Sep 26, 2017
Nguvu Ya Mtazamo Katika Kushindwa Au Kufanikiwa Kwako.
Mtazamo una nguvu ya
kubadili hali mbaya inayoonekana na kuwa hali nzuri kabisa. Nguvu yote hiyo ya
kubadili hayo inatoka kwenye mtazamo alionao mtu huyo.
Mtazamo unafanya maisha
kuonekana ya maana, hata pale ambapo wengi wanaona maisha hayana maana tena na
yanachosha.
Mtazamo una nguvu kubwa sana
ya kulainisha kile kinachoitwa kigumu na kuonekana kirahisi, hiyo yote ni kazi
ya mtazamo.
Unapokuwa upo kati kati ya
matatizo, hakuna kitu kingine kinachoweza kukuokoa na kutoka hapo na kuwa na
amani zaidi ya kubadilisha mtazamo wako.
Unapobadili mtazamo, hata kama tatizo lako lilikuwa kubwa sana, tatizo
hilo unaona linaanza kulainika na linakuwa linawezekana kutatuliwa.
Wengi wanaoshindwa katika
maisha na kuamua kukata tamaa kabisa ni watu ambao mara nyingi wameshindwa
kutawala mitazamo yao.
Kiuhalisia unaposhindwa kutawala
mtazamo wako na ukajikuta una mtazamo hasi, elewa kabisa maisha yako yatakuwa
magumu sana katika kila eneo.
Kwa hiyo unaona kabisa
mtazamo una nguvu kubwa sana ya kubadili maisha yako, inategemea tu wewe
unautumiaje huo mtazamo wako ulionao.
Ndio kila wakati unashauriwa
kukaa na watu chanya, watu ambao wataweza kukusaidia kukujengea mtazamo mzuri
wa kufanikiwa.
Kwa hiyo kuanzia sasa
hutakiwi kushangaa, unapoona wengine wanafanikiwa na wengine wanashindwa hilo
ni swala la mtazamo.
Kwa mfano, utakuta ni watu
wanaokaa katika mji mmoja au nchi moja lakini wengine wamefanikiwa na wengine
wameshindwa, hapo hakuna kingine zaidi ya mtazamo.
Anguko kubwa la watu
linaanza na mitazamo yao. Kwa jinsi unavyokuwa na mtazamo mbovu ndivyo maisha
yako yanazidi kuwa mabovu pia.
Lakini mtazamo mzuri una
siri kubwa ya kugeuza chochote kuwa mafanikio. Mtazamo mzuri unaweza kugeuza
hata maji kuwa almasi.
Mtu mwenye mtazamo mbovu
mara nyingi hata apewe fursa nzuri vipi sio rahisi kufanikiwa, kinachomwangusha
ni mtazamo wake tu.
Hiyo yote inaonyesha
kushindwa kwa wengi kunasabbishwa na mtazamo wake sana, na hapo ndipo ulazima
kwa kubadilisha mtazamo unahitajika kwa nguvu zote.
Leo kama unataka kufanikiwa,
hebu anza kubadili mtazamo wako ili ukusaidie kwani una uwezo wa kubadili chochote
na kuwa kizuri.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.