Jun 30, 2020
Kama Utazingatia Mambo Haya Mawili, Umefanikiwa.
Kama unataka kujenga maisha yako ya mafanikio, na ukajikuta mbali sana, unaweza ukazingatia sana mambo haya mawili tu. Haya ni mambo ambayo yamewasaidia sana wengi kufanikiwa;-
#1. Linda kazi yako ya siku na anzisha biashara ya muda.
Kama umeajiriwa anza na kulinda kazi yako kwanza, na kama umejiajiri, chunga sana kipato chako, hiyo inakusaidia sana, kujifunza biashara, na kuchukua uzoefu mkubwa wa biashara. Pia inakusaidia kuchukua umiliki wa maisha yako ya baadae, ya kwamba utakuwa wapi mara baada ya muda fulani.
Kwa kadri unavyokuwa kwenye ajira au biashara yako na huku unafanya biashara nyingine ya pembeni itakusaidia sana kujifunza mengi ambayo usingeweza kujifunza kama usingeanza kabisa biashara hiyo.
#2. Wekeza katika nyumba.
Ukiwekeza katika nyumba, ama "real estate" ni rahisi kwa benki kukupa mkopo na ukasonga mbele sana kimafanikio. Hivyo kazana kujenga nyumba hata kama ni ndogo ndogo tu, kwa ajili ya mikopo.
Wawekezaji wengi, wanafanikiwa kwa sababu ya kutumia mikopo ya nyumba. Unasubiri nini, anza kuwekeza kidogo kidogo kwenye nyumba ili ikusaidie kuchukulia mkopo, ila hakikisha isiwe nyumba yako ya kuishi.
Kila la kheri,
Imani ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com
#1. Linda kazi yako ya siku na anzisha biashara ya muda.
Kama umeajiriwa anza na kulinda kazi yako kwanza, na kama umejiajiri, chunga sana kipato chako, hiyo inakusaidia sana, kujifunza biashara, na kuchukua uzoefu mkubwa wa biashara. Pia inakusaidia kuchukua umiliki wa maisha yako ya baadae, ya kwamba utakuwa wapi mara baada ya muda fulani.
Kwa kadri unavyokuwa kwenye ajira au biashara yako na huku unafanya biashara nyingine ya pembeni itakusaidia sana kujifunza mengi ambayo usingeweza kujifunza kama usingeanza kabisa biashara hiyo.
#2. Wekeza katika nyumba.
Ukiwekeza katika nyumba, ama "real estate" ni rahisi kwa benki kukupa mkopo na ukasonga mbele sana kimafanikio. Hivyo kazana kujenga nyumba hata kama ni ndogo ndogo tu, kwa ajili ya mikopo.
Wawekezaji wengi, wanafanikiwa kwa sababu ya kutumia mikopo ya nyumba. Unasubiri nini, anza kuwekeza kidogo kidogo kwenye nyumba ili ikusaidie kuchukulia mkopo, ila hakikisha isiwe nyumba yako ya kuishi.
Kila la kheri,
Imani ngwangwalu,
dirayamafanikio@gmail.com
Jun 29, 2020
Namna Sahihi Ya Kuendana Na Mabadiliko Ya Kidunia Kwenye Jambo Unalofanya.
Wakati
mwingine unapaswa kuelewa kwamba kile ambacho unakijua leo baada ya miaka
mitano ijayo kinaweza kisiwe na faida tena au kinaweza kisilete matokeo yale
ambayo mwenyewe unayapata kwa sasa. Nimesema hayo kwa sababu kwa hivi sasa
mambo yanabadilika sana.
Ile
dunia ya jana si dunia ya leo. Mambo kila kukiacha yanabadilika sana, watalamu
nao hawalali kutwa wanaumizwa vichwa vyao kuweza kugundua mbinu mpya ambazo ni
rahisi kwa mwanadamu kuweza kumrahisishia kazi mbalimbali.
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba dunia inakwenda kasi hivyo ili kuendana sawa na mabadiliko hayo ni
kwamba hata wewe unapaswa kubadilika pia. Na njia pekee ambayo itakayokusaidia
kwa namna moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kila eneo unalofanyia kazi
ni kwamba unatakiwa kujiimarisha wewe mwenyewe kila siku.
Na
njia pekee itakayokusaidia kuweza kujiimarisha ni kwamba unatakiwa kuhakikisha
kwamba unaenda na mabadiliko yanayotokea kila siku, ni kujifunza mambo mapya kila wakati kwa sababu
usipojifunza mambo mapya ni kwamba utapitwa na vingi.
Ni
muhimu kuelewa kwamba kwenye kila sekta unayoifanyika kazi unapaswa kujifunza
namna ambavyo utakuwa bora kila wakati. Kumbuka kujifunza hakuna mipaka hivyo ni
muhimu sana kwako kuweza kujifunza mambo mbalimbali yatakayokusaidia kwa namna
moja ama nyingine kuwa bora zaidi kwenye kile unachokifanya kila wakati kwani
pindi utakaposhindwa kufanya hivyo ni kwamba hata wewe utapitwa na utashindwa
kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidunia yanayotokea.
Kwa
muktadha huo, unapaswa kila wakati uwekeze muda mwingi kwenye kujifunza vitu
vipya kila siku. Kama wewe ni mkulima basi ni jifunze mbinu mpya kila siku zitakazokuwezesha
kufanikiwa zaidi katika kilimo hicho, kama wewe ni mtalamu wa jambo fulani basi
yakupasa kuweza kujipambanua zaidi kwa kujiwekeza kwenye kupata maarifa sahihi
juu ya jambo hilo.
Ni
muhimu kupata maarifa fulani kila wakati
kwa sababu kwa sasa dunia inakwenda kasi
sana hivyo bila kuwa na maarifa mapya ni kwamba utazidi kuwa mtu wazamani kila
siku , kwani kila kitu ambacho kitakuwa kinafanywa na watu wengine kwako
kitakuwa kigeni.
Mwisho
naomba nitamatishe kwa kusema ya kwamba kila wakati ongeza ubobezi kwenye kila
eneo unalofanyia kazi kwa sababu ubobezi humsaidia mtu kuweza kufanya jambo
lililo bora zaidi, pia kila wakati unapaswa kuelewa kwamba ubobezi hupatikana
kwa kuweza katika kujifunza vitu vipya kila siku ili uweze kuendana na
mabadiliko ya kidunia.
