google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 25, 2016

Mambo Ya Kuzingatia Katika Biashara.

No comments :
Yamkini unataka kufanya biashara, au umekwishanza kufanya ila katika biashara unayofanya mara nyingi huoni matokeo ambayo ulikuwa unategemea. Hii ni kutoka unafananya au ulifanya biashara kwa kutokufanya uchunguzi wa kina juu ya biashara hiyo. Unajua ni kwanini  biashara yako haisongi mbele? Shusha pumzi kisha twende sawa kwani leo ndio siku ya pekee kwako kuweza kuona unapata faida endapo utaisoma Makala hii kwa umakini na kuielewa kisha kuiweka katika matendo, kwani inawezekana ukawa ni mfuatiliaji mzuri lakini sio mtendaji mzuri ila nikuombe tena kwa mara nyingine utakachokisoma hapa kiweke katika matendo na utakwenda kuona matokeo yake.

Yafuatayo ndiyo mambo ya kuzingatia katika biashara.

1. Elewa biashara yako vizuri.


Mara nyingi inawezakana unashindwa kuona unapata mafanikio hii ni kwa sababu hauifamu biashara yako vizuri. Inawezekana ukawa haujanielewa twende sawa, kuifamu biashara hapa nina maana ya kwamba watu wengi tunafanya biashara  kutokana na kusikia kwa watu ambao wamesema kuwa biashara fulani inalipa, na baada ya kusikia hayo unakwenda moja kwa moja kwenda kuifanya matokeo yake biashara hiyo inakufa. Hii unajua ni kwanini ni kutokana  na hukufanya utafiti wa kutosha juu biashara hiyo. Inawezekana kweli biashara fulani ikawa inalipa na wewe ukagundua hilo jambo la msingi jaribu kuchunguza ni mbinu zipi ambazo wanazutumia mpaka waseme hivyo.

Pia ukumbuke ya kwamba kusikia peke yake haitoshi, moja ya sifa kubwa ya mjasiliamali ni lazima ajue kufanya uchunguzi wa kutosha wa jambo lolote kabla hajaanza kulifanya. Wito wangu kwako Ni kwamba itambue biashara yako vizuri hii itakusaidia kujua changamoto na jinsi ya kukabiliana nazo. Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika ya kwamba usiishie kusema ndoto yangu ni kuwa hivi na vile bali anza kufanya sasa, ndoto hiyo kuwa kweli. Amini ya kwamba unaweza kuifanya ndoto kuwa kweli ndani ya muda mfupi.

2. Simamia na thibiti biashara yako.
Hili jambo la msingi zaidi kuliko hata kula anashangaa! Usishangae wala hujakosea kusoma upo sawa kabisa. Unajua kwa nini nimesema hivyo watu wengi biashara nyingi hazina Maisha marefu hii ni kutoka hatuna usimamizi wa mzuri wa shughuli zetu. Tupo baadhi yetu tunaendesha biashara kubwa ambazo kwa siku zinaingiza pesa nyingi kwa kuwa tunakwepa kuwalipa wafanyakazi mishara mikubwa tunajikuta tunawatafuta watu wanyonge wawe wasimamizi wa biashara hizo na kuwalipa mishara midogo na kwa kuwa wafanyakazi hao wanajua wewe bosi unaingiza shilingi ngapi mwisho wa siku wanaona unawalipa mishara midogo wanaanza kukuibia.

Kitu cha msingi ni kwamba jaribu kuwajenga wafanyakazi wako waione biashara yako ni sehemu ya maisha yao. Wapo baadhi ya wafanyakazi katika biashara endapo atanunua hata nguo mpya bosi wake humuuliza hiyo nguo umeitoa wapi unashangaa huo ndio ukweli, wewe bosi ukiishi katika misingi hiyo ni lazima utaibiwa tu kila siku na biashara yako haitakuwa ikisonga mbele maana kila mfanyakazi unayemuajiri utamuona jipu tu.

Kumbuka ya kwamba kuwa biashara yako inaweza kukua kwa kumfanya mfanyakazi kwa kumfundisha mambo ambayo yataijenga biashara yako. Mfundishe mfanyakzi wako kuweza kuongea vizuri na wateja, mfundishe kuandika kumbukumbu kwa kila mzigo unao ingia na kutoka hii itakusaidi sana pia na wewe bosi ni lazima uwe daftari ya tarifa ya kumbukumbu tofauti na wafanyakazi wako. Moja ya sababu inayopelekea biashara nyingi kufa ni kule kutokuwa na mahusiano mazuri baina ya mwajiri na mfanyakazi. Wito wangu kwako mfanyakazi ipende kazi yako kuwa mbunifu kwa kumshauri mwajiri wako mbinu kadha wa kadha katika kupanua soko. Na wewe mwajiri Kuwa na mahusiano mazuri na mfanyakazi usimuone eti kwa sababu hana pesa na elimu ya kutosha kama wewe.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada. Asante kwa kusoma Makala haya tukutane tena katika Makala ijayo.

Apr 22, 2016

Kitu Kinachokufanya Ushindwe Kutimiza Malengo Yako.

