google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 10, 2017

Mambo Mawili Muhimu Kwa Mjasiriamali Wa Sasa.

No comments :
Asilimia kubwa ya watu wengi wanaoanza biashara zao, hujikuta wakishindwa mapema hata kabla ya kuanza kufaidi yale matunda ya biashara zao vizuri. 
Yapo mambo mengi yanayosababisha hali hiyo kutokea ikiwa ni pamoja na hali ya kiushindani katika biashara, ukosefu wa elimu ya kutosha hasa juu ya  kuendesha kibiashara na mambo mengine madogo madogo.
Lakini hata hivyo hali hiyo pia ya kushindwa katika biashara mapema bila shaka inatuonyesha au inatupa picha kwamba hali ya ufanyaji wa  biashara ya sasa hivi sio sawa na ile ya zamani.
Katika dunia ya sasa ili upate faida nzuri kwenye biashara yako hakuna tena ule ufanyaji wa biashara wa kimazoea ambao utakupa faida moja kwa moja. Ni lazima ufanye kazi ya ziada.
Kwa mfano leo hii, ukianzisha biashara sehemu fulani, usishangae kesho ukaikuta mtaa wa pili au mkajikuta watu zaidi ya kumi mna biashara ya aina moja katika mtaa mmoja.

Itumie mitandao ya kijamii vizuri ili ikusaidie uwe mshindi katika biashara.
Sasa haya ni moja ya mambo yanayomfanya mjasiriamali mdogo kuweza kushindwa mapema hata kabla ya kufaidi matunda ya biashara yake na kujikuta ameacha.
Inawezekana kuna kitu unajiuliza ,ni kitu gani ambacho kinachotakiwa kifanyike? Ni kweli kabisa upo ulazima wa kila mjasiriamali wa leo kuweza kubadilika na kufanya biashara kwa kisasa ili kukabiliana na kila hali ya ushindani.
Nina sema upo ulazima wa kubadilika nikiwa na maana kwamba bila kufanya hivyo, suala la kushindwa katika biashara litakuwa ni la wazi kabisa na hutaweza kufanikiwa na kufika mbali sana kimafanikio.
Leo hii kupitia makala yetu haya nataka nikushirikishe mambo mawili ambayo ambayo ni ya lazima sana kwa mjasiarimali wa sasa au mjasirimali wa ‘digital’ ili kuweza kufikia mafanikio makubwa.
Jambo la kwanza ni tovuti/’website’,  kwa mjasirimali wa kileo ni muhimu sana kutengeneza tovuti yako au blogu ambayo inakuwa inawafikia watu wengi na kukusaidia kutangaza bishara zako moja kwa moja.
Kama unaona kufungua tovuti au ‘website’ ni gharama hilo halina shida sana unaweza ukaanza hata na blogu. Kupitia huko kwenye tovuti ni rahisi sana kuwapata wateja wengi ambao wako mbali na wewe.
Haijalishi sana ni kitu gani ambacho unauza lakini ni muhimu sana kutengeneza tovuti kwani ndiyo dunia ya sasa iliko na inataka mabadiliko kama hayo, hivyo ni muhimu sana kuwa nayo.
Mwanzoni inaweza isifahamike lakini siku zinavyozidi kwenda itajulikana na kuwa sehemu yako ya kukuzia na kuuzia bidhaa zako muhimu. Lichunguze hili na lifanyie kazi mara moja.
Jambo la pili la mjasiariamali wa sasa ni kutumia mitandao ya kijamii kwa faida. Mbali na mitandao ya kijamii kutumika kama 'kuchati' lakini inaweza ikakuingizia pato kubwa kama utaitumia kwa faida.
Ni muhimu sana kuitumia mitandao ya kijamii pia kutangaza biashara zako maeneo tofauti tofati. Kwa mfano unaweza ukafungua ukurasa wa ‘facebook’ ambao unahusiana na biashara zako tu ambazo unazozifanya.
Pia kupitia ukurasa wako unaweza ukaweka matangazo na bidhaa zako hapo kwa hali hiyo ni lazima utajikuta unazidi kukuza biashara yako pole pole kadri siku zinavyozidi kwenda.
Kama nilivyoanza katika makala haya ni muhimu sana kwa mjasirimali wa sasa, kutumia na kutawala mambo hayo mawili yaani tovuti na mitandao ya kijamii ili kufanikiwa kwa viwango.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.