Ndimi: Afisa Mipango Benson
Chonya.
0757-909942
Jun 28, 2020
Hivi Ndivyo Unavyoweza Kunufaika Kwa Ufugaji Wa Samaki.
Habari yako ndugu msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO .
Leo nataka tujikite kujadili ufugaji wa samaki na jinsi ambavyo tunavyoweza
kunufaika na ufugaji huu na kuweza hata kuongeza kipato chetu.
Kwanza kabisa samaki ni kitoweo kinachotumika na kupendwa sana
hapa nchini na duniani kwa ujumla, zaidi ya kupendwa tu ni kitoweo chenye faida
kubwa kwa mwili wa binadamu ambapo inaongeza protini ya kutosha na madini na
hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye mlo kamili.
Kwa hiyo basi kutokana na uhitaji mkubwa wa samaki, watu wengi
sasa wameamua kuanza ufugaji katika maeneo yao, na imekuwa biashara nzuri sana.
Ningependa basi kuwashirikisha katika mambo ya kitaalamu yanayotakiwa
kuzingatiwa katika ufugaji huu. Karibuni.
Ukitaka kuchimba bwawa la samaki lazima kwanza uchague eneo
linalofaa. Katika kuchagua eneo linalofaa, kuna mambo ya kuzingatia kama
ifuatavyo;
i) Eneo lenye vyanzo vya maji vya uhakika kama vijito, chemi
chemi, na mifereji.
ii) Eneo lenye mwinuko wa wastani ili kurahisisha uchimbaji na uvunaji wa samaki kwa kukausha bwawa.
iii) Eneo lisilo na miti yenye kuleta kivuli.
iv) Eneo lililo karibu na nyumbani ili iwe rahisi kuhudumia bwawa na kuzuia maadui wa samaki.
v) Eneo lenye udongo unaofaa.
ii) Eneo lenye mwinuko wa wastani ili kurahisisha uchimbaji na uvunaji wa samaki kwa kukausha bwawa.
iii) Eneo lisilo na miti yenye kuleta kivuli.
iv) Eneo lililo karibu na nyumbani ili iwe rahisi kuhudumia bwawa na kuzuia maadui wa samaki.
v) Eneo lenye udongo unaofaa.
Ninaposema udongo unaofaa ni ule wa mfinyanzi unaotuamisha maji,
kwa mfano udongo unaotumika kufyatulia tofali au kutengenezea vyungu.
Njia mbili hutumika kujaribu kama udongo unafaa au la. Njia ya
kwanza ni kuchukua udongo kwenye kiganja kilichojaa, lowanisha na maji na kisha
finyanga kama tonge la ugali. Tupa juu tonge la udongo lililofinyangwa na
lidake linaporudi chini au liache lianguke chini.
Kama tonge litabaki limeshikamana, kuna uwezekano kuwa udongo huo unafaa na unatuamisha maji. Kama litatawanyika inaashiria kuwa udongo huo una mchanga mwingi zaidi ya mfinyanzi hivyo hautatuamisha maji.
Kama tonge litabaki limeshikamana, kuna uwezekano kuwa udongo huo unafaa na unatuamisha maji. Kama litatawanyika inaashiria kuwa udongo huo una mchanga mwingi zaidi ya mfinyanzi hivyo hautatuamisha maji.
Njia nyingine na ya uhakika zaidi ni ile ya kuchimba shimo lenye
kina cha kiuno. Jaribu udongo wa chini shimoni kama ulivyofanya kwenye jaribio
la kwanza. Kama tonge litatawanyika udongo huo haufai na kama tonge litabaki
limeshikamana, endelea na jaribio lingine.
Mapema asubuhi jaza maji shimoni ili kuona kama udongo utatuamisha maji. Finika
shimo kwa kutumia matawi au kitu chocho ili kizuia kuvukizwa ( evaporation).
Jioni jaza tena maji iwapo yatakuwa yamenywea ardhini.
Kama asubuhi inayofuata maji mengi yatakuwa yamebaki shimoni, basi hilo ni eneo zuri la kuchimba bwawa la samaki. Udongo huo utakuwa una uwezo wa kutunza maji ya kutosha ambayo ni muhimu kwa samaki bwawani mwako.
Kama asubuhi inayofuata maji mengi yatakuwa yamebaki shimoni, basi hilo ni eneo zuri la kuchimba bwawa la samaki. Udongo huo utakuwa una uwezo wa kutunza maji ya kutosha ambayo ni muhimu kwa samaki bwawani mwako.
Unaweza kuchimba bwawa lenye ukubwa wowote unaopenda. Uchimbaji
wa bwawa kubwa unahitaji muda, eneo, virutubisho na vilishio vingi zaidi kuliko
uchimbaji wa bwawa dogo. Hata hivyo utapata samaki wengi kutoka kwenye bwawa
kubwa.
Mfano bwawa lenye upana wa mita 10 na urefu mita 10 litakupa
samaki takribani 200. Bwawa lenye ukubwa wa mita 15 kwa 15 litakupa samaki kama
450 hivi.
Vitu vitakavyoamua ukubwa wa bwawa lako ni eneo ulilonalo,
upatikanaji wa mbolea ya kurutubisha maji na vyakula vya kulishia samaki. Ikiwa
huna mbolea na vyakula vya kutosha, ni bora kuchimba bwawa dogo.
Bwawa moja linalohudumiwa vizuri, litakupa mazao mengi zaidi ya
mabwawa mengi yenye huduma mbaya. Hivyo ni vema kuwa na bwawa moja
linalohudumiwa vizuri kuliko kuwa na mabwawa mengi yenye huduma duni.
Kama chanzo chako cha maji ni kijito, itabidi utengeneze sehemu
ya kuingizia maji upande wenye kina kifupi. Maji yanapaswa kuwa safi kabla ya
kuingia bwawani. Njia rahisi kuhakikisha kuwa maji yanayoingia bwawani ni safi
ni kuchimba shimo dogo nje ya bwawa kwenye mfereji wa kuingizia maji. Maji
yataingia kwenye shimo dogo na kutulia kabla ya kuingia bwawani. Kama kijito
hicho chenye chanzo chako cha maji kina samaki, zuia samaki kutoka kwenye mtoni
wasiingie bwawani kwa kuweka wavu kwenye mfereji. Weka wavu nje kidogo ya bwawa
kabla maji hayajaingia bwawani.
