google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 30, 2017

Je, Bado Unalalamika Kwenye Biashara Yako?

No comments :
Mbona unalalamika kila siku kwamba biashara yako ni ngumu? Kwani wewe ulianzisha biashara yako kwa lengo gani? Malalamiko kutoka kwa wajasiriamali imekuwa ni sehemu ya Maisha yao.
 Kila unapojaribu kuongea na wajasiriamali lazima usikie malalamiko mengi ikiwemo ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara. Watu wanalalamika eti hawafikiriwi, hakuna anayewajali na hawasaidiwi!
 Yawezekana ni kweli, lakini kwa yeyote mwenye malalamiko na aketi chini na ajiulize hili; “Ndiyo hakuna anayenijali, hakuna anayenifikiria na hakuna anayenisaidia, kwahiyo…...” 
Ukishajiuliza swali la “kwahiyo…” –bila shaka utaamua mojawapo kati ya haya: ama ni kuacha kufanya biashara au kuendelea na biashara”. Endapo utaamua kuacha biashara kero na malalamiko yako yote vitakuwa vimeishia hapo na kimsingi utaweza kuendelea na maisha mengine. 

Endapo utachagua kuendelea na biashara, maana yake ni kwamba matatizo unayolalamikia si makubwa kiasi cha kukuzuia kupata faida na pengine ndiyo maana umechagua kuendelea na biashara bila kujali matatizo na changamoto zilizopo.
Utamaduni wa kulalamika juu ya kazi tunazozifanya tumeurithi kutoka kwa watumishi hasa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniani uko katika umbo la pembe tatu (piramidi). Ambapo unakuta mkubwa ni mmoja na chini yake kunakuwa na watu wengi kutegemea na ukubwa wa taasisi au kampuni husika iliyokuajiri. Mara nyingi watu walioko chini wakishindwa jambo lolote humsukumia yule aliyejuu ili afikiri na kutoa suruhisho kwaniaba ya wale wote anaowaongoza.

Kwa maana nyingine ni kwamba katika umbo hilo hapa juu, kuna mambo mengine huruhusiwi kuyafanya au kuyatolea maamuzi isipokuwa aliye juu yako. Pili, ukiwa mwajiriwa wa ngazi za chini kuna mambo ambayo yakikushinda unayapeleka kwa mkubwa wako kwa ajili ya ufumbuzi zaidi.

Kwahiyo, chimbuko la tabia ya kulalamika ni utaratibu wa kutegemea maamuzi ya aliye juu yako. Kama anayepaswa kuamua jambo fulani, hafanyi hivyo kwa wakati au akafanya maamuzi vibaya basi utakuta waajiriwa walioko chini wanafanyakazi kwa kunung’unika muda wote, wanalalamika muda wote wanasema hovyo muda wote na hasa wakiwa maeneo ya nje ya ofisi zao.

Ikumbukwe kuwa, kinachowapa waajiriwa uhalali wa kulalamika ni ule mfumo au utaratibu wa ajira duniani ambao unatoa nafasi kwa mwajiriwa kuweza kupeleka malalamiko yake ngazi za juu endapo ataona kuna mambo ambayo hayaendi sawa.

Katika mfumo mzima wa ajira “MKUU” ni mtu wa mwisho na hatutarajii halalamike kwasababu hakuna mtu mwingine aliye juu yake ambaye anatakiwa kumpelekea malalamiko, ingawaje wengine ujikuta nao wakilalamika kwa watu wa chini yao. Wewe kama ni “Mkuu” kazi yako ni kuamua na kutenda basi!

Unapoamua kuwa mjasiriamali au kuanzisha biashara ni kwamba wewe umejipa nafasi ya kuwa “MKUU”. Haijalishi biashara ni ndogo au ni kubwa kiasi gani bali wewe ni mkuu tu! Wewe ni kiongozi mkuu wa biashara unayoifanya, na pia wewe ni kiongozi mkuu wa maisha yako. 
Mafanikio ya biashara au mradi wako yanategemea sana maamuzi na kutenda. Kamwe tusiwaige waajiriwa, kwani wao wanayo sehemu ya kupeleka malalamiko—kwa viongozi wao au kwa wakuu wao katika utumishi. 
Sisi wajasiriamali ni tofauti na waajiriwa kwasababu hatufungwi na kitu chochote katika kuamua nini tufanye na nini tusifanye, ilimradi tu tunafuata sheria za nchi. 
Wajasiriamali tunao uhuru wa kurekebisha kile kinachotukera na kama ni kikubwa kiasi cha kutuletea hasara bado tunayo maamuzi ya kufunga biashara hiyo na tukaendelea na maisha mengine yanayotupa faraja.
Haipendezi hata kidogo mjasiriamali kulialia kila wakati. Wengi kilio chao ni kusaidiwa mtaji, kuonewa huruma, kubembelezwa n.k. sijui! lakini nionavyo mimi, hakuna atakayekufunga endapo utaamua kuacha ujasiriamali, badala yake wewe ndiye utapata hasara ukiacha au faida ukiendelea kufanya vizuri hicho unachofanya.
Eti unataka uwezeshwe na mtu ambaye shughuli zake tu zinategemea zaidi pesa unazomchangia kila mara, je hiyo inawezekanaje mtu huyo huyo akuwezeshe pesa?
Ndugu yangu umefika wakati sasa ujitambue na uache kulalamika kama waajiriwa. Kaa kimya huku ukizidi kufanya kazi zako zote kwa juhudi na maarifa. Pia, tekeleza majukumu yako kadiri ya uwezo wako wote. Jione kuwa wewe ni kiongozi mkuu na hakuna mtu mwingine mbele yako na hata juu yako.
Kuwa tayari kuwajibika kwa maamuzi na matendo yako unayofanya kila siku. Kila unapokabiliwa na changamoto usikimbilie kulia na kulalamika, usikimbilie kuacha bali ujiulize ni kwanini ulianzisha hiyo biashara unayofanya.
Pia, fikiria ni watu wangapi watafurahia kuona wewe unashindwa kufanikisha hicho unachokifanya. Ukitambua hili, nina hakika kuwa muda si mrefu utaanza kuona mafanikio yakianza kupatikana.
Endelea kujifunza kupitia hapa DIRA YA MAFANIKIO ili upate kufahamu mbinu za kujiongoza na siyo kulalamika kama waajiriwa.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA CYPRIDION MUSHONGI WA MAARIFA SHOP BLOG.