No comments :
Bila shaka umewahi kuwaona watu ambao katika maisha yao siku zote ni watu wasio na pesa na ni watu ambao wanaishi maisha ya kutotimiza  malengo yao siku hadi siku. Umeshawi kujiuliza watu hawa tatizo kubwa walilonalo nini linaowafanya waishi maisha hayo siku zote?Ni kitu ambacho pengine kimekuwa kikikushangaza.

Ukija kuangalia ama ukichunguza kwa makini utagundua kuwa watu hawa, ambao  inaweza ikawa ni wewe pia, wamekuwa wakiishi maisha ya kutokutimiza malengo yao  sio kwa sababu hawana pesa ama muda wa kutimiza malengo yao. Kitu kikubwa kinachowafanya wasitimize malengo ni kukosa nguvu ya uzingativu katika malengo yao.

Hiki ndicho kitu muhimu wamekiwa wakikikosa katika maisha yao na kimewafanya waishi maisha magumu yasiyo na pesa. Kwa kawaida, unapokosa nguvu ya uzingativu na kushindwa kutilia mkazo kwa kujikumbushia malengo yako mara kwa mara kinachotokea kwako ni lazima ushindwe kufikia malengo yako.


Watu wengi wenye mafanikio makubwa wanajua ukweli huu na wanaufanyia kazi kila siku kwa kujikumbushia malengo yao mpaka yanatimia. Kama unafikiri natania nenda kamuulize Thomas Edson na ugunduzi wake wa glopu/balbu alikosea mara 9999 bila kuchoka hadi akaja kugundua kitu ambacho kina manufaa kwetu mpaka leo.


Kama Thomas Edson angekata tamaa na kushindwa kuweka nguvu za kutosha za uzingativu kwenye malengo yake aliyojiwekea basi pengine leo hii dunia yote ingekuwa inalala giza. Kunapokuwa na nguvu ya uzingativu na kuielekeza akili yako yote kwa kile unachokifanya huwa kuna matokeo makubwa ya kimafanikio.

Nakumbuka nikiwa darasa la sita, katika somo la sayansi mwalimu wangu mmoja alikuwa akitufundisha namna ya kutumia kioo ambacho kilikuwa kipo katika mfumo wa lensi kuweza kuchoma vitu kama karatasi. Alikuwa akichukua kioo kile na kukielekeza kwenye karatasi ambapo baada ya muda kwa kukiweka kioo sehemu moja kilikuwa kinakusanya mwanga wa jua na kuweza kuchoma karatasi.

Mwalimu Yule aliweza kutufafanulia  kuwa mwanga wa jua una nguvu sana lakini kama umesambaa hauwezi kuleta madhara yoyote, mpaka ukusanywe pamoja na kitu kama lensi ya kioo ndio unaweza ukaleta madhara na kuchoma vitu kama karatasi. Kwa kupitia mfano huo hivyo ndivyo tulivyo katika maisha yetu.


Mara nyingi binadamu tunazonguvu nyingi sana na kubwa ambazo tunauwezo wa kuzitumia na kutuletea mabadiliko makubwa katika maisha yetu kama tutaziwekea nguvu ya uzingativu. Yale mambo ambayo umekuwa ukishindwa mara kwa mara ukijakuangalia unashindwa sio kwa sababu huwezi ila ni kwa sababu unakosa nguvu hii muhimu kwako.

Kama unataka kufanikisha malengo yako na kuona ndoto zako zikiwa zinatimia ni jukumu lako wewe kuweza kujifunza kutumia nguvu hii vizuri ya uzingativu ili ikuletee matokea chanya unayohitaji. Hata kama umeshindwa mara ngapi kwa kile unachokifanya acha kupoteza mwelekeo kwa kukosa nguvu hii muhimu kwako na mafanikio yako.

Kitu pekee kinachowafanya watu wengi wawe waoga, wawe watu wa kuahirisha mambo, wakose uvumilivu na nidhamu binafsi  ni kutokana na kukosa nguvu hii ambayo wakiwa nayo itawasaidia kufikia malengo yao waliyojiwekea. Unapokosa uzingativu wa kulenga kile unachokitaka kiwe katika maisha yako, inakuwa ni ngumu sana kufikia malengo yako.

Ili uweze kutimiza malengo yako unahitaji kuwa na nguvu ya uzingativu hasa kwenye malengo yako iliyojiwekea kila wakati. Kuwa na mafanikio siyo suala la bahati kama wengi wanavyofikiri ni kitu cha kupanga na kuamua kisha kuweka nguvu zako zote huko, uwe na uhakika malengo yako hapo yatatimia.

Nakutakia mafanikio mema, endelea kutemblea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza na kuhamasika, mpaka maisha yako yaimarike.

IMANI NGWANGWALU,









Apr 21, 2016

Kinachokufanya Ushindwe Kufikia Uhuru Wa Kipesa Ni Hiki Hapa.