Kumbuka kuwa Bwawa la samaki lina sehemu mbili kwa ndani, sehemu
yenye kina kirefu na sehemu yenye kina kifupi.
Itabidi pia ujenge sehemu ya kutunzia mbolea kwa kutumia mianzi
au miti kwenye moja ya kona upande wenye kina kirefu. Sehemu ya kutunzia mbolea
inatakiwa iwe na ukubwa wa asilimia 20 ya ukubwa wa bwawa lote.
Sehemu ya kutunzia mbolea itahifadhi mbolea ambayo utaweka kwa ajili ya kurutubisha maji ya bwawa. Mbolea hii inatengeneza chakula cha asili cha samaki.
Sehemu ya kutunzia mbolea itahifadhi mbolea ambayo utaweka kwa ajili ya kurutubisha maji ya bwawa. Mbolea hii inatengeneza chakula cha asili cha samaki.
Ukimaliza kuchimba bwawa, panda nyasi juu ya tuta kuzuia
mmomonyoko wa udongo inaoweza kuletwa na mvua. Baada ya yote hayo bwawa lako
liko tayari kujazwa maji, kurutubishwa kwa mbolea na hatimaye kupandikizwa
vifaranga vya samaki.
Katika makala ijayo Utapata
maelezo zaidi ya jinsi utakavyoweza kuwalisha samaki wako.
Endelea kufuatilia.
Endelea kufuatilia.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA MTAALAMU WA KILIMO
MARCODENIS MISUNGWI.
MAWASILIANO:-
0768 470 808
Jun 27, 2020
Ni Muhimu Kutambua Mafanikio Ni Utamaduni.
Utamaduni
ni kigezo cha msingi kwa maendeleo ya jamii yoyote. Hakuna taifa lilowahi
kuendelea bila kujali utamaduni, kutii, na kufuata misingi muhimu ya utamaduni
wao.
Nchini
kwetu vitabu vingi vimeeleza maana ya utamaduni kwa ama upotoshaji mkubwa au tafsiri
nyonge, kwa mfano, vitabu vingi vinaufafanua utamaduni kama ngoma, harusi,
mavazi, vyakula, lugha, nyimbo, mila na desturi.
Kweli
hivi vinaweza kuwa viashiria au vipengele vya utamaduni, lakini ni kweli
utamaduni ndiyo huo? Matokeo ya tafsiri hizi na dhalimu ni kwamba watoto wetu
wanakuwa na kuelewa kuwa utamaduni ni ngoma au nyimbo, kuvaa manyoya, kucheza
na nguo zilizochanika mbele ya viongozi uwanja wa ndege kwa lengo la
kuwaburudisha wazungu wanaokuja kutembelea nchi yetu. Huo ni udhaifu mkubwa wa
mitaala yetu.
Kimsingi
utamaduni unatafsiriwa katika nyanja kuu tano;
Moja, ni fikra na namna mtu anavyofikiri. Eneo hili ndilo limekamata
sehemu kubwa ya matendo ya utamaduni wa mtu na matendo yake ya kila siku.
Pili, mitazamo, ni
eneo muhimu la utamaduni. Hapa akili imekamatwa na desturi zilizozaa mitazamo
inayomuongoza mtu kufanya anachotaka na
kuamini anachokiamini.
Tatu, mielekeo/utashi wa kimaisha, nalo
ni sehemu ya utamaduni wa jamii yoyote ile. Kila mtu ana mwelekeo anaouweka
katika kupambana na maisha ili kufikia maendeleo yake na familia. Mielekeo ndiyo
inayomtengeneza mtu kuwa mnyonyaji au mzalishaji.
Nne, imani,
Yaani kile mtu anachiokiamini na kukiishi ni kigezo muhimu cha kumfanya yeye
aendelee au abaki maskini. Imani ya mtu husanifu mitazamo na uamuzi wa
kimaisha.
Tano, mila, jadi na desturi.
Hizi zinajenga mtu na kumuumba awe alivyo. Na mara nyingi hujenga kanuni au
taratibu za kuishi. Mila jadi na tamaduni ndizo huunda michepuo ya akili ya
watu. Binadamu anaijua dunia kwanza kupitia jadi, mila na desturi ambayo ni
kanuni za msingi za kujenga ufahamu kwenye akili ya mtu. Ndiyo maana mila
desturi na jadi hazijaandikwa popote.
Haya
ni mambo ya muhimu katika utamaduni wa jamii yoyote ulimwenguni. Kuyadharau na
kukimbilia ngoma, nyimbo na mavazi ya asili ni sehemu ndogo ya ukweli wa nini
maana ya utamaduni.
Tukifahamu
hivyo tunaweza kuweka sera na mikakati ya maendeleo kwa kuzingatia utamaduni wa
jamii husika. Na ikumbukwe kwamba hakuna jamii hata moja duniani yenye
utamaduni mbaya. Kila linalofanyika ndani ya jamii linasababu yake, hata kama
ni mbaya kwa mwingine.
Kwa
Waarabu nguruwe ni haramu, lakini kwa Wazungu nguruwe ni nyama nono; Utamaduni
kwa Waafrika nyoka ni adui mkubwa lakini kwa Wachina nyoka ni nyama nono!
Hakuna utamaduni mbaya hapa duniani bali kuna desturi na vitendo vibaya ndani
ya jamii fulani.
Pili,
utamaduni hauna madaraja, kwamba, utamaduni wa jamii fulani ni mzuri kuliko
utamaduni wa jamii nyingine. Wengi wamepotoka na kuvurugwa na utamaduni wa
kizungu ulioletwa na wakoloni. Wanajaribu kudharau tamaduni zao na kujaribu
kuishi uzungu ambao wengi umewapeleka kuzimu na kuvuruga akili zao, sasa
wamegeuka kuwa watumwa wa wazungu. Michepuo ya akili hujengwa na tamaduni asili
siyo za kigeni. Ndiyo maana tunasoma lakini hatuna wabunifu wala wavumbuzi.