Apr 29, 2017

Kitu Chenye Nguvu Kubwa Kuliko Pesa Ni Hiki Hapa.

No comments :
Kwa wengi wetu si rahisi sana kuweza kuamini kwamba kipo kitu chenye thamani kubwa kuliko pesa. wengi huamini sana pesa ni kila kitu, kwamba ukiwa na pesa basi, ndio mambo yote yameishia hapo.
Lakini upo ukweli mwingine ambao pengine huujui. Mbali na thamani ya pesa yenyewe, malengo ni kitu ambacho kinathamani kubwa sana hata kuliko pesa yenyewe ,malengo ninayoyazungumza hapa ni malengo yanayofanyiwa kazi.
Kama una mashaka kidogo na hili, naomba uwangalie watu ambao kuna wakati wanaweza kupata pesa huku wakiwa hawana malengo ni kitu gani kinawatokea. Najua utagundua pesa zao zilipotea.
Unapokuwa una malengo hata upate pesa nyingi sana, si rahisi sana kupotea, tofauti na mtu ambaye anajiendea tu bila kuwa na malengo yoyote. Ni rahisi kuweza kufuata malengo yako na kufanikiwa.

Ipo nguvu kubwa sana kwenye kufuata malengo yako.
Kwa hiyo mpaka hapo unaona kwamba kitu ambacho kinaweza kuwa na thamani kubwa hata kuliko pesa ni malengo yenyewe. Hasa hili linakuja kutokana na nguvu ya malengo katika kupata pesa.
Pesa nyingi hazipo kwenye pesa yenyewe, pesa nyingi zipo kwa wale wanajiwekea malengo na kuamua kuyafuata kila inapoitwa leo. Kama una malengo imara na unayafuta pesa utapata tu.
Kwa vyovyote maisha yako yalivyo, kwa vyovyote na hali yoyote uliyonayo hata iwe mbaya vipi, hauwezi kutoka hapo na kufanikiwa hata upewe pesa nyingi. Pesa hizo utazipoteza usipokuwa na mikakati imara.
Kwa hiyo ili uweze kufanikiwa kipesa zaidi, hebu hakikisha una mipango imara, hakikisha una malengo yaliyo sahihi. Hapo utatengeneza pesa nyingi na kupata mafanikio.
Tunamalize makala hii kwa kusema kwamba, kitu kingine chenye nguvu kuliko hata ya pesa yenyewe ni  yale malengo unayojiwekea. Hicho ndicho kitu chenye nguvu kuliko malengo yenyewe.
Nikutakie siku njema na endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com

Apr 27, 2017

Mambo Kumi Ya Kuimarisha Maisha Yako.

No comments :
Maarifa ni msingi mkubwa wa mafanikio kwa jambo lolote lile. Ndio maana kwa kadri jinsi unavyozidi kuwa na maarifa bora na ndivyo maisha yako yanazidi kusimama na kuwa ya mafanikio makubwa.
Hivyo kwa mantiki hiyo ni muhimu sana kujifunza mambo yanayoimarisha maisha yako karibu kila siku. Hebu leo katika makala haya, twende pamoja tujifunze mambo kumi ya msingi yanayoweza kuimarisha maisha yako.
1. Washindi katika mafanikio hawafanyi sana mambo tofauti na unayofanya wewe bali wanafanya mambo hayo kwa UTOFAUTI.
2. Msingi mkubwa wa mafanikio unajengwa na mtazamo wako ulionao. Mtazamo ulionao ndio unaokufanya ufanikiwe au ushindwe katika jambo unalolifanya.
3. Mara nyingi fursa kubwa za mafanikio zinakuwa zipo miguuni petu au katika maeneo yanayotuzunguka. Acha kutumia muda mwingi  sana  kuangalia fursa zilizo mbali na wewe na kusahau pale ulipo.