No comments :
Kwa wale wafatiliaji wazuri wa mtandao wetu wa dira ya mafanikio wiki iliyopita katika moja ya makala zetu tuliongelea juu ya tabia ambazo zinaweza zikakuzuia kupata kiasi kikubwa cha pesa unachokitaka. Kwa kifupi tuliona mchango wa tabia hizo katika suala zima la kukuzuia wewe kupata pesa za kutosha. Leo katika makala haya, mbali na tabia hizo tutaangalia kitu kingine cha kipekee ambacho kina uwezo mkubwa wa kukufaya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa hata kama unaweka juhudi nyingi.
Najua unatamani kujua kitu hiki ambacho kinauwezo mkubwa wa kukuzuia kupata pesa. kama ni hivyo tulia, acha kuwa na haraka sana. Kumbuka kwamba wakati mwingine, linapokuja suala la kukosa kile kiwango cha pesa unachotaka tatizo huwa sio ukosefu wa pesa, au pesa hazitoshi kama wengi wanavyodai. Tatizo huwa ni moja tu ambalo ni hofu ya kupata kiwango kile cha pesa unachokihitaji. Usishangae sana hili ndilo tatizo lingine linalokufanya ushindwe kufikia uhuru wa kipesa unaoutaka.

Naona hunielewi elewi vizuri na unajiuliza maswali mengi kwamba ninaongea kitu gani? Sikiliza. Kama wewe ni mfanyakazi na unataka kujiajiri na umeona biashara fulani ndiyo itakayokulipa moja kati ya maswali ambayo utakuwa unawauliza sana watu ambao walishafanya hiyo bishara hiyo ni kwamba hivi nitapata kiasi hiki cha pesa kwa mwezi. Unajua ni kiasi gani ambacho utakuwa unauliza? Ni ile pesa ambayo unataka kujua kama itakuwa sawa na ile unayolipwa. Utakuwa una lengo la kulinganisha mshahara na pesa unayoipata kwenye biashara.
Sasa unapoona hivyo ujue hiyo ni moja ya hofu ambayo inaweza kukuzuia kufikia kwenye uhuru wa kipesa. Unapochagua kufanya biashara fanya biashara kwa nguvu zote. Kwa kadri unavyozidi kuendelea inakuwa inazidi kukua polepole na kuwa biashara kubwa kuliko ulivyokuwa ukifikiri. Lakini suala la kujijengea hofu sana litakuzuia kufikia uhuru wa kipesa usipokuwa makini. Waangalie wote wenye hofu kama waapesa. Naamini unajua hwana pesa nalo. Hofu haina msaada wowote katika maisha yako, hata wewe kama hofu yako ni kubwa huwezi kufikia uhuru wa kipesa na huwezi pata pesa pia.
Ili uweze kufikia uhuru wa kipesa jenga imani kubwa ndani yako ya kuamini kwamba hilo kwanza linawezekana. Ukishajijengea hiyo imani anza kuchukua hatua. Kwa kuchukua hatua, hiyo itakusaidia sana kufikia mafanikio makubwa. Acha kuruhusu imani ya ‘siwezi’ ikakutawala ndani yako. Kama utakuwa na imani hii basi itakuwa ni chanzo kimojawapo kikubwa cha kukufanya ushindwe kufikia uhuru wa kifedha.
Kwa leo tuishie hapa ila kumbuka endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,

Apr 20, 2016

Huu Ndio Mchango Sahihi Wa Marafiki Katika Maisha Yako.

No comments :
Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.  Aina ya kwanza ni marafiki ambao ni wema na marafiki wabaya. Tukianza na kuangalia aina hiyo  ya kwanza hao ni marafiki ambao ni watu ambao wana mawazo chanya katika kushauri hata kutenda mambo mbalimbali. Pia katika kundi hili la marafiki wapo marafiki wa aina hii wachache sana.
Aina ya pili ya marafiki hawa ni marafiki ambao ni watu ambao hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa tu.
Watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu ambazo hatusatili kuishi na watu hao . Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba ushauri kwa watu ambao sio sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao.
Tumekuwa tukushuhudia  baadhi ya wanafunzi ambao pindi waendapo  masomoni baada ya kufikia huko wamekuwa na tabia za ajabu hii ni kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi. Tumeona baadhi ya vijana hao wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,  utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.

Chagua marafiki sahihi kwenye maisha yako.
Mpenzi msomaji wa makala haya naendelea tena juu ya somo hii la marafiki. Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo mazuri na kuwashirikisha marafiki zao, na marafiki hao wamekuwa wanazidi kuwakatisha tamaa tu.
Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako na kumwambia nataka kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki uliyenaye utamsikia akisema biashara hiyo hatatoka kwa sabubu fulani anaifanya au fulani kaliteka soko la biashara hiyo, hivyo hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya. Ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye.
Wapo baadhi ya marafiki ambo wao ukiwashirikisha jambo lako na wao huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata kidogo.
Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki sahihi ambao unahisi wewe wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke wanasema ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua marafiki wema. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.
Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia "always forward, backward never" ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko. Marafiki sahihi wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi kwa kile ulichowashirikisha na sababu za msingi.
Swali dogo la kujiuliza marafiki ulio nao ni wema au wabaya? kama ni wabaya unachukua jukumu gani baada ya kukupa somo hili?  ni muda wako mzuri wa kufikiri juu ya jambo hili na kuchukua uamuzi sahihi.
Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung'unike kutokana na magumu unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana mbele ya jamii.

Mwandishi: Afisa mipango na Maendeleo Benson Chonya
Mawasiliano
simu; 0757-909942

Apr 19, 2016

Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio Yako.

No comments :
Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndio kila kitu. Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndio ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujizalisha. Zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.
Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara  na majina mengine mengi.  Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.
Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuna mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mpango wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.
Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivyo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo la msingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mpangilio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.