Utamaduni
unabeba vipengele vya msingi vya mchakato wa maendeleo na unasaidia kuimarisha
kujitegemea, mamlaka ya kujiamlia mambo yako mwenyewe na ni kitambulisho cha
taifa na ndiyo maana ni muhimu kutambua mafanikio ni utamaduni pia.
Bila
kutii na kuchambua fursa na vikwazo vya utamaduni wa jamii unayotaka
kuiendeleza, kamwe huwezi kupata maendeleo. Hii ni sababu inayofanya maelfu ya
miradi ya Benki ya dunia kushindwa kuleta maendeleo yoyote katika nchi maskini
ni kutotii utamaduni wa jamii husika.
Mathalani
mwananchi wa Uingereza anachofikiria kwanza akipata fedha ni tofauti na
mwananchi wa China na hata Vietnam. Vivyo hivyo, ukimpa laki moja Mchaga wa
Moshi, na Mnyiramba wa Singida kiasi hichohicho na uwaulize wanataka kufanya
nini, fikra na mipango inatofautiana pia.
Ukitumia
mabilioni ya fedha kununua chakula na vijiko vya misaada kuwapelekea waathirika
wa Tsunami huko India kaskazini na Bangladeshi, itakuwa ni upotezaji wa fedha.
Maana utamaduni wa Wahindi ni kula kwa mkono, hawatatumia vijiko kamwe.
Hii
ni mifano michache ya kuonyesha jinsi gani utamaduni una nguvu katika kuchochea
na kuzuia maendeleo. Miradi yoyote ya maendeleo duniani inabidi itanguliwe na
uchambuzi wa utamaduni wa mahali husika ili kuona fursa na vikwazo vilivyomo
kwenye utamaduni huo. Vinginevvyo ni kupoteza fedha na muda bure.
Miradi
ya maendeleo ni lazima iweze kutokana na jamii yenyewe. Ndiyo maana ni muhimu
jamii ichague vipaumbele vya maendeleo, kwani yenyewe ikachagua itaakisi utamaduni
na mahitaji yake, na kuifanya ishiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wake.
Yapo
hata mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yalifanya juhudi kubwa za kuanzisha
miradi ya maendeleo vijijini bila kuzingatia utamaduni wa mahali hapo. Miradi
mingi imeishia kupoteza fedha na muda. Umaskini umebaki palepale. Mradi unaobuniwa
Ulaya na wazungu, ukaletwa kijijini Chabutwa, kamwe hauwezi kuzaa matunda wala
kudumu.
Unaweza
kukua kwa siku za mwanzo lakini hauwezi kuondoa umaskini wala kuwa endelevu.
Lakini mradi utakaobuniwa na wanakijiji wa Chabutwa wenyewe, ukapata msaada wa
mashirika au serikali huo utakuwa endelevu na utaleta mafanikio makubwa na ya
kudumu kwa wanakijiji. Hii ni kwa sababu utakuwa umetoka kwao na umezingatia
utamaduni wao.
Wanafunzi
na jamii kwa ujumla wanapaswa kufundishwa ukweli kuwa kile ambacho utamadani
unagusa cha kwanza kabisa ni fikra, mitazamo, miiko, mwelekeo na wala siyo
ngoma na nyimbo tu kama ilivyozoeleka.
Lazima
wafundishwe mambo mazuri katika utamaduni wetu na yale mabaya ili wajue namna
ya kuyaepuka mabaya na kuyaendeleza mazuri.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA MTEMI ZOMBWE,
DAR ES SALAAM.
MAWASILIANO- 0713 000027
Jun 26, 2020
HADITHI; Acha Kufukuza Furaha, Kwa Sababu Ya Vitu Hivi…
Hapo
enzi za kale, kulikuwa na mzee aliyekuwa akiishi kijijini. Mzee huyu naweza
kusema, alikuwa ni mmoja wa watu wa bahati mbaya sana ulimwenguni, kwa nini
nasema hivi, ni kwa sababu, karibu kijiji kizima kilikuwa kimemchoka.
Mzee huyu alikuwa amechokwa kwa sababu gani,
kwani kila wakati yeye alikuwa anatetemeka, kila wakati alikuwa akilalamika tu
na kila wakati alikuwa katika hali mbaya, sura yake ikiwa imekunjamana kwa
kukunja uso.
Kwa jinsi
mzee huyu alivyokuwa akizidi kuishi kwa muda mrefu, maneno yake yalizidi kuwa
sumu kwa wengi na yasiyopendeza. Kwa hali hii watu walimwepuka, kwa sababu ya
kauli zake mbovu na mbaya za kukera.
Mzee huyu aliunda hisia za kutokuwa na furaha
kwa wengine. Kutokana na hisia hizo, pia alijikuta naye akichukiwa na wana
kijiji, kwa sababu ya hisia zake hizo na
tabia yake hiyo ambayo alikuwa amejitengenezea.
Lakini
siku moja, alipokuwa na umri wa miaka themanini, jambo la kushangaza lilitokea.
Mara moja kila mtu alianza kusikia uvumi huo, eti kwamba "mtu mzee anafurahi leo, halalamiki juu ya kitu chochote,
anatabasamu, na hata uso wake unatabasamu."
Kijiji
kizima kilikusanyika pamoja. Mzee huyo aliulizwa na wana kijiji, nini kimetokea
na kwa nini leo anaonekana ana furaha? Jibu, alilotoa mzee huyo lilishangaza
kidogo wengi, kwani aliwaambia hivi.
"Hakuna
kitu maalum kilichotokea, ila kwa miaka themanini najuta nimekuwa nikiifukuzia furaha, na sikuwa nikiipata. Na hapo niliamua
kuishi bila furaha, kumbe nilikuwa najitesa na sikujua kumbe furaha ipo ndani
mwangu tu”
….”Ndio
maana nimefurahi sasa baada ya kujua, vitu vya nje haviwezi kukupa furaha, bali
furaha ya kweli inaanza na wewe mwenyewe na mtazamo wako ulionao, lakini
kutafuta furaha ya nje huko ni kujichosha wewe.”
Fundisho
la hadithi hii fupi ni nini? Kwenye maisha yako, acha kufukuza furaha kwa
vitu vya nje, furahia maisha yako.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jun 25, 2020
Mambo Muhimu Mnapaswa Kuelewa Wakati Mnapitia Nyakati Ngumu Kiuchumi Kwenye Mahusiano Ya Ndoa.