Hapo ulipo pia kuna fursa, kuwa makini na eneo ulilopo kuangalia fursa zinazokuzunguka kufanikiwa. Unajua, ni rahisi sana kuona fursa zilizo upande mwingine na kusahau fursa ulizonazo karibu yako.
4. Fursa yoyote kubwa ikija kwako kama utaipoteza, sio rahisi fursa hiyo tena kuweza kujitokeza kwako kwa namna nyingine.  Kwa hiyo kama kuna fursa imejitokeza kwako na una uwezo nayo itumie kwa uhakika kukufanikisha.
5. Mtazamo wowote ulionao uwe chanya au hasi, unajengwa na mambo makubwa matatu, Mazingira yanayokuzunguka, uzoefu katika maisha na elimu. Hayo ndiyo mambo matatu yanayojenga mtazamo wako, Hakuna mtazamo unaojengwa nje ya  mambo hayo hapo.
6. Faida za MAWAZO CHANYA katika maisha yako.
      Kuongeza ufanisi na ubora katika kazi.
      Kuongeza faida kwa ukifanyacho.
   Kutatua changamoto nyingi kwa urahisi.
   Kupunguza msongo wa mawazo.
   Kudumisha mahusiano bora na ya wengine.
7. Hasara za MAWAZO HASI katika maisha yako.
   Msongo mkubwa wa mawazo.
   Kupoteza afya.
   Kuwa na hisia nyingi za maumivu.
    Maisha yako kukosa maana.
Pamoja na kwamba unajua hasara za mawazo hasi wengi wetu bado hawabadiliki unajua ni kwa nini? ni kwa sababu ni asili ya binadamu kukataa mabadiliko, hapo unahitaji nguvu nyingi ya kukutoa kwenye hali ya mazoea ili ufanikiwe kujenga mawazo chanya.
8. Hauhitaji elimu kubwa sana ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu bora ambayo unaihitaji au  unatakiwa uipate ni elimu ya kubadilisha maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu inayotoa thamani ya maisha yako na sio vinginevyo.
Kwa hiyo kama kwa namna moja au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika mahali unajilaumu kwamba ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea, huu sio wakati wa kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani itakayobadilisha maisha yako. na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani darasani, inatafutwa mtaani kwa watu sahihi.
Ni mzigo mkubwa sana kwako na kwa jamii kwa ujumla kuwa umesoma halafu hauna mafanikio makubwa. Kama iko hivyo kwako, jiongeze kidogo tu, anza kuisaka elimu sahihi, elimu ambayo itakupa thamani sahihi ya maisha yako na kukubadilisha na kuwa mtu wa mafanikio. Maisha ya mafanikio hayaji kwa kusoma saana, bali ni kwa kujifunza vitu sahihi ambavyo vina uwezo wa kubadilisha maisha yako.
9. Kama vile ambavyo miili yetu ina hitaji chakula kizuri kila siku, pia akili zetu zinahitaji maarifa bora kila siku ambayo yataweza kutubadilisha hapa tulipo na kutupeleka eneo zuri zaidi kimafanikio.
10. Njia mojawapo ya wewe kujisikia vizuri ni kufanya vitu ambavyo hutaweza kuhitaji malipo yake kutoka kwa wengine. Unapojisikia vizuri ni rahisi sana kuweza kufanya mambo makubwa na kwa msukumo mkubwa pia ulio ndani yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Apr 24, 2017

Tatizo Kubwa La Kutokutaka Kukosea Wakati Unatafuta Mafanikio Ni Hili Hapa.

No comments :
Hakuna mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kukosea, kama hutakosea na ukaweza kufanikiwa basi wewe naweza kusema ni miongoni mwa watu ambao wana bahati sana. Mafanikio ni matokeo ya kujifunza kutokana na makosa.
Tatizo la watu wengi wanataka kufanikiwa lakini bila kukosea na wanasahau kwamba hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana kwa namna hiyo. Mafanikio yanakuja kwa kukosea na hilo si kosa, pengine kama unavyofikiri.
Unapotaka kufanikiwa bila kukosea, kiuhalisa huwezi kufanikiwa sana kwa sababu, tatizo kubwa la kutokukosea linakufanya ufanye mambo mengi kwa woga na mwisho wa siku kujikuta ukipata mafanikio kidogo sana.
Kwa hiyo ikiwa na maana kwamba kama unataka kufanikiwa, kukosea hakukwepeki, na wala hilo sio suala la kuanza kujutia, ninaposema kukosea si maanishi kukosea kwa makusudi bali naamanisha zile ‘mistake.’
Kama kuna kitu umelenga kukifanya, hebu kifanye kwa moyo wote, acha kuwa na woga. Ikitokea kama umekosea au umefanya makosa kwa bahati mbaya usisimame, endelea kusonga mbele na kutafuta kilicho bora kwako.
Kushindwa kwako kutakufanya ujirekebishe na kuwa na uwezo wa kufanikiwa kwa viwango vya juu sana. Acha kuumizwa na kutokutaka kukosea kwako, kwani kumbuka kila wakati tatizo kubwa la kutokutaka kukosea ni kushindwa kufanikiwa sana.
Unahitaji sana kujifunza kutoka kwenye kukosea kwako kila wakati, fanya maisha yako yawe shule bora ya kuweza kukusaidia kufanikiwa kwa viwango vya juu kabisa, hivyo ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Makala hii imeandikwa na Imani Ngwangwalu, DIRA YA MAFANIKIO.

