mafanikio na furaha tele.
3. Kanuni ya 3; Jenga mtazamo sahihi
kila wakati.
Hivyo
ulivyo leo katika suala la mafanikio ni matokeo ya mawazo yako. Kama mawazo
yako ni hasi basi hata maisha yake yatakuwa vivyo hivyo. Kama unataka unataka
kubadili maisha yako, basi badili na mawazo yako na kuwa chanya.
4. Kanuni ya 4; Tafuta njia ya
mafanikio yako.
Kama
tutaamua kutafuta mafanikio ya kweli ni lazima tutafuta njia ya kuyapata
mafanikio hayo, ila kama hatuhitaji mafanikio ni lazima tutafuta visingizio.
Hivyo ili tuweze kufika katika kilele cha mafanikio tunatakiwa kutafuta njia ya
kupata mafanikio hayo.
5. Kanuni ya 5; Jenga uwezo wa kutatua
changamoto;
Katika
maisha haya kila kitu kinawezekana, kama kuna jambo unaliona ni changamoto na
haliwezekani basi mahala hapo ndipo palipo na fursa lukuki zilizojificha, hivyo
jifinze kushughulika na kila changamoto zilipo katika jamii yako kwani hapo
ndipo palipo na fursa.
6. Kanuni ya 6; Toa hofu zako.
Siraha
hatari zaidi duniani si bunduki wala mabomu ya nyuklia kama wengi wadhanivyo,
bali siraha hatari zaidi duniani ni hofu. Hofu ndio chanzo kikubwa cha kuua
ndoto za walio wengi, wengi wetu tunashindwa kuthubutu kufanya jambo fulani eti
kwa sababu ya kwamba tunaogopa kitu fulani.
Hivyo
kama kweli unataka kupiga hatua za kusonga mbele tunatakiwa kuhakikisha ya
kwamba tunaondokana na hofu, kwani hofu ni adui nambari moja wa mafanikio.
Asante
sana kwa kusoma makala haya kupitia mtandao huu wa Dira Ya Mafanikio, nikutakie
siku njema na mafanikio mema.
Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)