Kuna
wakati katika maisha ya mahusiano yako
ya ndoa unaweza usiyaelewe kabisa, hii ni kwa sababu kuna wakati mnaweza
mkajikuta katika maisha hayo ya ndoa mnakata tamaa kabisa ya kuendelea kuishi
pamoja, hii ni kwa sababu ya ugumu wa maisha ambao mnaupitia.
Tumekuwa
mashuhuda wazuri sana kwa kuona ndoa nyingi zikivunjika katika karne hii, hii ni kwa sababu ya ugumu wa kiuchumi ambao
umejitokeza katikati ya safari ya mahusiano hayo ya ndoa.
Zipo
sababu nyingi ambazo husababisha mahusiano mengi ya ndoa kufa ila kubwa zaidi ni suala la kuyumba kwa
kiuchumi baina ya wanandoa hao husasani ukosefu wa kifedha katika kutekeleza
mambo mbalimbali.
Wapo pia baadhi wa wanawake wamediriki hata
kunyanyua vinywa vyao kuwatamkia waume zao kuwaita wanaume suluari hii yote
ikiwa waumeo hao wameyumba kiuchumi hawawapi mahitaji yao ya kifedha kama
ilivyokuwa hapo awali.
Kwani
hapo awali, mwanzo wa mahusiano hayo walikuwa wanapewa kila kitu kutoka kwa
wanaume wao, ila kwa sasa wamekuwa hawapati tena kile walichokuwa wanapewa
mwanzo. Ikumbukwe kuwa wanawake hao wamesahau kwamba katika safari mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka.
Kuna
wakati mtakuwa katika hali nzuri kiuchumi na kuna wakati mtakuwa na hali mbaya
sana kiuchumi. Hivyo mkiona mnapitia wakati mzuri kiuchumi katika mahusiano
yenu mnapaswa kumshukuru mwenyezi Mungu.
Pia
mnapopitia nyakati ngumu kiuchumi katika mahusiano yenu ya ndoa ni kwamba
mnapata kumshukuru Mungu kwa hatua ambayo mnapitia pia, Hii ni kwa sababu wapo
baadhi ya watu katika mahusiano ya ndoa wanapopitia kipindi ambacho wameyumba
kiuchumi wao hukata tamaa kabisa.
Wengi
wao wamefika hatua ya kutoona thamani ya
kuendelea kuishi tena kwa pamoja kwa sababu eti mambo yamekuwa hayaendi sawa. Ukiona hata wewe umefikia
hatua hii kumbuka kwamba mnakaribisha shetani aweze kuyasambaratisha mahusiano
yenu.
Kitu
pekee ambacho mnapaswa kuelewa wakati mnapitia nyakati ngumu kwenye mahusiano
ya ndoa hususani suala la kuyumba kiuchumi mnapaswa kufanya mambo yafuatayo;
Mtangulizeni Mungu;
Kama
nilivyosema hapo awali kwamba katika mahusiano ya ndoa kuna kupanda na kushuka,
kuna wakati mtakuwa vizuri kiuchumi na kuna wakati pia mtakuwa katika nyakati
ngumu.
Hivyo
inapotokea hali kama hii mnapaswa
kuelewa Mungu ndiye muweza wa kila jambo, hivyo mnapaswa kumuomba awasaidie
kuyalinda mahusiano yenu ya ndoa, vile vile
mnapaswa kumuomba yeye ili aweze
kuwasaidia katika kunyanyuka na kukua kiuchumi.
Msiruhusu Mawazo hasi
yawatawale.
Inapotokea
mmeyumba kiuchumi hampaswi kuyafanya mawazo hasi yatawale akili zenu, hii ni
kwa sababu ninyi ni watoto wema wa Mwenyezi Mungu na mawazo hasi ni ya shetani.
Hivyo
mnapoyaruhusu mawazo hasi yatawale akili zetu ni kwamba ninyi mtaona njia bora
ya kutatua tatizo hilo ni kuachana na kufanya kila mtu afanye mambo yake,
kitendo hicho si kizuri kwa sababu mnakiuka kiapo chenu cha ndoa pia
mnamkaribisha shetani aweze kuwatala vyema.
Shirikianeni katika kazi.
Miongoni
mwa mambo yatakayowasidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kuwa na mahusiano
ya ndoa yaliyobora ni pamoja na kushirikiana vyema katika kufanya kazi.
Ni
muhimu kushirikiana vyema katika kufanya
kazi kwa sababu hata pale inapotokea kuna anguko la kiuchumi basi wote muweze
kujua ni wapi ambapo pamewafanya mpate anguko hilo la kiuchumi.
Jambo
hili ni muhimu sana, hii ni kwa sababu ndoa nyingi zinaamini mtu mmoja ndiye
ambaye atahusika kuinua uchumi wa familia, hili si kweli bali ukweli mnatakiwa
kushirikiana vizuri kwenye kila kazi mnayoifanya ili mjue faida na hasara
mnayoipata katika kazi fulani muifanyayo.
Jifunzeni kuweka akiba.
Ili
msiweze kupata anguko la kiuchumi kwa namna moja ama nyingine basi kila
wanandoa ni vyema wakajifunza kuweka akiba. Kuweka akiba ni muhimu sana kwa
sababu kuna wakati akiba hiyo hutumika hasa pale unapokuwa umepatwa na anguko
kiuchumi.
Hivyo
kivyovyote vile wanandoa mnapaswa kujifunza juu ya utaratibu wa kuwekea akiba
ila akiba hiyo iweze kuwasaidia baadae
hasa pale mnapopata angulo la kiuchumi.
Jifunze kutokana na makosa.
Kuanguka
kiuchumi isiwe sababu kwa wanandoa kukata tamaa bali liwe na somo kwao kuona ni
wapi ambapo wamekosea na kurekebisha makosa yao.
Pia
ikumbukwe kuwa unafuu wa kila jambo hususani suala la unguko la kiuchumi kwa
wanandoa hutokana na anguko hilo kama somo la kuweze kurekebisha makosa ili
baadae waweze kuwa vizuri zaidi.