Apr 21, 2017

Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.

No comments :
Njia pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia kikamilifu hadi ikuletee mafanikio.
Ili kuanzisha biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako iweze kudumu na kutoa faida uitakayo.
Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.
 1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa huduma hiyo.
2. Kuwa mbunifu,  hilo ndilo jambo kubwa zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara  yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama.

3. Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi katika biashara yako. hakua biashara ambayo italeta mafanikio makubwa kama wewe mwenyewe una lugha mbovu na wateja wako.
4. Epuka kutoa pesa ya mtaji kwa mahitaji binafsi utaua biashara. Hakikisha mahitaji ya biashara na mahitaji yako binafsi unatenga kabisa. ni sumu kubwa sana katika biashara kama eti huwezi kutofautisha matumizi binafsi  na biashara yako. 
5. Jenga utaratibu wa  kufanya tathimi ya biashara yako wapi ulipotokana wapi ulipo na wap unaelekea,? Je, unasonga mbele au unarudi nyuma, ukiona unarudi nyuma jiangalie upya, kujitathimini na ushituke mapema kabla jahazi halijazama.
6. Hifadhi kumbukumbu, hasa matumizi pamoja na mapato hata ya shilingi moja ya sehem ya biashara. Jambo ambalo watu wengi hasa sisi weusi ni ngumu kwetu, na hii ni kila siku unatakiwa kufanya. Huwezi kuendesha biashara na  ikakua bila ‘documentation’. Hutajua ulikotoka, ulipo na unako enda kibiashara.
7. Kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali wanaofanya biashara kama yako na kufanikiwa pia usiwapuuze walioshindwa kwani nao wanacho cha kukufundisha. Jifunze kwao kila siku hadi uweze kufanikiwa.
8. Kuhakikisha biashara/duka haliishiwi bidhaa na kama likiishiwa bidhaa maana yake uliowakopesha hawajarudisha, pia jitahidi kuweka mambo, mazingira ya kuvutia wateja. Ukiweka mazingira hayo ujue ni lazima utaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
9. Kujitahidi kuweka aina ya bidhaa ambazo wateja wako watapata kwa urahisi na jamii itakayo kuzunguka. Mteja anapenda sana duka ambalo kila akienda hakosi bidhaa ambayo anaihitaji. Hapo ndipo mahali pake.
10. Jitahidi na jifunze kukubali challenges/changamoto  katika biashara yako na kutafuta njia madhubuti ya kuzimaliza au kuzishughulikia. Ukiwa mtu wa kulia na hutaki changamoto uwe na uhakika hutafika popote.
11. Jitahidi kuangalia mbele kadri unavyona faida inaongezeka, jitahidi kuongeza mtaji na kuzid kupanua biashara, hata kwa kufungua matawi zaidi pengine na kuongeza ubora na ufanisi.
 12. Usafi, ukarimu, kusoma nyakati, utafiti na ubunifu na ni moja pia ya mambo ya kuzingatia. Eneo lako la biashara likiwa safi na ukaongeza na ukarimu ni lazima utawavuta wateja wako katika biashara kwa sehemu kubwa.
Kama unataka kuanzisha biashara na ikakupa faida, hayo ndiyo mambo ya msingi sana unatakiwa kuyazingatia na kuyatilia maanani kwa kiasi kikubwa ili kupata mafanikio makubwa katika biashara yako.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa kibiashara.
Kama unapenda kujifunza kwa ukaribu kabisa na sisi na kupata mafunzo mengi zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App, kujiunga tuma neno THE UNIVESITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35, ili kupata nafasi ya kuunganishwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

Apr 20, 2017

Jinsi Ya Kufanikiwa Katika Ulimwengu Huu Wenye Kelele Nyingi.

No comments :
Tunaishi katika ulimwengu ambao una vitu au mambo mengi yanayotutaka kila siku tuyafatilie tena ikiwezekana kwa ukaribu.
Si ajabu kuamka asubuhi ukakutana na meseji 50 kwenye wasap au ukakutana na habari nyingi ambazo unatakiwa uzijue na kuzifatilia.
Pia si ajabu kabla hujakaa sawa ukatumiwa meseji za kawaida au kupigiwa simu kabisa ambapo kikawaida unatakiwa uzijibu.
Si ajabu tena ukapewa ‘appointment’ na mtu ambayo unatakiwa uitekeleze ‘appointment’ hiyo bila kufanya hivyo unaweza kaanza kujihisi mnyonge.
Ukiangalia kwa siku moja unaweza kuwa na vitu vingi sana vya kufanya ambavyo vyote hivyo vinataka kutumia muda wako.