Kuwa makini na mpangilio wa pesa.
Kukopa pesa hovyo.
Hili ndilo kosa kubwa ambalo linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!  madeni yanavyowatesa au yanavyokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.
Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja. Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unaunguna na wale wanaosema pesa ni shetani.
Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa. Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.
Mwandishi: Afisa mipango na Maendeleo Benson Chonya
Mawasiliano
simu; 0757- 90 99 42

Apr 18, 2016

Maswali Ya Kujiuliza Ili Kupata Mafanikio.

No comments :
Wakati mwingine hauhitaji nguvu nyingi katika kusaka mafanikio, ila unahitaji akili za kufikiri ili kuyapata hayo mafanikio. Ukishapata hayo mafanikio ndipo unapohitaji nguvu nyingi katika kufanya kazi. Inawezakana ukawa hajanielewa, ngoja nikueleweshe ni kwamba kila kitu kinaanza na kufikiri hapa ndipo wazo linapoanza kutengenezwa. Wazo hilo likishakamilika ndipo unapohitaji nguvu katika kufanya kazi.
Mpenzi msomaji wa makala hii siku ya leo  tutangalia katika kujua umuhimu wa kufikiri ili kupata mafanikio. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika ya kuwa watu wengi tumekuwa na maisha yaleyale ambayo yanatufanya tusisonge mbele kimafanikio hii ni kwa sababu tumekuwa tunafikiri mambo ya kawaida sana.
Mambo ambayo unahitaji kujiuliza ili kupata mafanikio.
1. Unataka kuwa na nani?
Hili ni swali la muhimu sana la kujiuliza uwe unayetaka mafanikio zaidi. Mfano wewe ni mwanafunzi wakati unasoma katika masomo yako je umewahi kujiuliza unataka kuwa na nani katika maisha yako ya hapo baadae? Pia na wewe mfanya biashara katika maisha yako umewahi kujiuliza unataka kuishi maisha gani? Je, biashara yako unataka iweje baada ya miaka kadhaa? Je, unataka kuwa hapo ulipo au unataka kuwa mfanyabishara mkubwa au mdogo?
Ukishajiuliza maswali hayo lazima ujiulize tena sifa hizo unazo au huna? na kama huna sifa hizo unazipata wapi? Ewe unayesoma makala haya shusha pumzi kisha twende sawa hebu jione upo  mahali baada ya muda fulani ndoto zako zimetimia. Kimsingi ni kwamba hayo yote yanakupa nafasi nzuri ya kujua malengo yako na kujua ni kitu gani ambacho unakihitaji katika maisha yako.

Jiulize maswali ya msingi ili kufanikiwa.
2. Unataka kutatua matatizo yapi?
Kwenye kutatua matatizo ndipo pesa zilipo. Unashangaa wala usishangae pia haujakosea kusoma. Ulimwengu wa leo ni ulimwengu wenye matatizo mengi ambayo yanahitaji majibu na mtoa majibu ni wewe. Unatoa macho ndio wewe ndiye mtoa majibu ya changamoto zinazowakabili watu. Badilisha mkao uliokaa kisha tuendelee, aliyegundua facebook leo hii katatua tatizo la watu na kutukutanisha watu pamoja na kuifanya dunia kuwa kinganjani mwako na tunafurahia maisha hayo, mtu huyo leo ni miongoni mwa watu matajiri ulimwenguni kwa sababu aliweza kusoma mazingira na kuona watu tuna changamoto yeye akaja na changamoto.
Kutatua changamoto za watu hauhitaji mifano kutoka kwa wazungu ila kila jambo unalotaka kulifanya kumbuka liwe linatoa majibu ya changamoto ya watu. Wewe unayefanya biashara ya kuuza chipsi endelea na kazi hiyo maana unasaidia unatatua tatizo la njaa kwa haraka zaidi, kitu cha msingi ongeza ubunifu katika kazi yako ili kuongeza wateja wengi zaidi. Huo ni mfano tu ila kumbuka kutatutua matatizo ya watu ili kupata pesa.
Hadi kufikia hapo afisa sina la ziada, kitu cha msingi na cha kukumbuka ni kwamba endelea kufuatilia makala za kimafanikio ili uweze kufanikiwa zaidi.
Imeandikwa na : Afisa mipango na maendeleo  Mr. Benson chonya
Simu: 0757-909942

Apr 15, 2016

Mambo Yanayokufanya Ukose Furaha Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu kinalenga kupata furaha ya kweli. Tunatafuta pesa, tunajenga nyumba nzuri, tunanunua gari nzuri, tunaoa au kuolewa na wachumba wazuri kwa sababu ya furaha.
Furaha ya kweli inapokosekana katika maisha, kwa wengi kunakuwa hakuna maana ya kuishi tena ndio maana umeshawahi kusikia kuna wengine wamejiua lakini hiyo yote baada ya kuona furaha halisi wanaikosa kwenye maisha yao.
Lakini kwa mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, pamoja na binadamu kuisaka furaha hiyo usiku na mchana lakini kuna wakati furaha hiyo huwa inakosekana kutokana na mambo mabalimbali yanajitokeza.
Ili kuijenga furaha hiyo tena na kwa muda mrefu kitu cha kufanya kwanza ni lazima ujue mambo hayo yanayoweza kukupotezea furaha.
Kwa kusoma makala haya utajua mambo ya msingi yanayokupotezea furaha kwenye maisha yako.

