Apr 18, 2017
Kama Kweli Unataka kufanikiwa Wekeza Akili Yako katika Jambo hili.
Kuna wakati
mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo
hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu
wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu
wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo.
Na umakini ni
ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda
jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo
kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika
kufikiri na kutenda jambo hilo.
Kamwe
hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa
umaikini. Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo
hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu
anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo
husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo
hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo.
Hivyo umakini
katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii
kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa
kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.
Mwisho jitahidi kuwa makini juu ya mambo haya;
1. Kuwa
makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda.
2. Kuwa
makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka.
Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu
wengine.
3. Jitahidi
kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi
ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea.
4. Kuwa
makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati.
5. Kuwa
makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija
gani kwako.
6. Kuwa
makini katika kutambua thamani ya muda na pesa.
Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.
Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.
Endelea
kutembelea blog hii ya DIRA YA MAFANIKIO
kila wakati, kwani tunaamini siri ya mafanikio yako ipo katika blog hii.
Imeandikwa na afisa mipango; Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.