Kitu cha kujiuliza utafanikisha vipi mambo yote hayo kwa muda ulionao? Jibu ni rahisi tu hapo hutaweza.
Ili uweze kufanikisha karibu kila kitu hapo na kwenda katika hali ya usawa ya kufanikisha ukitakacho, unatakiwa kuweka nguvu ya uzingativu kwa jambo moja tu.
Kuwa na mambo mengi sana na kutaka kuyaacha yote kwa pamoja au kugusa gusa mara umegusa hiki, mara umeacha utajikuta hufanikiwi kwa mambo mengi.
Kitu kubwa unatakiwa kujiwekea ratiba ya vitu vya kufanya. Unapoamka asubuhi tambua kabisa ni mambo gani ambayo utayafanya.
Ukishayajua mambo hayo anza kutekeleza moja baada ya jingiine bila kuyumbishwa mawazo yako popote pale.
Ukishaweka mawazo yako pamoja, usiyumbishwe na kitu mpaka unahakikisha kazi ambayo ulikuwa umejiwekkea imeweza kufika mwisho kabisa.
Huwezi kufanikiwa ikiwa akili zako zitakuwa zinaruka ruka ruka mara huku mara kule, unatakiwa kutulia kufanya kitu kimoja tena kwa utulivu mkubwa.
Hakuna muujiza ambao unaweza ukautumia kuweza kufanikiwa katika dunia hii yenye mambo mengi zaidi tena bila kuweka nguvu zako nyingi za uzingativu pamoja.
Watu wenye mafanikio ndio wanavyofanya na kufanikiwa. Ni watu wa kufatilia jambo moja kwa umakini na utulivu mkubwa mpaka kuona kila kitu kipo sawa.
Hebu anza leo kuweka nguvu zako kwenye jambo lako moja hadi likupe mafanikio, kinyume cha hapo utakuwa unajidanganya sana.
Hivi ndivyo unavyoweza kufanikiwa katika ulimwengu ambao una kelele na mambo mengi sana, kikubwa weka nguvu ya uzingativu.
Chukua hatua katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu.


Apr 19, 2017

Pesa Inatakiwa Kuja Kwako Kwa Sababu Hii.

No comments :
Kila binadamu amezaliwa kama mchumi na anapaswa kuwa mchumi, lakini kwa wastani watu wengi siyo wachumi kwa sababu hatujui thamani ya vitu ambavyo tayari tunavyo.

Kuwa mchumi maana yake siyo kuwa mbahili, bali ni ile hali ya kuweza kupata matokeo makubwa kutokana na matumizi kidogo. Kazi ya kupata matokeo makubwa kutoka kwenye matumizi madogo.

Hiki si kitu cha hivi hivi bali ni..kitu kinachotulazimu wote kujifunza “menejimenti” ya rasirimali mbalimbali kwa lengo la kupata bidhaa au huduma. Unapojifunza menejiment inakusaidia kufanikiwa.

Katika mtazamo wa maisha ya binadamu ni kwamba neno menejimenti ni uwezo wa wewe kuweza kuongeza thamani ya kipaji chako ambacho kimsingi ndiyo zawadi uliyopewa na Mungu.

Zawadi au kipaji chako unatakiwa ukitoe nje katika sura ya suluhisho kwa matatizo yanayoikabili jamii na dunia kwa ujumla na hasa tukianza na wale waliotuzunguka. Je, kitu cha kujiuliza, unakitumia kipaji chako?

Ili haya yote yaweze kufanyika ni lazima kila mmoja ajifunze kuwa na kuishi maisha ya “meneja”. Kuwa meneja siyo lazima uwe bosi au msomi uliyebobea bali ni ule uwezo wa kuweza kuunganisha nguvu ya akili na nguvu ya mwili kuzalisha bidhaa au huduma.

Pia lazima kazi ya menejimenti iambatane na udhibiti katika kutumia rasilimali zilizopo ili hatimaye mambo makubwa yatokee kutoka kwenye mambo madogo. Naamini hili linawezekana.

Endapo ukiamua kuwa na kuishi kama meneja, pesa ni rahisi kuipata, na katika hali ya kawaida hakuna sababu ya pesa kutokuja kwako. Kwa maneno mengine, pesa siyo tatizo bali tatizo ni manejimenti ya pesa.

Pesa inahitaji nidhamu, juhudi, maarifa bila kuchoka na udhibiti. Watu wengi tunafaulu kiasi fulani kipengele cha kutafuta pesa, lakini mbinu tunazotumia kudhibiti pesa zetu ni za kizamani sana na zimepitwa na wakati.

Matokeo yake, pesa nyingi tunayoipata, hatujui inapoteaje na inaenda wapi. Na kila wakati hubki tunajiuliza maswali mengi sana kwa nini kila wakati tunaishia na pesa, kumbe tatizo ni “menejiment” ya pesa.

Maana nyingine ya manejimenti ni ile hali ya kuwa mbunifu, mwangalizi na mdhibiti wa rasirimali ili ziweze kutumika kulingana na vipaumbele vilivyowekwa na mhusika. Katika historia ya maisha ya binadamu, imeonekana kuwa Mungu huwa hatoi pesa kwa waumini BALI yeye utoa pesa kwamameneja.

Kila wakati unapoomba kupata pesa Mungu anakupa WAZO. Tatizo la waumini wengi tunataka taslimu (cash), hatutaki MAWAZO. Na tukumbuke kuwa, ili mawazo yetu yaweze kubadilika kuwa pesa, lazima kitumike kitu kinachoitwa “menejimenti”.