1. Watu wanaokurudisha nyuma.
Mara nyingi ni vigumu sana kukubali ukweli wa mambo hasa kama kuna watu wanaokuumiza. Watu hawa watakuumiza moyo na kuiona dunia yote chungu kwako.
Nini cha kufanya?
Kitu kimojawapo cha kufanya ili usiendelee kuumia acha kuwaweka watu hao kichwani mwako. Kama kuna sehemu walikurudisha nyuma basi hiyo imeisha, wafute kichwani mwako na anza maisha mapya.
Kumbuka, maisha yako unaweza ukayafanya upya na kuwa bora tena.


Toa mawazo hasi akilini mwako, uishi maisha ya furaha.
2. Mawazo hasi.
Kuwa na mawazo hasi kila wakati hukufanya ujione hufai na isitoshe unaweza kukonda kabisa.
Unapokuwa na mawazo hasi yanakufanya ujione wakati mwingine unashindwa kwenye karibu kwenye kila jambo.
Nini cha kufanya?
Toa mawazo yako hasi yaliyo kwenye kichwa chako. Muda wote jione mshindi na beba vitu vya kukusaidia ikiwemo pamoja na kujisomea vitu chanya.

3. Kujishusha sana.
Kujikosoa, kujishusha na kujitilia shaka, ni mambo ambayo yanaweza kukuumiza sana na kukukosesha furaha kama utaendelea na kujikosoa huko.
Kitu gani kinachotokea? Kwa mfano unapojikosoa unakuwa tena huwezi kufanya kitu chochote cha kukusaidia. Kwa sababu kila unachotaka kufanya umeshajiwekea mipaka tayari.
Nini cha kufanya?
Tambua maeneo bora kwako na yafanyie kazi. Pia jipongeze kwa mafanikio madogo uliyowahi kupata na weka malengo tena ya kukufanikisha.

4. Kuchukulia mambo kwa ujumla.
Kama kuna mtu amekufanyia kitu kibaya au hajakufanyia kama ulivyotaka, usichukulie kama mtu huyo ndivyo alivyo na ukaanza kuumia.
Chochote kinachokutokea kwenye maisha yako kiwe kizuri au kibaya usikichukulie kwa ujumla wake. Fikiri mara mbili kwanza kabla hujajitolea hukumu,  vinginevyo utaumia sana.
Nini cha kufanya?
Jifunze kuona mambo yanavyokwenda kwa uhalisia wake. Na usichukulie kwa ujumla sana. Hiyo itakusaidia kujenga furaha ya muda mrefu.

5. Kujiwekea kumbukumbu mbaya kwenye akili yako.
Chanzo kingine cha kukufanya uzidi kukosa furaha ni kuendelea kujiwekea kumbukumbu mbaya zilizotokea hasa kwa kipindi cha nyuma.
Kama kuna jambo baya lilikutokea kipindi cha nyuma liache kama lilivyo, lakini kwa kuling’ang’ania litakusababishia kuendelea kukosa furaha kwenye maisha yako.
Huna haja ya kuweka kumbukumbu sana na mambo yanayokuumiza akili mwako kwa muda mrefu.
Nini cha kufanya?
Kuanzia sasa jaza ubongo wako mambo mapya ili kutoa mambo ya zamani ambayo yameujaza ubongo wako kwa muda mrefu na yanakuumiza. Kwa kujaza ubongo wako utajenga furaha upya ya maisha yako.

Endelea kujifunza kupitia DIRA YAMAFANIKIO kila siku.  Ni wako rafiki Imani Ngwangwalu. Mawasiliano +255 713 048 035.



Apr 14, 2016

Maadui Wakubwa Wa Mafanikio Walio Ndani Yako.

No comments :
Wengi kulingana na uzoefu tumezoea kuona maadui wengi wa mafanikio yetu walio nje yetu. Mara nyingi tunakuwa hatuko tayari kukubali kuwa rafiki na mtu ambaye kwa namna moja au nyingine tumetambua ya kwamba yeye ni kikwazo au adui wa mafanikio yetu, naamini hili unalijua vizuri. Kwa hilo huwa tupo tayari kumweka kando mtu huyo kwa sababu ni  chanzo cha kutufanya tushindwe kufanikiwa.
Hata hivyo pamoja na kuwa makini na wale tunaomini ndio maadui wa mafanikio yetu, tumekuwa tukisahau kwamba wapo baadhi  ya maadui wakubwa wa mafanikio ambao wako ndani yetu. Kwa bahati mbaya sana maadui hawa tumekuwa hatupo makini nao sana lakini ndio wamekuwa wakituzuia kufanikiwa kuliko hata wale maadui wa nje tunaowajua. Je, unajua hawa ni maadui wapi ulionao na wanakufaya ushindwe kufanikiwa?
1. Woga.
Kati ya kitu ambacho kinamsumbua sana binadamu ni pamoja na woga. Binadamu kwa kawaida kimaumbile ni mtu wa kuogopa mambo mengi sana ikiwemo hata woga wa mafanikio yake. Woga huu mara nyingi hupatikana kutokana na kujifunza, uzoefu au kusikia lakini ukija kuungalia hata kile kinachoogopwa kinakuwa sio halisi ama kwa lugha nyingine tunaweza kusema hakipo.
Inapofika mahali ukawa una woga mkubwa ndani yako suala la kufanikiwa katika maisha linakuwa ni gumu. Hiyo yote inakuwa ni kwa sababu hakuna hatua ambayo utaweza kuichukua zaidi ya wewe kuogopa na kujihisi hutaweza. Kwa hiyo kama unaendekeza woga, tambua huyo ni adui mkubwa sana aliye ndani yako ambaye anakuzuia kufanikiwa. Waangalie watu wengi waoga maisha yao huwa ni ya kushindwa sana karibu siku zote.