Hivyo
ikiwa mmepata anguko katika mahusiano yenu ya ndoa mnapaswa kujifunza namna ya
kutokana na anguko hilo ila baadae msiweze kuanguka tena.
Mkiyazingatia
hayo yote ambayo nimeyaeleza kwa siku ya leo ni kwamba maisha yenu ya ndoa
yatakuwa ni mzuri sana, kila mmoja wetu atayafurahia mahusiano hayo. Asante.
Ndimi; Afisa Mipango Benson Chonya
0757-909942
Jun 23, 2020
Jifunze Mambo Haya Utafanikiwa.
Msingi wa maisha ya mafanikio upo kwenye kujifunza. Kupitia kujifunza kuna mambo mengi utayajua na yatakusaidia sana ikiwa utayafanyia kazi.
Kupitia makala haya, nimekuandalia mambo mbali mbali ya kujifunza katika maisha ili uweze kufanikiwa. Mambo hayo ni yepi, twende pamoja kujifunza.
1. Unapokuwa mjasiriamali unatakiwa uwe na maono, imani na moyo wa kusonga mbele. Hivi ni vitu vya msingi unatakiwa kuwa navyo. Kama utakosa kitu kimojawapo hapo, itakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa.
VISION + FAITH + COURAGE.
Kama ukiwa na vitu hivyo, basi safari yako ya ujasiriamali itakuwa ya mafanikio. Hata Nuhu wakati anajenga safina alikuwa na vitu hivyo vitatu vya msingi sana na ambavyo kwa kila mjasiriamali anatakiwa awe navyo na kuvitumia.
Hebu fikiria, wakati nuhu anamwambia mkewe, na watoto wake kwamba anajenga safina, unafikiri watoto wake walimshangaa vipi, unafikiri mkewe na jamii ilimshangaa vipi? Hapa ni lazima Nuhu alionekana kituko.
Amini wengi walimwambia mzee unaota hii ni nchi ya jangwa, hakuna mvua kubwa ya namna hiyo ambayo inaweza ikanyesha. Inawezekana mzee Nuhu sasa unaelekea kuchanganyikiwa. Hayo ndio maneno alikuwa pengine akipewa.
Lakini, kwa sababu ya maono, imani na nguvu ya kuendelea mbele, Nuhu aliamua kufanya kazi hiyo bila kuchoka ya kujenga safina. Na mwisho wa siku safina ikapona na baada ya muda mvua ikanyesha.
Jiulize ukiwa mjasiriamali, je, una maono/vision? Je, una faith/Imani ya kukuongoza, je una courage/ moyo wa kuendelea mbele hata kama kuna watu wanakukatisha tamaa. Vitu hivi ni lazima na muhimu ili uweze kufanikiwa kwenye ujasiriamali wako.
2. Huwezi ukajifunza biashara kwenye kitabu, ni lazima uwe na biashara halisi na ambayo utakuwa unaifanyia mazoezi kila siku ili ikupe mafanikio. Kama unaishia kujifunza kwenye vitabu na kusema unajifunza biashara unapotea.
3. Marafiki hawana uwezo mkubwa wa kutengeneza biashara ya ushirika/ business partner. Jifunze kutengeneza biashara ambayo haina uwezo wa kuhusisha ushirika wa marafiki yaani hapa namaanisha business partner.
4. Ni muhimu kwako kuwa na kumbukumbu au rekodi za kipesa; kila pesa unayoitumia ni lazima iwe na rekodi zake. Usikubali kutumia pesa hovyo pasipo kuwa na kumbukumbu zake huko kunakuwa ni kujipoteza wewe.
5. Kuna wakati inachukua pesa nyingi, kutengeneza biashara ambayo unayoipenda. Si kitu cha mara moja, biashara sahihi inataka pesa, hivyo ukae hilo ukilijua akilini mwako kwamba pesa inahitajika.
6. Sio ukosefu wa pesa ndio unaua biashara, bali biashara zinakufa kwa sababu ya kukosa uzoefu kwenye biashara na kukosa kusema ukweli. Hayo ndio mambo mawili yanayoua sana biashara nyingi sana kila wakati.
7. Kila unaposhindwa, iwe kwenye biashara au kwenye jambo lolote. Hiyo inakuonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo wewe hujui mambo mengi, na ni wapi urekebishe, kwa hiyo kushindwa kwako isiwe inshu, jifunze kwa kushindwa kwako.
8. Ni muhimu sana kuwa na elimu ya msingi wa pesa, mapema kwenye maisha yako. Ikiwezekana elimu hii, itafute kila siku na anza kuwapa watoto wako mapema, kwani itawasaidia kujenga msingi bora sana wa maisha yao ya kifedha.
9. Watu wengi wanafanya kazi hadi uzeeni kwa sababu, ni watu ambao wanakuwa bado hawajajiandaa na maisha ya uzeeni. Hata watu hao ukiwaona wamevaa suti na wamependeza, lakini wanakuwa hawajajiandaa na maisha, baada ya kustaafu.
10. Kama unatafuta pesa au unafanya uwekezaji wowote anza kuufanya kwanza kichwani mwako. Kama pesa utaanza kuiona kwenye akili yako, huku nje nako utaiona tu. Pesa ukiona kwenye akili kwanza, amini na kwa nje pia utaipata.
11. Kwenye maisha yako jifunze kuwa mwekezaji/investors na usiishie kuwa mfanyabiashara tu. Faida kubwa ya kuwa mwekezaji ni kwamba, hata soko likibadilika na kushuka sana bado mwekezaji ataendelea sana kutengeneza pesa ya kutosha na faida juu.
Uzuri wa mwekezaji ni kwamba anatengeneza pesa wakati wote. Kiwe kipindi kigumu pesa inatengenezwa au kipindi cha kawaida pesa inatengenezwa. Hivyo, mwekezaji hawezi kulia lia na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi kama alivyo mfanyabiashara.
12. Kila wakati unatakiwa kujua kwamba, kuna mabadiliko ya kiuchumi, ambayo yanaweza kutokea mbele ya maisha yako. Usifikiri hali ya uchumi ya sasa na ndio itakuwa kesho. Kaa, ukijua, maisha yanabadilika na wewe unatakiwa kubadilika.
