Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, September 7, 2016

Namna Ya Kukiendeleza Kipaji Chako.

No comments :
Siku kaadha zilizopita kama utakuwa ni mfuatiliaji wa safu hii nilieleza kwa kina namna ya kugundua kipaji chako, hivyo naomba nifanye mwendelezo wa maada hiyo kwa kueleza ni jinsi gani ya kuendeleza kipaji chako ili kisife maana watu wengi hufa na vipaji vyao.

Kama ambavyo nilieza ya kwamba kipaji ni uwezo ambao mtu huzaliwa nao (talanta). Talanta hiyo imegawanyika katika makundi mbalimbali na kumfanya mtu aweze kufikiri, kubuni, kuvumbua au kusanifu kitu fulani, vilevile kipaji huusisha kwa asilimia kubwa na viungo vya mwili katika kufanya jambo fulani kama vile ufundi, kucheza na vitu vingine vingi.

Pia watu wengi hujiuliza kipi kinaanza kati ya ndoto na kipaji? Ukweli ni kwamba kipaji huanza kisha ndoto kufuata. Kwa mfano leo unaweza ukawa una kipaji cha kucheza  mpira lakini ndoto yako ni kuwa mchezaji mkubwa wa mpira afrika mashariki na kati.

Pia ikumbukwe ya kwamba kipaji huwa hawasomei maana ni uwezo ambao mtu huzaliwa nao mtu, hivyo elimu hutumika kama nyenzo ya kukuza na kupalilia kipaji hicho.

Zifuatazo ndizo mbinu za kukuza kipaji chako.

1.Tafakari kila unachokiona na kusikiliza.

Hii ni mbinu bora sana katika suala la ukuzaji wa kipaji chako kwa sababu ulimwengu wa leo una vitu vingi hivyo ni lazima ujue ni vitu gani ambavyo unapenda kusikiliza na kukiona zaidi na kuachana na vitu ambavyo havikusaidii.


Kwa mfano, kama leo unataka kuwa muigizaji bora wa filamu ni lazima mara kwa mara upende kutazama filamu za watu mbalimbali pia ni lazima masikio yako yawe tayari kusikiliza mambo yote ya muhimu yahusuyo masuala ya filamu.

Vivyo hivyo kwa kuutazama mfano huo ni lazima ujue ni kipi kwako ni cha muhimu katika kukupa taarifa sahihi katika ukuzaji wa kipaji chako.

2. Tafuta mtu wa kukuongoza.

Hili ni tatizo kubwa sana kwa watu wengi, watu wengi wana vipaji ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuibadili jamii na maisha yake kwa kiwango kikubwa, lakini changamoto kubwa ambayo inawakabili watu hao ni kwamba hawana mtu sahihi ambaye ana husika kwa asilimia kubwa katika kumuongoza katika tasnia ambayo anayoifanya.

Watu wengi wanapenda kukomaa peke yao katika vipaji vyao na mwisho wa siku vipaji hivyo hufa.

Inawezekana ukawa unadhani nazungumzia mtu ambaye anakuvutia ambaye mnafanana kipaji, la hasha mimi nazungumzia mtu ambaye atakupa ‘network’ ya kukuza kipaji na hatimaye kutengeneza pesa.

Siku zote ukumbuke unahitaji mtu sahihi wa kukuongoza na kukisimamia kipaji chako ili uweze kutimiza ndoto zako, hiyo ni ya muhimu sana kuliko neno lenyewe.

3. Jiunge katika vikundi mbalimbali.

Ili uweze kuwa bora zaidi katika kipaji chako huna budi kujiunga katika vikundi mbalimbali ambavyo vinajihusisha na vitu ambavyo vinalandana na kipaji chako.

Kwa mfano, unapenda kuwa mwanamziki bora ni lazima ufuatane na watu wenye vipaji vya mziki kwani kufanya hivyo ni kujifunza mengi kutoka kwao, pia ukumbuke ule usemi kutoka kwa wahenga wetu ambao husema penye wengi pana mengi.

4. Hudhuria semina.

Kama una amini katika kujifunza, bali endelea kujifunza kwa kuwa karibu na watu ambao huendesha semina ambazo zinaendana kwa asilimia kubwa na kipaji chako.

Kufanya hivi kutakupa hamasa na ufanisi wa kiutendaji ili kuhakikisha ya kwamba ndoto ya kipaji chako inakwenda kuwa kweli baada ya muda mfupi hasa pale ambapo utachukua jukumu ya yale uliyojifunza kuyaweka katika matendo.

5. Kujifunza vitu vipya.

Kujifunza vitu vipya ndipo ambapo siri ya mafanikio kila mmoja wetu ilipo, nimesema kujifunza vitu vipya kila kwa sababu ulimwengu wa sasa kila siku kuna uvumbuzi wa vitu mbalimbali kila itwatayo leo hivyo fanya makusudio ya dhati kuweza kujifunza. 

Hivyo wito wangu kwako ni uwe karibu sana na vyombo mbalimbali ambavyo vitakupa taarifa sahihi hususani suala zima la  jinsi gani utaweza kukuza kipaji chako na hatimaye kupata pesa.

Dunia ni pana, ila ina maneno machache naomba kwa leo niishie hapo tukutane katika makala iyayo, pia usisite kumshirikisha mwingine kama ambayo mimi nimeamua kufanya kwako.

Endelea kujifunza zaidi kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa kujifunza.

Ndimi: Afisa Mipango Benson Chonya.
0757-909942.

No comments :

Post a Comment