Kwa maana nyingine ni kwamba, pesa yoyote inakuja kwako endapo utatumia “menejimenti” katika kutumia vizuri rasilimali kwa malengo na makusudio ya WAZO linalokujia akilini mwako.

Usidhani wewe huna pesa, nasema pesa unayo, LAKINI unachokikosa ni menejimenti ya mawazo pamoja na jinsi ya kuyageuza kuwa pesa. Manejimenti ndiyo lengo la msingi kwa binadamu yoyote yule.

Ukweli ni kwamba, kila utakaposhindwa kuwa na menejimenti ya vitu au mawazo uliyonayo lazima upoteze hata hicho kidogo ulichonacho. Menejimenti ndiyo inayovuta rasilimali zingine kuja kwako. Kama hakuna menejimenti, biashara yoyote haiwezi kukua hata kidogo.

Kutokana na sisi kushindwa kuwa mameneja wa maisha yetu; ndiyo maana hatuwezi kulipa madeni tunayodaiwa; ndiyo maana tunawafanyia kazi watu wengine hata kama wanatutukana na kutudharirisha bado tunawafanyia kazi kwasababu moja tu! tumeshindwa kuwa mameneja wa mstakabali wetu wa maisha yetu.

Jenga sababu ya pesa kuja kwako.
Kutokana na kushindwa au kupuuzia umuhimu wa menejimenti; tumebaki kuwa watu wa kutegemea “miujiza”. Lakini kumbuka kwamba miujiza siku zote ni kwa wale watu wavivu, kwa wachapa kazi hakuna miujiza.

Endelea kujifunza kila siku kwa kutemblea DIRA YA MAFANIKIO kila siku, kama unataka kujifunza kwa ukaribu na kuendelea kupata mafunzo mengi, jiunge nasi kwenye kundi la whats app. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 04 80 35 ili kuunganishwa.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA CYPRIDION MUSHONGI WA MAARIFA SHOP BLOG.

Apr 18, 2017

Kama Kweli Unataka kufanikiwa Wekeza Akili Yako katika Jambo hili.

No comments :
Kuna wakati mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo.
Na umakini ni ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika kufikiri na kutenda jambo hilo.
Kamwe hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa umaikini.  Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo.

Hivyo umakini katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.
Mwisho jitahidi kuwa makini  juu ya mambo haya;
1. Kuwa makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda.
2. Kuwa makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka. Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu wengine.
3. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea.
4. Kuwa makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati.
5. Kuwa makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija gani kwako.
6. Kuwa makini katika kutambua thamani ya muda na pesa.
Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.
Endelea kutembelea blog hii ya DIRA YA MAFANIKIO kila wakati, kwani tunaamini siri ya mafanikio yako ipo katika blog hii.
Imeandikwa na afisa mipango; Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com


Apr 17, 2017

Kuwa Makini Sana Na Mambo Haya Yanaweza Kukuzia Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Kuna wakati unaweza ukawa unashangaa kwa nini ndoto zako hazitimii?  Utakuta umejiwekea malengo yako vizuri, lakini unashangaa ni malengo machache sana yanayotimia au wakati mwingine hakuna kabisa.
Sina shaka yoyote umeshawahi kukutana na hali kama hii wakati fulani katika maisha yako. Kiuhalisia, yapo mambo mawili ambayo kitaalamu hupelekea ndoto zako kushindwa kutimia ikiwa hutayajua vizuri.
Jambo la kwanza, ni kutokujua kile unachokitaka vizuri. Hili ni jambo ambalo hupelekea wengi kushindwa kufanikisha ndoto zao kabisa. Kama hujui kile unachokitaka vizuri, suala la kufanikisha ndoto zako litakuwa gumu kidogo.
Katika akili yako ili uweze kufanikisha ndoto yako au jambo unalolitaka kwa urahisi, ni lazima kile kitu unachokitaka uweze kukijua vizuri. Tambua njia utakazotumia hadi kukipata kitu hicho pia tambua kitu hicho changamoto zake ni zipi.

