Apr 5, 2017
Jinsi Ambavyo Mazoezi Yanaweza Kukuongezea Afya Ya Mwili Na Akili Yako.
Si
wengi sana ambao wanaona umuhimu wa mazoezi katika suala zima la kuboresha afya
zao. Wengi huyaona mazoezi ni kitu cha kawaida na hawayachukulii katika ule
uzito wake.
Kutokana
na wengi kuupuza mazoezi hapo ndipo hujikuta wapo katika matatizo mengine ya
kiafya ambayo kumbe wangeyaepuka kama wangekuwa ni watu wa mazoezi.
Kwa mtu
yeyote anayezingatia mazoezi ni rahisi sana kujenga afya ya mwili na akili,
katika maisha yake. Inatokea hivyo kwa sababu, pia uimara wa mwili wako
unategemea mazoezi.
Hebu
tuangalie ni kwa jinsi gani mazoezi yanaweza kuongeza afya ya mwili na akili
yako kwa ujumla?
1. Mazoezi yanakufanya ujiamini.
Kwa
mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha kwamba ni kitu cha kawaida sana kwamba
mazoezi mara nyingi yanakufanya ujisikie vizuri. Na kwa jinsi unavyojisikia
vizuri na kujiamini kunakuwa kunaongezeka ndani mwako.
Waangalie
watu wote ambao ni watu wa mazoezi, utawaona ni watu ambao wa kujiamini sana. Ni mara chache sana kukuta
mtu ambaye anafanya mazoezi halafu tena akawa ni mtu wa kutojiamini, wengi
wanajiamini.
\
Mazoezi ni afya ya mwili wako. |
2. Mazoezi yanaifanya akili yako iwe ya
ubunifu.
Hili
linaweza kunekana ni jambo la kushangaza kidogo kwako, lakini mazoezi yana
uwezo huo wa kuifanya akili yako ikawa na ubunifu wa hali ya juu sana kuliko
ambavyo unaweza ukadhani.
Katika
moja za tafiti zilizofanyika, zinaonyesha kwa kadri mtu anavyofanya mazoezi,
anazalisha seli nyingi sana kwenye ubongo wake, matokeo yake seli hizo huongeza
ubunifu. Hutaki kuamini katika hili, anza kufanya mazoezi leo uone.
3. Mazoezi yanaipa akili yako uwezo wa
kukabiliana na changamoto.
Mbali
na mazoezi kuifanya akili yako ikawa na ubunifu lakini pia, ni ukweli ulio wazi
mazoezi yanauwezo wa kuifanya akili yako ikawa na uwezo mkubwa wa kukabiliana
na changamoto.
Akili
yako inakuwa imekaa katika mkao wa kupambana na kila aina ya changamo
inayojitokeza. Uwezo huu wa akili kuweza kupambana na changamoto hauji hivi
hivi tu bali ni kwa kufanya mazoezi.
4. Mazoezi yanakupunguzia msongo wa
mawazo.
Kila
mtu kwa namna fulani anakuwa ana msongo wa mawazo hata kwa kidogo. Kuna ambao
msongo wao wa mawazo unatokana na maisha magumu na kuna wengine unatokana na
mapenzi.
Haijalishi
msongo wako wa mawazo chanzo chake ni nini, lakini dawa kubwa ya kutoka kwenye
msongo wa mawazo ni kufanya mazoezi. Wengi wanaofanya mazoezi kwa sehemu
hupunguza sana msongo wa mawazo.
5. Mazoezi yanakupa nguvu.
Bila
shaka umeshawahi kuliona hili sana na kutambua kwamba kwa wote wanaofanya mazoezi
miili yao huonekana ina nguvu sana yaani ikiwa imekakamaa na huku ikiwa
shupavu.
Kinachotokea
kwenye mwili unapofanya mazoezi hupelekea kukujengea misuli mingi sana ndani
yako. Kwa hali hiyo ni lazima mwili wako unaonekana wenye nguvu na afya ya
kutosha.
6. Mazoezi yanakufanya ulale usingizi
mzuri.
Kwa
wale wote wanaofanya mazoezi sana, tatizo la kukosa usingizi huwa si kubwa sana
kwao. Hiyo yote ni kwa sababu mara nyingi wanakuwa wamechoka na miili huhitaji
kumpumzika.
Ni mara
chache sana kukutana na mtu ayefanya mazoezi ya kutosha halafu akawa na tatizo
la kukosa usingizi. Hicho ni kitu kigumu sana, ndio maana tunasema mazoezi ni
muhimu kwa afya na akili yako pia.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku na washirikishe na
wengine pia waweze kujifunza na kupata maarifa bora kabisa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.