Toa woga, utatengeneza mafanikio makubwa.
2. Wasiwasi.
Tukiachana na suala la woga pia adui mwingine ambaye binadamu anambeba ndani yake ni wasiwasi. Watu wengi wanakuwa ni watu wa kutilia wasiwasi au mashaka kwa mambo wanayoyafanya au wanayotaka kuyafanya. Utakuta mtu anataka kufanya kitu fulani lakini ndani yake kunakuwa kuna maswali mengi sana ndani yake anayojiuliza kama ‘hivi kweli hapa nitafanikiwa’ na je ikitokea nimeshindwa itakuwaje?’.
Kwa wasiwasi huu mwingi ambao wengi wanakuwa nao unakuwa unawafanya kushindwa kufanikiwa. Utakuta kweli mtu huyu amefanikiwa kuushinda woga na kujaribu kuchukua hatua. Lakini, kitendo cha kuthubutu huku ukiwa na wasiwasi mkubwa ndani yako wa ‘sijui nitafanikiwa au nitashindwa, huwafanya kushindwa moja kwa moja. Na hii huwa inatokea kwa sababu ya mawazo ya kina yanakuwa yanaamini kile unachokihofia ndicho unachokitaka mwisho wa siku unajikuta umeshindwa.
 3. Imani potofu.
Maisha yote ya mafanikio yanaongozwa na imani. Unaweza ukawa una mipango na malengo mazuri kabisa ya kukusaidia kufanikiwa, lakini kitu cha kujiuliza je una imani inayokusaidia kufikia mafanikio hayo? bila kuwa na imani sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio ni rahisi kushindwa. Watu wengi wanakuwa wanatafuta mafanikio lakini huku ndani mwao wakiwa na imani hasi, imani potofu ambazo zinawazuia kufanikiwa.
Kwa mfano utakuta mtu anatafuta mafanikio lakini wakati huo huo ndani yake anaamini watu wanaofanikiwa ni wezi, mafisadi au wanyonyaji kwa wengine. Kwa imani kama hizi kufanikiwa inakuwa ni ngumu kwa sababu ndani yako unakuwa na imani potofu inayokuzuia kufanikiwa huko. Ni lazima kujenga mtazamo chanya ambao utakupa mafanikio. Acha kuwaza hasi ama kujenga imani potofu utakwama kufikia mafanikio yako makubwa.
4. Maamuzi mabovu.
Kila mtu katika maisha yake ana maamuzi ya aina fulani ambayo anayatoa kila siku. Kwa maaumuzi hayohayo hupelekea maisha yako kuwa mabaya au mazuri. Kama ndani yako unabeba maamuzi mabaya kila wakati basi elewa una adui mkubwa anayekuzuia kufanikiwa. Kwani kwa kuwa na maamuzi hayo itasababisha maisha yako kuwa mabovu na ya ajabu sana.
Kwa mfano maisha yako yapo hivyo kwa sababu ya maamuzi ambayo ulishayafanya siku za nyuma. Kama ulifanya maamuzi mabovu ndivyo na maisha yako yalivyo sasa. Kuwa na maamuzi mabovu ni adui mkubwa sana aliye ndani yako ambapo usipokuwa makini anaharibu sana maisha yako pasipo wewe kujua. Kitu cha msingi kwako ni kuwa makini na kujifunza kuwa na maamuzi sahihi. Kinyume cha hapo utapotea.
5. Hamasa.
Ili ufanikiwe ni lazima uwe na hamasa kubwa sana ndani yako kila siku. Bila kuwa na hamasa hakuna mafanikio utakayoweza kuyafikia. Kwa bahati mbaya au nzuri hamasa huwa zinaanzia ndani mwetu. Kama ikitokea umekosa hamasa pole pole unakuwa umebeba adui wa kukuangusha bila kujijua. Kwa hiyo unahitaji kujijengea hamasa ili uweze kufikia mafanikio yako kwa kiasi kikbwa siku hadi siku.
Kwa vyovyote vile, ni lazima kupambana na maadui hao walio ndani yetu ili kufikia mafanikio makubwa. Chukua hatua mapema za kubadili maisha yako.
Nakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,
E-mail;- dirayamafanikio@gmail.com
Blog;- dirayamafanikio.blogspot.com

Apr 13, 2016

Tabia Zinazokuzuia Ushindwe Kupata Pesa Kwa Kiasi Kikubwa.

