Apr 19, 2017
Pesa Inatakiwa Kuja Kwako Kwa Sababu Hii.
Kila binadamu amezaliwa kama mchumi na anapaswa kuwa mchumi,
lakini kwa wastani watu wengi siyo wachumi kwa sababu hatujui thamani ya vitu
ambavyo tayari tunavyo.
Kuwa mchumi maana yake siyo kuwa mbahili, bali ni ile
hali ya kuweza kupata matokeo makubwa kutokana na matumizi kidogo. Kazi ya
kupata matokeo makubwa kutoka kwenye matumizi madogo.
Hiki si kitu cha hivi hivi bali ni..kitu
kinachotulazimu wote kujifunza “menejimenti” ya rasirimali mbalimbali kwa lengo la
kupata bidhaa au huduma. Unapojifunza menejiment inakusaidia kufanikiwa.
Katika mtazamo wa maisha ya binadamu ni kwamba neno “menejimenti” ni uwezo wa wewe kuweza kuongeza thamani
ya kipaji chako ambacho kimsingi ndiyo zawadi uliyopewa na Mungu.
Zawadi au kipaji chako unatakiwa ukitoe nje katika sura ya suluhisho
kwa matatizo yanayoikabili jamii na dunia kwa ujumla na hasa tukianza na wale
waliotuzunguka. Je, kitu cha kujiuliza, unakitumia kipaji chako?
Ili haya yote yaweze kufanyika ni lazima kila mmoja ajifunze
kuwa na kuishi maisha ya “meneja”. Kuwa meneja siyo lazima uwe bosi au msomi
uliyebobea bali ni ule uwezo wa kuweza kuunganisha nguvu ya akili na nguvu ya
mwili kuzalisha bidhaa au huduma.
Pia lazima kazi ya menejimenti iambatane na udhibiti katika
kutumia rasilimali zilizopo ili hatimaye mambo makubwa yatokee kutoka kwenye
mambo madogo. Naamini hili linawezekana.
Endapo ukiamua kuwa na kuishi kama meneja, pesa ni rahisi
kuipata, na katika hali ya kawaida hakuna sababu ya pesa kutokuja kwako. Kwa
maneno mengine, pesa siyo tatizo bali tatizo ni “manejimenti ya pesa”.
Pesa inahitaji nidhamu, juhudi, maarifa bila kuchoka na
udhibiti. Watu wengi tunafaulu kiasi fulani kipengele cha kutafuta pesa, lakini
mbinu tunazotumia kudhibiti pesa zetu ni za kizamani sana na zimepitwa na
wakati.
Matokeo yake, pesa nyingi tunayoipata, hatujui inapoteaje na
inaenda wapi. Na kila wakati hubki tunajiuliza maswali mengi sana kwa nini kila
wakati tunaishia na pesa, kumbe tatizo ni “menejiment” ya pesa.
Maana nyingine ya manejimenti ni ile hali ya kuwa mbunifu,
mwangalizi na mdhibiti wa rasirimali ili ziweze kutumika kulingana na
vipaumbele vilivyowekwa na mhusika. Katika historia ya maisha ya binadamu,
imeonekana kuwa Mungu huwa hatoi pesa kwa waumini BALI yeye utoa pesa kwa“mameneja”.
Kila wakati unapoomba kupata pesa Mungu anakupa WAZO. Tatizo la
waumini wengi tunataka taslimu (cash), hatutaki MAWAZO. Na tukumbuke kuwa, ili
mawazo yetu yaweze kubadilika kuwa pesa, lazima kitumike kitu kinachoitwa “menejimenti”.
Kwa maana nyingine ni kwamba, pesa yoyote inakuja kwako endapo
utatumia “menejimenti” katika kutumia vizuri rasilimali kwa
malengo na makusudio ya WAZO linalokujia akilini mwako.
Usidhani wewe huna pesa, nasema pesa unayo, LAKINI unachokikosa
ni menejimenti ya mawazo pamoja na jinsi ya kuyageuza kuwa pesa. Manejimenti
ndiyo lengo la msingi kwa binadamu yoyote yule.
Ukweli ni kwamba, kila utakaposhindwa kuwa na menejimenti ya
vitu au mawazo uliyonayo lazima upoteze hata hicho kidogo ulichonacho.
Menejimenti ndiyo inayovuta rasilimali zingine kuja kwako. Kama hakuna
menejimenti, biashara yoyote haiwezi kukua hata kidogo.
Kutokana na sisi kushindwa kuwa mameneja wa maisha yetu; ndiyo
maana hatuwezi kulipa madeni tunayodaiwa; ndiyo maana tunawafanyia kazi watu
wengine hata kama wanatutukana na kutudharirisha bado tunawafanyia kazi
kwasababu moja tu! tumeshindwa kuwa mameneja wa mstakabali wetu wa maisha yetu.
Jenga sababu ya pesa kuja kwako. |
Kutokana na kushindwa au kupuuzia umuhimu wa menejimenti;
tumebaki kuwa watu wa kutegemea “miujiza”. Lakini kumbuka
kwamba miujiza siku zote ni kwa wale watu wavivu, kwa wachapa kazi hakuna
miujiza.
Endelea kujifunza kila siku kwa kutemblea DIRA YA MAFANIKIO kila siku, kama unataka kujifunza kwa ukaribu na
kuendelea kupata mafunzo mengi, jiunge nasi kwenye kundi la whats app. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 04 80 35 ili kuunganishwa.
MAKALA HII IMEANDIKWA
NA CYPRIDION MUSHONGI WA MAARIFA SHOP BLOG.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.