Apr 4, 2017
Ni Kitu Gani Kinachokupa Hamasa Katika Kutenda Mambo Yako Ya Kimafanikio?
Asante kwa kuendelea kutembelea mtandao huu kila wakati
kwani ni imani yetu elimu zinazotolewa hapa zinakusaidia kwa namna moja ama
nyingine.
Na siku ya leo nataka tuangazie macho na akili zetu katika
kujiuliza swali lifuatalo; Ni kitu gani kinachokupa hamasa katika kutenda mambo
yako?
Watu wengi maisha yetu yamekuwa kila siku katika hali ya kawaida
kwasababu tumekuwa hatujui ni kipi ambacho kimekuwa kikitusukuma katika kufikia
malengo yetu.
Na katika hili kuna aina mbili ya hamasa ambazo zimekuwa
zikimsukuma mtu katika kutenda au kutokutenda jambo hilo. Aina ya kwanza ambazo
zimekuwa zimkimsukuma mtu kutenda jambo fulani ni hamasa ya hofu.
Hamasa hii ya hofu mara nyingi mtu hufanya jambo fulani si
kwa kupenda kutoka nafsini mwake, bali ni kwa kumuogopa mtu fulani au kuogopa
madhara yatakayotokea kama hataweza kufanya jambo hilo.
Kwa mfano hivi hujawahi kuona mtu anawahi ofisini eti kwa
sababu anamgopa bosi wake? Bila shaka umewahi kuona aina hii ya watu. Tuendelee
kutafakari kidogo hivi hujawahi kuona mtu anaendesha chombo cha usafiri nyakati
za usiku sana eti kwa sababu anawakwepa askari wa usalama barabarani?
Tafuta hamasa ya mafanikio yako kila siku. |
Bila shaka umewahi kuona aina hii ya watu. Aina hizi za tabia
ndizo tunazozita hamasa za hofu, unafanya jambo kwa sababu ya kumuogopa mtu
fulani, lakini ukweli ni kwamba aina hii ya hamasa si nzuri kuitumia kama
kweli unataka mafanikio ya kweli.
Ila kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli kila wakati
unahitaji "hamasa ya upendo" katika kutenda mambo yako ya
kimafanikio. Mara nyingi unashauriwa kufanya kitu kwa kukipenda kitu hicho
kutoka nafsini mwako.
Kwa mfano kama unafanya kazi usifanye kazi kwa sababu unamuogopa
bosi wako bali fanya kutokana upendo ulionao juu kazi yako.
Usifanye kitu kwa kuwaridhisha watu wengine bali ifanye kazi
yako kutokana na dhamira ambayo inakusukuma kutoka nafsini mwako. Ukifanya kitu
kutoka nafsini mwako itakufanya ufanye kazi kwa moyo wako wote kwani utafanya
kazi ambayo utakuwa unaipenda, na italeta matokeo chanya.
Hivyo kila wakati afisa mipango nasisitiza ya kwamba kwa
kila kitu ambacho unakifanya hakikisha unakifanya kitu hicho kwa sababu ya upendo
wa dhati juu ya kitu hicho, na sio kufanya jambo fulani kutokana na hofu.
Pia hakikisha ya kwamba hofu haikupi kipaumbele katika
maisha yako kwani hofu ni chukizo mbele ya Mugu na mafanikio yako kwa ujumla.
Kabla sijamaliza nikukumbushe tu ya kwamba maisha ni
kuchagua, hivyo jiulize sasa kipi ambacho kitaongoza maisha yako je hofu
au upendo? Usinipe jibu.
Ndimi afisa mipango Benson Chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.