No comments :
Katika safari ya maisha ya mafanikio, kitendo cha kutengeneza pesa nyingi ni kitu au hatua ambayo kila mtu anataka aifikie. Bila shaka utakubaliana nami hakuna mtu ambaye haitaki pesa, kila mtu kuamka hadi kulala kwake shughuli zake nyingi karibu zote zinahusisha juu ya kupata pesa. Hiyo yote inaonyesha pesa inahitajika kwa namna yoyote ile kwa wingi na tena kwa kila mtu.
Lakini hata hivyo pamoja na kiu yote hiyo ya kutaka kuwa na mafanikio makubwa ya kifedha wengi wetu bado huwa hawafanikiwi. Unajua ni kwa nini? Ngoja nikwambie. Kwa kawaida huwa yapo mambo mengi yanayomfanya mtu huyu apate pesa nyingi na mwingine akose. Lakini leo hii nataka nikupe siri na kukwambia jambo moja tu linakufanya ushindwe kutengeneza pesa ya kutosha. Jambo hilo si lingine ni tabia.
Ndio. Nimesema ni tabia. Zipo tabia ambazo ukiwa nazo ni lazima zitakufanya ushindwe kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa. Ni tabia ambazo wengi tunazo na ni kweli zinaturudisha nyuma kwa kiasi kikubwa. Kwa kusoma makala haya, utajifunza tabia hizo ambazo zimekuwa kama kizuizi kwako na kukukufanya ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa. Karibu na twende pamoja kujifunza.
1. Tabia ya kushindwa kuifanya pesa ikuzalishie.
Kati ya kitu ambacho kinakuzuia ushindwe kutengeneza pesa nyingi, ni kule kushindwa  kuifanya pesa unayoipata ikuzalishie zaidi. Kwa mfano kama unapata shilingi laki tano kwa mwezi je, unaifanya vipi hiyo pesa ikaongezeka zaidi ya hapo? Kama unashindwa kuifanya hiyo pesa ikuzalishie zaidi, basi elewa hiyo ni moja ya tabia inayokufanya ushindwe kupata pesa kwa kiasi kikubwa.
Kitu cha kufanya kama hilo ndilo linalokuzuia, tafuta ni wapi au eneo lipi unaweza kuwekeza kwa pesa unayoipata. Ukishapata kitu hicho acha kupoteza muda kwa kujiuliza uliza na anza mara moja kutengeneza pesa kwa kuiweka kwenye uwekezaji. Kwa kujijengea tabia hiyo kutakufanya uzidi kutengeneza pesa za ziada. Jambo la msingi na la kukumbuka ifanye pesa yako ikuzalishie zaidi hata kama ni kiasi kidogo unapata

TOA THAMANI UTENGENEZE PESA ZA KUTOSHA.
2. Tabia ya kushindwa kutoa thamani.
Ni rahisi kushindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa kama pia utashindwa kutoa thamani kwa kile unachokitaka. Mara nyingi mafanikio yoyote yanaanza kwa kutoa thamani uliyonayo ndani mwako kwanza. Kwa mfano hapo ulipo kuna kiasi fulani cha pesa unachokipata kwa mwezi. Kiasi hicho cha pesa hakiji hivi hivi bali kuna thamani au kitu unachokitoa ndani mwako kinachopelekea upate pesa hiyo.
Kama tafsiri yake  iko hivyo, hiyo inamaanisha kwamba kama unashindwa kutoa thamani kubwa maana yake utashindwa kutengeneza pesa nyingi. Wengi  kutokana na kuishi kwa mazoea wamejikuta wakiwa ni watu wa kuishi maisha yale yale bila kutoa thamani kubwa sana. Kwa kufanya hivyo hujikuta ni watu wa kushindwa kutengeneza pesa nyingi karibu muda wote wa maisha yao.
3.Tabia ya kufanya mambo kwa ukawaida sana.
Sumu kubwa ya kufikia mafanikio makubwa na kushindwa kutengeneza pesa kwa kiasi kikubwa ni kufanya kazi kwa ukawaida sana, Watu wengi wana mazoea ya kufanya kazi kwa viwango vya kawaida. Ili uweze kufanikiwa na kutengeeza pesa nyingi maishani mwako, jifunze kufanya kazi kwa bidii zote bila kuchoka. Kwa kadri utakavyozidi kuongeza juhudi katika kafanya kazi kwa bidii itakufanya uzidi kutengeneza mpato makubwa sana.
Kama unafikiria natania, angalia watu ambao maisha yao yote wameyaweka kwenye kujituma huku wakiwa wamekubali kujifunza. Watu hawa mara nyingi wanatengeneza pesa nyingi sana kutokana na kile wanachokifanya kwa juhudi zote. Kwa hiyo  moja ya kitu kinachokufanya ushindwe  kutengeneza pesa nyingi sio mkosi au laana kama unavyofikiri bali ni kufanya kazi kwako kwa ukawaida. Jitume mara kumi ya hapo tuone ni nini kitakutokea kwenye maisha yako.
4. Tabia ya kuridhika mapema.
Kuna watu wana tabia hasa pale wanapopata mafanikio madogo tu, huwa ni watu wa kuridhika sana. Huwa ni watu wa kujiona wamefika na hata zile juhudi kubwa walizokuwa nazo mwanzo zinakuwa zinapotea kidogo kidogo kwa sababu ya mafanikio hayo. Unapokuwa na na tabia kama hii tambua kabisa hicho ni chanzo kikubwa sana kinachokufanya  ushindwe kutengeneza pesa nyingi.
Kwa mfano jaribu kuangalia baadhi ya wasomi wetu, akijenga nyumba na kununua gari kwao ndio basi. Maisha huwa kama yameishia hapo na hakuna juhudi kubwa tena wanayokuwa wanaifanya. Kitu cha kuelewa mafanikio sio nyumba wala gari peke yae. Tunatakiwa kufanya mambo makubwa zaidi ya hapo. Kama mafanikio ni nyumba tu sasa jambo la kujiuliza ni nani ayeishi kwenye tundu kama ndege, bila shaka hakuna. Hivyo acha kuridhika, ili utengeneze pesa za kutosha.
Kimsingi zipo tabia nyingi ambazo zinaweza zikakuzuia wewe ukashindwa kupata pesa kwa kiasi kikubwa na kukufanya usifikie mafanikio mkubwa. Lakini kwa kupitia makala haya hizo ni baadhi tu ya tabia hizo.
Ansante kwa kuwa msomaji mzuri wa DIRA YA MAFANIKIO lakini washirikishe wengine waendelee kujifunza kila siku kupitia mtandao huu.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu;- 0713 04 80 35,