Acha kufanya kosa la kuuchanganya ubongo wako kwa kuupa vitu vingi. Kuwa maalumu kwa kujua vizuri kile unachokitaka. Usipojua kile unachokitaka kwa uhakika na kukifanyia kazi, ni wazi hutaweza kufanikiwa na hilo halina ubishi.
Jambo la pili, ni kukosa hamasa ya kutosha kwa kitu hicho unachokitaka. Hamasa ni kitu cha muhimu sana ili kufikia ndoto zako. Ukishakijua kitu hicho vizuri, hamasa itakusaidia kufanya kila jitihada hata kama umechoka.
Wengi ni watu wa kutaka kufikia lengo fulani katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hujikuta ni watu wa kukosa hamasa ya kuwasukuma kuweza kukamilisha malengo yao.
Ili kufanikiwa, fanya kila ufanyalo kuhakikisha una hamasa ya kufanya hicho unachotaka kukifanya katika maisha yako. Inapotokea hamasa hiyo umeikosa acha kusimama eti kwa sababu ya kukosa hamasa.
Maisha hayasimami eti kwa sababu wewe hujisikii kufanya kitu fulani au umekosa hamasa. Endelea kusonga mbele, huku ukitafuta hamasa ya kufanikiwa kwako kila siku. Ukifanya hivyo utafika mbali kimafanikio.
Katika hali ya kawaida, kama kila wakati unakosa mambo haya mawili suala la kufanikiwa kwako linakuwa ni gumu sana. Hivyo, ni lazima sana kwako kujua vizuri kile unachokitaka na kuwa na hamasa kubwa yaani ‘burning desire’ ya kuhakikisha kitu hicho ni lazima unaweza kukipata.
Ukichunguza watu wengi ambao hawajafanikiwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu hizi mbili tu na si vinginevyo. Kama unafikiri natania anza kufatilia, huku lakini ukianza na wewe.
Kama unajiona hujafanikiwa vya kutosha jiulize binafsi je, unakijua vizuri kile unachokitaka na huna tamaa ya kutaka  hiki mara kile na mwisho wa siku kuwa na malengo mengi yasiyotekelezwa?
Usiishie hapo tu, tena kama unaona hujafanikiwa vya kutosha jiulize, je, una hamasa kubwa ya kuona ndoto zako zinatumia? Je, unakosa usingizi na kuamua kujituma usiku na mchana hadi kufanikiwa?
Ukipata majibu ya maswali hayo yatakusaidia sana kuweza kufanikiwa na kuwa mtu mwingine tofauti na hatimaye kuweza kufanikisha zoezi zima la kutimiza ndoto zako. Jitoe kikamilifu kuona ndoto zako zinatimia kwa kuyajua mambo hayo mawili.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Apr 16, 2017

DIRA YA MAFANIKIO; Ujumbe Wetu Kwako Katika Siku Hii Ya Pasaka.

No comments :
Habari za muda huu mpendwa msomaji wetu wa blog hii ya DIRA YA MAFANIKIO, ni matumaini yetu u mzima na unaendelea vyema na pilikapilika za hapa ili kuhakikisha mkono unaenda kinywani.
Ikiwa leo ni siku ya tarehe 16/04/017, siku hii ni muhimu sana duniani kote kwani ni siku ambayo tunasherehekea sikukuu ya pasaka. Siku hii kwa mujibu wa mandiko katika biblia ni siku ambayo tunaadhimisha kufufuka kwa bwana yetu Yesu kristo.
Kwa kulitambua hilo uongozi mzima wa blog hii, unapenda kuchukua nafasi hii adhimu kuweza kukutakia siku njema katika kusheherekea siku hii, huku tukuzidi kukumbusha siku hii ifanye ni siku ya kumuomba na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa uzima na mafanikio ambayo amaekujalia. Usifanye siku hii kama ruksa au sehemu ya kutenda dhambi.

Kwani tumekuwa tukishuhudia baadhi ya watu siku kama hii ya leo, wamekuwa wakieguza kama sehemu ya kuanguka dhambini. Hivyo tunachokudisitiza ni kwamba epuka mambo ambayo yatakufanya uanguke katika mambo ambayo ni chukizo mbele ya Mungu.
Mwisho kabisa tunashukuru kwa namna mmoja ama nyingine kuwa mdau wetu mzuri, katika kufuatilia makala mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwekwa katika mahala hapa, ni imani yetu zinakusaidia kwa kiwango kikubwa sana, kwa falsafa yetu inasema Badili maisha yako kwa kuwa na fikra sahihi kwa kila kitu huanza katika fikra.
Endelea kuwa sehemu yetu kwa kusoma makala mbalimbali mahala hapa, nasi tutaendelea kuwa sehemu yako kwa kukuleta elimu zitakazo kusaidia kupata mafanikio zaidi. Pia kwa maoni na ushauri wowote usisite kuwasiliana nasi.
"Tunakutakia pasaka njema na siku njema kwako"
Asante.
Imeandaliwa na uongozi mzima wa blog ya Dira Ya Mafanikio.

Apr 15, 2017

Tafakari Kwa Kujifunza Mambo Haya Yatakayoboresha Maisha Yako Leo.

No comments :
1. Mafanikio makubwa sana utayapata kama unafanya kitu ambacho unakipenda sana toka moyoni. Ikiwa hukipendi kile unachokifanya yaani unakifanya kitu hicho kwa kujilazimisha uwe na uhakika, hutafanikiwa sana.
Hivyo kila wakati pata muda wa kujiuliza je, ni kitu gani ambacho unakipenda? Kisha baada ya hapo kifanye kitu hicho kwa nguvu zote. Kumbuka siku zote mafanikio makubwa yanakuja kwa kufanya kile kitu unachokipenda.
2. Ni rahisi kufanikiwa na kupata karibu kila kitu unachokihitaji katika maisha yako ikiwa utakuwa tayari kuwasidia wengine nao kuweza kufanikiwa. Ndio maana mara nyingi watu wenye mkono wa ‘birika’ si rahisi sana kuweza kuwaona wakifikia viwango vya mafanikio makubwa.
Jiulize kitu gani ulichonacho ambacho unaweza ukakitoa na kikawa msaada mkubwa kwa wengine? Kama kitu hicho unacho hebu kitoe, acha kukaa nacho tu wewe peke yako, washirikishe na wengine ili kiwe baraka kwenu wote.

