Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, January 11, 2017

Jifunze Mambo Haya Muhimu Ya Mafanikio Yakupe Nguvu Ya Kufanikiwa.

No comments :
1. Kama unataka kufanya mabadiliko madogo katika maisha yako ni vyema ukaanza kubadili tabia zako. Ila kama unataka kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako, anza kubadili imani uliyonayo juu ya mafanikio. Hapo ndipo mabadiliko makubwa yanapoanzia.
Watu wengi sana wanajaribu kuanza kubadili tabia zao kabla hawajabadili imani waliyonayo juu ya mafanikio. Kubadili tabia peke yake hakutakusaidia sana ni lazima kubadili tabia  kuambatane na kubadili imani ulionayo juu ya mafanikio, hapo utaona unafanikiwa sana.
2. Watu wengi katika maisha wanavuta mambo yale sio wanayoyataka, bali ni watu wa kuvuta mambo kama vile jinsi wao walivyo. Picha iliyo kwenye mawazo yako ndio inayokupa hicho unachokitaka katika maisha yako na sio kinyume cha hapo.
Kama unawaza mafanikio muda mrefu, ni wazi utayapata mafanikio hayo bila shida yoyote. Kama unawaza kushindwa, ni wazi utashindwa sana katika maisha mpaka utabaki unashangaa.
Jenga picha sahihi ya kile unachokitaka kwenye mawazo yako na utafanikiwa. Ukiwa huna picha sahihi ya unataka nini maishani mwako utaishia kushindwa na maisha yako yatakuwa mabaya kila wakati.

3. Acha kuuchanganya ubongo wako kwa kuupa vitu ambavyo huvihitaji. Kwa lugha  rahisi waza vitu ambavyo unavihitaji katika maisha yako. Tofauti na hapo utakuwa unajichanganya sana kwa kuufanya ubongo wako ushindwe kuelewa kipi unachokitaka na kipi hukitaki.
Unataka mafanikio tulia, tambua ni kipi unachokitaka na ukifanyie kazi hicho kila siku. Ila ukiwa ni mtu wa tamaa mara unataka hiki mara kile  itakupelekea kupata matokeo ambayo siyo sahihi katika maisha yako na usishangae ukishindwa kufanikishakaribu kila kitu. kumbuka kila wakati Contradicting desires create contradicting results.
4.  Mafanikio makubwa sana utayapata kama unafanya kitu ambacho unakipenda sana toka moyoni. Ikiwa hukipendi kile unchokifanya yaani unakifanya kitu hicho kwa kujilazimisha uwe na uhakika, hutafanikiwa sana.
Hivyo kila wakati pata muda wa kujiuliza je, ni kitu gani ambacho unakipenda? Kisha baada ya hapo kifanye kitu hicho kwa nguvu zote. Kumbuka siku zote mafanikio makubwa yanakuja kwa kufanya kile kitu unachokipenda.
5. Ni rahisi kufanikiwa na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako ikiwa utakuwa tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara nyingi watu wenye mkono wa ‘birika’ si rahisi sana kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.
Jiulize kitu gani ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa wengine? Kama kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako, washirikishe na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.
6. Kitu kibaya katika maisha yako ni kule kujishusha na kujiona ni mdogo kumbe wakati hata hauko hivyo. Wengi wanatabia ya kujishasha sana na kujiona ni kama wadudu kumbe ni wakubwa sana kuliko fikra zao hizo.
Hebu jiulize ni kwa nini unajishusha sana na kujiona hufai? Je, unafikiri kuna kitu ambacho umekikosa hadi ikapelekea ukajiona mnyonge kiasi hicho. Sikiliza hujaumbwa ili uwe mnyonge au uwe mdogo kama unavofikiri, wewe ni mtu tofauti sana.
Amini unaweza ukapata mafanikio mara kumi ya hapo ulipo sasa. Unashangaa, ndio unaweza kufanikiwa zaidi ya mara kumi ya hapo ulipo wala hutakiwi kujiwekea mipako. Kila kitu kinawezekana kwako ukiweka nia na kuamini, itakuwa.
7. Kila wakati jiulize ni kwa namna gani kupitia kile unachokifanya utakwenda kubadilisha maisha ya wengine na kuwafanya wawe watu wa mafanikio. Jitahidi kila siku uwe baraka kwa wengine. Weka juhudi si za kukusaidia wewe tu ila mpaka kuwasadia wengine pia.
Kwa hiyo unapotafuta pesa kumbuka zote sio zako, tenga angalau kidogo ambazo unaweza ukampa yule ambaye hajiwezi. Kama ambavyo nasema mara kwa mara, wakati mwingine mafanikio makubwa yanakuja kupitia utoaji wako. Je, unatoa kiasi gani kuwasaidia wenye uhitaji hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
8. Sumu kubwa sana inayowazuia wengi kuwa matajiri ni kung’ang’ania kila kitu kufanya wao. Kama upo hivyo huwezi kuwa tajiri kwa sababu unakuwa huna uwezo wa kutengeneza faida ya kutosha peke yake ni lazima uanhitaji msaada.
Ni jambo la muhimu sana kwa kila mjasiriamali kutengeneza mfumo ambao unakuwa unaingiza pesa hata kipindi ambacho wewe haupo moja kwa moja. Ukitengeneza mifumo kama hii ni rahisi kufikia utajiri.
Acha kuniambia habari ya kuibiwa. Kila biashara duniani ina ‘risk’ zake. Kikubwa jifunze ni kwa namna gani ambavyo unamudu kuweza kutawala hizo hali hatarishi, kuliko kukaa na kutaka kukumbatia kila kitu, hapo utakwama sana.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,

No comments :

Post a Comment