Apr 12, 2016

Unaweza Kubadilisha Maisha Yako Kabisa Ukiamua Na Kufanya Hivi.

No comments :
Moja kati ya kosa kubwa ambalo watu wengi wanafanya katika maisha yao ni kule kuamini kwamba hawawezi kufanya mambo fulani na badala yake uwezo huo wamewaachia watu wengine. Kwa mfano utakuta mtu anakwambia hawezi kufanikiwa kwa viwango vya hali juu sana kwa sababu hana uwezo huo lakini ingawa kiuhalisia sio kweli.
Chochote unachokitaka katika maisha yako, unaweza kukipata ikiwa utauamini uwezo mkubwa ulio ndani yako. Una uwezo mkubwa sana ndani yako usioelezeka ambao ukiutumia unaweza kukupa chochote ukitakacho kama tu utachukua hatua. Lakini kama utaendelea kuamini huwezi kufanikiwa ni wazi kabisa hutaweza kufanikiwa. Utapata kile unachokiamini akilini mwako.
Jiulize kama kuna watu wengine wanaweza kufanikiwa kwa nini wewe ushindwe kufanikiwa? Wanaofanikiwa kumbuka ni watu wa kawaida wenye macho, miguu, nywele, akili na kila kitu sawa na wewe. Kitu ambacho pengine wamekuzidi ni maamuzi  na kiu ya kufanikiwa kwao. Kama ni hivyo fanya uamuzi sahihi wa kufanikiwa.
Kama fulani aliweza kufanikiwa na wewe unaweza pia kufanikiwa ukiamua.
Kama Oscar Pistorius mwanariadha mlemavu aliweza kufanya hivyo na kufanikiwa wewe pia unaweza kufanikiwa kwa hali yoyote uliyonayo.
Kama Ben Carson mwandishi wa vitabu aliweza kufanikiwa akitokea kwenye mazingira magumu ya kimaskini  na wewe unaweza.

TUMIA AKILI YAKO  VIZURI KUKUFANIKISHA.
Kama Aliko Dangote aliweza kufanikiwa na kufikia viwango vya juu vya utajiri duniani pia na wewe unaweza kufanikiwa.
Kama Nick Vujicic akiwa kwenye hali yake ya ulemavu ameweza kufanikiwa na wewe una uwezo huo wa kufanikiwa.
Una kila kitu na uwezo mkubwa wa kufanikisha kila unachokihitaji katika maisha yako.
Kuwa makini sana…usijishushe wala kujiangalia hasi hasi yaani kujiangalia hufai au kwamba huwezi kufanikiwa. Ipo nafasi kubwa ya kufanikiwa kwako tena. Hakuna kinachoshindikana ikiwa utaamua kuifungua akili yako na kubadilika.
Kama kuna sehemu umeanguka amua kuamka tena  na wala usikate tamaa. Rekebisha makosa yako, jifunze kwa wengine na songa mbele. Ishi kwa ndoto zako kila siku na jione kama msindi kwa kile unachokiendea.
Tambua mabadiliko yote unayoyataka kwenye maisha yanaanza na akili yako kwanza. Kile unachokifikiri na kukibeba sana kwenye akili yako mara kwa mara ndicho kinachotoa hatma ya maisha yako.
Kama ulikuwa unafikiri umechelewa kufanya mabadiliko katika maisha yako, haujachelewa. Anza kufanya mabadiliko kwenye akili yako kwanza kila siku baada ya muda utabadili kila kitu kwenye maisha yako na hakuna kitu cha kukushinda.
Kumbuka kama wengine wanaweza na wewe unaweza kufanikiwa pia.
Unao uwezo wa kuwa mtu wa tofauti.
Unao uwezo wa kufanikiwa.
Unao uwezo mkubwa wa kuwa nyota wa maisha yako.
Hakika unaweza, ikiwa utachukua hatua na kukubali kujifunza.
Ansante kwa kusoma makala haya na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,