3. Kama unataka kuwa TAJIRI, kila wakati hakikisha unakuwa na akili ya kijasiriamali na kujitahidi sana kufanya yale kama wanayoyafanya matajiri hata kama umeajiriwai. Ikiwa utakwenda kinyume cha hapo sahau kabisa kuwa TAJIRI maishani mwako.
4. Kitu kibaya katika maisha yako ni kule kujishusha na kujiona ni mdogo kumbe wakati hata hauko hivyo. Wengi wanatabia ya kujishusha sana na kujiona ni kama wadudu kumbe ni wakubwa sana kuliko fikra zao hizo.
Hebu jiulize ni kwa nini unajishusha sana na kujiona hufai? Je, unafikiri kuna kitu ambacho umekikosa hadi ikapelekea ukajiona mnyonge kiasi hicho. Sikiliza hujaumbwa ili uwe mnyonge au uwe mdogo kama unavofikiri, wewe ni mtu tofauti sana.
Amini unaweza ukapata mafanikio mara kumi ya hapo ulipo sasa. Unashangaa, ndio unaweza kufanikiwa zaidi ya mara kumi ya hapo ulipo wala hutakiwi kujiwekea mipako. Kila kitu kinawezekana kwako ukiweka nia na kuamini, itakuwa.
5. Kila wakati jiulize ni kwa namna gani kupitia kile unachokifanya utakwenda kubadilisha maisha ya wengine na kuwafanya wawe watu wa mafanikio. Jitahidi kila siku uwe baraka kwa wengine. Weka juhudi si za kukusaidia wewe tu ila mpaka kuwasadia wengine pia.
Kwa hiyo unapotafuta pesa kumbuka zote sio zako, tenga angalau kidogo ambazo unaweza ukampa yule ambaye hajiwezi. Kama ambavyo nasema mara kwa mara, wakati mwingine mafanikio makubwa yanakuja kupitia utoaji wako. Je, unatoa kiasi gani kuwasaidia wenye uhitaji hapo ndipo mafanikio yako yalipo.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

Apr 14, 2017

Mambo Matatu Yatakayokusaidia Kuwa Mtu Wa Heshima Katika Jamii Yako.

No comments :
Hakuna ubishi wowote, heshima ni moja ya kitu ambacho karibu kila mtu anakitafuta katika maisha yake. Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika, heshima inatafutwa na watu wengi sana.
Ndio maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile.
Pamoja na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima zao katika jamii?
Je, pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi?
Katika makala haya tumekuandalia dondoo muhimu za kufuata na ambazo zitakusaidia kuweza kujenga heshima katika jamii yako. Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;-
1. Toa thamani.
Ili uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vitu ambavyo vinagusa maisha ya watu. Haijalishhi unafanya kitu gani lakini lilokubwa fanya kitu ambcho kinagusa maisha ya watu, kina mchango wa kubadili maisha ya wengine.
Siku zote haijalishi una pesa za kiasi gani, lakini je, kupitia hizo pesa wewe binafsi unatoa mchango gani kwa wengine kufanya maisha ya yakabadilika? Watu wote wanaotoa thamani na kuweza kubadili maisha ya wengine ni watu wa kuheshimika.
Kama unafikiri natania kuhusu hili angalia watu waliokuwa wakipagania uhuru, heshima zao zikoje katika jamii zao, utangudua heshima zao ni kubwa sana. Hivyo hiyo inatuonyesha njia mojawppo ya kujiwekea heshima toa thamani kwa kugusa maisha ya watu.

2. Wakubali watu.
Mbali na kutoa thamani, njia mojawapo nyingine ambayo inaweza kukujengea heshima ni kuwakubali watu. Kubali mawazo yao wanayotoa ila kama kweli yanasaidia kujenga jamii au kuwasaidia wengine.
Kama unahitaji kuwakosea, tafadhari usiwakosoe hadhari, jitahidi ukosoe kwa pembeni. Hiyo pia ni njia nzuri ya kukusaidia kujua au kutambua kwamba yapo makosa ambayo umeyaona na ni muhimu kurekebishwa.
3. Unapokosea, omba msamaha.
Hakuna mtu ambaye tunaweza tukasema yupo kamili kwa asilimia zote. Hivyo, unapokosea iwe kwa jamii yako au kwa watu wako wa karibu, hebu kuwa mwepesi wa kuomba msahamaha.
Msahama ni kitu kidogo sana lakini utakusaidia kukujengea picha kwa watu wengine kwamba una busara. Kwa sababu ya busara zako utajikuta ukiwa ni mtu wa kuheshimika karibu na watu wote.
Hizi ni mbinu miuhimu ambazo mtu yoyote anayataka kuheshimiak katika jamii yake anaweza akazitumia kama njia mjawapo ya kumsaidia kumjengea heshima kubwa katika jamii yake.
Kumbuka unapokuwa unaheshimika katika jamii yako hiyo inakupelekea wewe kuweza kukubalika na kuaminika kwa kiasi kikubwa sana katika maisha yako.
Tunakutakia siku njema na mafanikio mema yawe upande wako,
Endelea kujifunza kupita DIRA YA MAFANIKIO kila siku kupata maarifa yatakayobadilisha maisha yako.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com