13. Kama unaishi maisha yale yale, kama unachukua hatua zilezile, sahau kabisa maisha yako ya kesho kuwa bora kuliko yalivyo leo. Hiyo ni kwa sababu, hatua unazozichukua ni zile zile na hakuna mabadiliko, kwa hiyo hata matokeo ni yale yale.
14. Unaweza ukapoteza kila kitu, na ukajikuta umeingia kwenye ulimwengu halisi huna kitu. Hata hivyo nikwambie, unaweza ukarudi kule ulikotoka, na ukajenga mafanikio upya ikiwa wewe utaamua iwe kwako hivyo na ukachukua hatua madhubuti.
15. Ni vyema na ni vizuri kuwa na mpango sahihi wa kustaafu. Nchi, nyingi duniani zina mpango sahihi wa kustaafu kwa wananchi wake. Hata kampuni, zinaandaa mpango sahihi wa kustaafu kwa wafanya kazi wake. Na wewe unatakiwa uwe na mpango wako sahihi wa kujiandaa na uzeeni.
16. Watu wengi wenye maisha ya kati, wanashindwa kuwa matajiri kwa sababu, ya kukosa elimu ya pesa. Kwa kadri unavyokosa elimu ya pesa ndivyo uwekezaji kwako unakuwa mgumu na unajikuta unapoteza pesa nyingi ukiwekeza.
Dawa ni kuwa na elimu nzuri ya pesa, ili ukiwekeza uweze kufanikiwa. Ukikosa elimu ya pesa, unajiweka kwenye wakati mgumu sana wa wewe kuweza kufanikiwa. Anza kujifua na kuwekeza kwenye elimu ya pesa, itakusaidia sana kufanikiwa kwako.
17. Kuna elimu tatu za muhimu. Hizi ni elimu ambazo kila mmoja anatakiwa kuzijua zote, ingawa kwa bahati mbaya elimu mojawapo kati ya hizo tatu, haifundishwi shuleni.
Kwa kifupi, haya ndio Mambo ya msingi ambayo unaweza utajifunza kqmwenye maisha yako na kufanikiwa. Hebu chukua hatua na hakikisha ndoto zako zinatimia. Kila la kheri.
Jun 22, 2020
Kama Utatumia Nguvu Hizi, Ni Lazima Ufanikiwe.
Binadamu
tumeumbiwa nguvu za aina nne ambazo tunatakiwa kuzitumia kwa ufasaha ili tuweze
kupata mafanikio makubwa. Kama utaweza kumudu kuzitumia nguvu hizo vizuri, ni
wazi utafanikiwa na hakuna ubishi.
Watu
wengi hawafanikiwi kwa sababu, kwa namna moja au nyingine hawatumii nguvu hizo
kiufasaha au kuna baadhi ya nguvu hawazitumii kabisa. Katika Makala haya nataka
kukuonyesha nguvu hizo, ikiwa utazitumia, utafanikiwa.
1.
Nguvu ya mwili (Physical energy).
Ili
kufanikiwa, unahitaji mwili wenye afya, unahitaji mwili wenye nguvu ili
ukusaidie kufanya kazi zako. Kama utakuwa una mwili ambao hauna afya, sahau
mafanikio. Ndio maana tunasema, afya ndio kitu cha kwanza kwenye maisha yako.
Kwa hiyo
kila siku, kabla hujafanya kazi zako, angalia kazi ambazo zinahitaji matumizi
makubwa ya nguvu za mwili kabla hujachoka. Kisha, anza na kazi hizo ili
ukichoka utafanya kazi laini, lakini ukumbuke nguvu ya mwili ni muhimu sana.
2. Nguvu ya ubora (Emotional energy).
2. Nguvu ya ubora (Emotional energy).
Hapo
ulipo ndani mwako una nguvu fulani ya ubora ambayo imejificha. Ili ubora huo
uweze kuonekana kwa nje unatakiwa kutumia kwa namna moja au nyingine. Kama
utaulalia ubora wako basi tu elewa utakwama.
Unatakiwa
kuujua na kuutumia ubora wako kwa namna yoyote ile. Usijadanye kwamba wewe si
bora, hapana, ndani yako una ubora wa aina fulani ambao unatakiwa kutumia kila
siku ili ukuletee mafanikio na maajabu makubwa.
3. Nguvu
ya akili (Mental energy).
Pia
akili ni nguvu mojawapo ambayo umeumbiwa ili tuweze kufanikiwa. Kama umeweza
kusoma hapa, basi akili zako ziko sawa na unatakiwa ujue jinsi ya kutumia nguvu
hiyo ya akili ili kujenga mafanikio makubwa.
Watu
unawaona wana mafanikio, wanatumia akili zao ili kuweza kufanikiwa. Na wewe
unaweza ukatumia akili zako kuweza kufanikiwa kwa viwango vya juu sana. Sugua
akili yako na ujue ni nini cha kufanya, na nini ambacho hutakiwi kufanya.
4. Nguvu ya kiroho (Spritual energy).
Hii ni
pia ni nguvu muhimu kwa sababu, inasaidia kutuongoza kujua ni lipi jema na lipi
ambalo sio jema. Kwa kujua hivyo inasaidia sana kututengenezea mafanikio
makubwa maisha mwetu kila wakati.
Hivyo
kwa kufika hapo, bila shaka umezijua nguvu nne, ambazo nguvu hizo kila binadamu
anatakiwa kuzitumia ili kufanikiwa. Kwa kumudu kutumia nguvu hizo mafanikio
kwako yatakuwa jambo la lazima na si kuuliza tena.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jun 21, 2020
Ikiwa Unapata Matokeo Usiyoyataka, Acha Kujiona Hivi.
Ikiwa unapata
matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge na
kukata tamaa, endelea kuweka juhudi. Kwa kuendelea kuweka juhudi huko, matokeo
unayoyataka utayapata.
Ikiwa unapitia
kwenye changamoto nyingi za kimaisha pia acha kukata tamaa, endelea kuweka
juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto hizo na kuwa huru, huwezi
kubaki kwenye changamoto hizo milele.
Ikiwa huridhiki
kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye
umepoteza, pia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi. Kwa kuendelea kuweka
juhudi, itafika wakati utaona mwelekeo wa maisha yako.
