Apr 14, 2017
Mambo Matatu Yatakayokusaidia Kuwa Mtu Wa Heshima Katika Jamii Yako.
Hakuna
ubishi wowote, heshima ni moja ya kitu ambacho karibu kila mtu anakitafuta
katika maisha yake. Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika, heshima
inatafutwa na watu wengi sana.
Ndio
maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga
heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha
thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile.
Pamoja
na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na
wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima
zao katika jamii?
Je,
pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho
unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii
na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi?
Katika
makala haya tumekuandalia dondoo muhimu za kufuata na ambazo zitakusaidia
kuweza kujenga heshima katika jamii yako. Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima
na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;-
1. Toa thamani.
Ili
uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vitu
ambavyo vinagusa maisha ya watu. Haijalishhi unafanya kitu gani lakini
lilokubwa fanya kitu ambcho kinagusa maisha ya watu, kina mchango wa kubadili
maisha ya wengine.
Siku
zote haijalishi una pesa za kiasi gani, lakini je, kupitia hizo pesa wewe
binafsi unatoa mchango gani kwa wengine kufanya maisha ya yakabadilika? Watu
wote wanaotoa thamani na kuweza kubadili maisha ya wengine ni watu wa
kuheshimika.
Kama
unafikiri natania kuhusu hili angalia watu waliokuwa wakipagania uhuru, heshima
zao zikoje katika jamii zao, utangudua heshima zao ni kubwa sana. Hivyo hiyo
inatuonyesha njia mojawppo ya kujiwekea heshima toa thamani kwa kugusa maisha ya
watu.
2. Wakubali watu.
Mbali
na kutoa thamani, njia mojawapo nyingine ambayo inaweza kukujengea heshima ni kuwakubali
watu. Kubali mawazo yao wanayotoa ila kama kweli yanasaidia kujenga jamii au
kuwasaidia wengine.
Kama
unahitaji kuwakosea, tafadhari usiwakosoe hadhari, jitahidi ukosoe kwa pembeni.
Hiyo pia ni njia nzuri ya kukusaidia kujua au kutambua kwamba yapo makosa
ambayo umeyaona na ni muhimu kurekebishwa.
3. Unapokosea, omba msamaha.
Hakuna
mtu ambaye tunaweza tukasema yupo kamili kwa asilimia zote. Hivyo, unapokosea
iwe kwa jamii yako au kwa watu wako wa karibu, hebu kuwa mwepesi wa kuomba
msahamaha.
Msahama
ni kitu kidogo sana lakini utakusaidia kukujengea picha kwa watu wengine kwamba
una busara. Kwa sababu ya busara zako utajikuta ukiwa ni mtu wa kuheshimika
karibu na watu wote.
Hizi
ni mbinu miuhimu ambazo mtu yoyote anayataka kuheshimiak katika jamii yake
anaweza akazitumia kama njia mjawapo ya kumsaidia kumjengea heshima kubwa
katika jamii yake.
Kumbuka
unapokuwa unaheshimika katika jamii yako hiyo inakupelekea wewe kuweza
kukubalika na kuaminika kwa kiasi kikubwa sana katika maisha yako.
Tunakutakia
siku njema na mafanikio mema yawe upande wako,
Endelea
kujifunza kupita DIRA YA MAFANIKIO
kila siku kupata maarifa yatakayobadilisha maisha yako.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713
048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.