Apr 12, 2017
Kama Unataka Kutunza Muda Wako Vizuri, Fuata Sheria Hizi Tatu Muhimu.
Sina
shaka wengi wetu wamekuwa wakijua umuhimu
na faida za kutunza muda vizuri, lakini kwa bahati ni wachache sana
wanaofanikiwa kuweza kutunza muda wao vizuri. Wengi hujikuta ni watu wa
kupoteza muda sana karibu kila siku.
Kitu
cha kujiuliza ni kitu gani ambacho mara nyingi kinapelekea wengi wanapoteza
muda wao, ingawa tayari wanajua au wameshaambiwa muda ni kitu cha thamani sana
na ukipoteza muda huwezi kuurudisha tena?
Naamini
kabisa kitu kinachopelekea wengi kuendelea kupoteza muda wao ni kwa wao wenyewe
kutokujua sheria zinazofaa kutumiwa ili kulinda muda wao vizuri. Ni wakati
muafaka umefika wa kujua sheria hizo ili ikusaidie kutunza muda wako vizuri.
Hata
hivyo, kabla sijakwambia sheria hizo naomba nikwambie hivi mara nyingi watu
wanaotunza muda wao vizuri, wanafanya mambo yao kwa uhakika mkubwa sana na kwa
ubora wa hali ya juu.
Mpaka
hapo unaona suala la kutunza muda ni la lazima sana kwako ili kuweza kufikia
mafanikio ya juu. Ni wakati wako sasa wa kwenda pamoja ili tujifunze sheria za
muhimu ambazo unaweza ukazitumia zikusaidie kutunza muda wako kwa ufasaha.
1. Weka vipaumbele.
Ili uwe
na matumizi mazuri ya muda wako ni lazima uwe na vipaumbele ambavyo utakwenda
kuvifanya kwa siku husika. Na vipaumbele hivi haviji kwa bahati mbaya bali
vinatokana na majukumu ambayo umejiwekea kufanya kwa siku hiyo.
Kabla
hujaanza kufanyia kazi orodha ya kazi ulizojiwekea kwa siku hiyo ni muhimu sana
kwako kujua kitu gani cha muhimu na kitu gani sio cha muhimu kwako kukifanya. Sio
kila jambo ni la muhimu katika kukufikisha kwenye ndoto zako.
Ili kujua
hilo angalia hicho unachokifanya kinakusogeza kwenye ndoto zako au kinakurudisha
nyuma na ndoto zako. Hivyo ukashaona hivyo, utajifunza na utaanza utaratibu wa
kupangilia ndoto zako kwa ufasaha hadi kufanikiwa.
2. Vunja vunja muda wako.
Kuna
wakati kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu inaweza isikupe matokeo unayoyataka. Kama
hiyo iko hivyo, maana yake unahitajika kuvunja vunja muda wako katika sehemu
ndogo ili uweze kufanya kitu cha uhakika wakati akili yako ina nguvu.
Wataalamu
wengine wa masuala ya muda, wanatuambia kwamba inachukua dakika 90 kwa ubongo
wa binadamu kufanya kazi kwa ufasaha. Hiyo ikiwa na maana ukizidisha dakika
hizo, hakuna kazi ambayo unaweza ukaifanya kwa ufasaha mkubwa tena.
Hivyo
ni jukumu lako kuweza kuangalia ni muda upi ambao ni rasmi kwako utautenga ili kutekeleza majukumu
yako. Kwa mfano, unaweza ukaanza kufanya kazi kwa dakika 25 kisha dakika 5
unapumzika au unaweza ukavunja muda kwa jinsi unavyoweza wewe ili kuleta
ufanisi.
Hii ni
mbinu inayokusaidia ufanye kazi nyingi bila ya wewe kuweza kuchoka sana na
kujikuta karibu umekamilisha kila kitu ambacho ulikuwa unakihitaji kukimalisha
kwa muda wako husika.
3. Gawa majukumu kwa watu wengine.
Acha
kuwa king'ang'anizi wa kujaribu kufanya kila kitu mwenyewe, jifunze kufuta watu
ambao wanaweza kukusaidia majukumu ambayo sio lazima ufanye wewe. Wape watu kazi
wakusaidie, hiyo itakuokolea sana muda wako kuliko unavyodhani.
Mbinu
hii ya kugawa majukumu kwa watu wengine, ni mbinu mojawapo bora ya kukuokolea
muda wao. Watu wenye mafanikio wanatumia mbinu hii kuweza kufanikiwa. Hakikisha
unawapa watu wengine majukumu, ama ‘leverage’
ili wakusaidie kufanikiwa.
Endelea
kujifunza kupitia mtandao wako bora wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713
048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.