Kwa kila hatua
unayochukua kwenye maisha yako hata ikiwa ndogo sana, inaleta mabadiliko kwenye
maisha yako. Usijadanganye eti hatua hii ni ndogo haiwezi kuleta mabadiliko,
kila hatua inaleta mabadiliko kwenye maisha yako hata kama huyaoni.
Angalia ulikotoka
kwenye maisha, sasa kwa nini ukate tamaa na wakati sasa hivi upo mbali sana?
Dawa si kukata tamaa ni kuweka juhudi tena. Usikubali ukakatishwa tamaa na chochote,
weka juhudi utafanikiwa.
Hata upate matokeo
mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani
lazima juhudi zako zitaleta matunda. Matokeo mabaya unayoyaona, ni ya muda tu,
lakini una uwezo wa kuyabadili sana.
Hakuna mtu katika
dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo
hayupo. Kila anayeweka juhudi endelevu, mwisho wake unakuwa mzuri na anavuna
anachokitaka.
Hivyo, hata
ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani
upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa huyaoni mabadiliko hayo kwa nje.
Kila hatua
unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. Hakuna hatua
utakayochukua na kuifanyia kazi halafu ikaja kukuangusha, hata ukianguka chukua
kama fundisho. Chukua hatua sahihi, ili ufikie mafanikio yako.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jun 20, 2020
Jenga Utaratibu Wa Kujiuliza Maswali Haya, Utafanikiwa.
Katika maisha yako,
anza kujenga utaratibu mpya wa kujiuliza maswali kwa mambo unayoyataka yawe
katika maisha yako. Kwa mfano, unaweza ukawa unajiuliza nina fanyaje ili
niingize kipato kikubwa zaidi au ninafanyaje ili niweze kutoka hapa nilipo.
Akili kama akili
imeumbwa ili ikusaidie kutafuta majibu kwa yale mambo magumu. Sasa kama upo upo
huisumbui akili yako ikusaidie kutatua changamoto zako, aisee uwe na uhakika
utabaki sana hapo ulipo.
Kumbuka kila wakati
akili ya binadamu, inafanya kazi kwa kuuliza maswali na kujijibu. Chochote
ambacho unajiuliza sana kwenye akili yako haijalishi ni kibaya au kizuri, ni
lazima kitu hicho utaweza kukipata.
Acha kukukosea
katika hili, jiulize maswali magumu yatakayosaidia kuboresha maisha yako. Ukiisumbua
akili yako, utapata hicho unachokihitaji na utajenga msingi wa maisha bora sana
kwako na kizazi chako cha baadae.
Ukiilaza akili yako, na ujue pia kuna mambo mengi sana utayalaza na hutafika mbali kimafanikio. Kwa hiyo jukumu lako ni kila siku kuisumbua akili yako ikupe majibu ya kitu gani unachokitaka maishani.
Ukiilaza akili yako, na ujue pia kuna mambo mengi sana utayalaza na hutafika mbali kimafanikio. Kwa hiyo jukumu lako ni kila siku kuisumbua akili yako ikupe majibu ya kitu gani unachokitaka maishani.
Kwa kadri
unavyoisumbua akili yako, utakuta majibu na yale mambo unayoyataka unayapata. Acha
kulaza damu waza, tumia kichwa chako kufikiri na sio kutumia kichwa chako
kukiburudisha tu na kutulia.
Nikwambie, hutaweza
kufa eti kwa sababu ya kuwaza, sumbua akili yako, waza tena na tena mpaka upate
majibu sahihi ya nini unachokitaka kwenye maisha yako. Waliofanikiwa elewa,
wanasumbua akili zao na sio watu wa kulala tu.
Akili inayojishughulisha
na kutafuta majibu ya changamoto ndio inayofanikiwa. Ikiwa wewe unajidanganya
kwamba mafanikio yako yatakuja yenyewe, nakwambia unajidanganya na hautaweza
kufika popote kwa sababu unajidanganya.
Usikubali kushindwa
kwa kujiambia ‘oooh mimi siwezi,’ nani aliyekwambia huwezi? Akili yako umepewa ina
nguvu na majibu mengi ya changamoto zako. Ikiwa kweli umewaza na umefika
mwisho, nikwambie Mungu ataonyesha njia kwako.
Kama haujishughulishi
na kuwaza, kutafuta suluhu ya changamoto zako na ukaamua kutafuta msaada wa
Mungu, kwako ni lazima utakwama. Umiza akili yako, jenga uataratibu wa
kujiuliza maswali kwa yale unayotaka na utafanikiwa.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA
MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF
WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo
utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa
vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app;
0713048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jun 17, 2020
Haya Ndiyo Mahitaji Muhimu Kwako Yatakayokupa Maisha Ya Mafanikio.
Yapo mahitaji matatu ambayo ni ya lazima kwako ili
kuishi vizuri na kukujengea msingi mkubwa wa mafanikio. Haya ni mahitaji ambayo
kwa namna yoyote ile huwezi kuyakwepa, ni lazima uwe nayo na uyatawa
Kwanza,
mahitaji ya mwili,
hapa ni lazima mwili wako unahitaji kuvishwa nguo nzuri na kula chakula kizuri
ili kujenga afya. Kama huli vizuri ni rahisi sana na mambo mengine pia kwenda
hovyo.
Pili,
mahitaji ya akili, ili
akili yako ifanye kazi vizuri ni lazima pia kuizoesha kuilisha vizuri kwa
kujifunza. Hata kama sio utamaduni wako kujifunza, hebu anza kidogo kidogo.
Jifunze kusoma vitabu vya kukujenga na sio kukubomoa.
Tatu,
mahitaji ya kiroho, ni
lazima sana pia kukua kiroho ili kuleta usawa katika maeneo yote matatu.
Unahitaji kujifunza neno la Mungu na kutambua misingi ya kiroho. Kumbuka sisi sio
miili tu ni zaidi ya hapo.
Maisha yako yanakuwa sawa na maana ikiwa maeneo yote
hayo matatu yatakuwa na uwiano ulio sawa. Hakuna mwenye mafanikio makubwa na
akawa na furaha kama eneo moja hapo likawa lina upungufu mkubwa.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kumbuka, ufalme hauji kwa maneno bali unakuja kwa vitendo,...chukua hatua.
Nikutakie kila la kheri,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA NDOTO ZAKO ZITUMIE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Mawasiliano, Whats app; 0713048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)