Apr 21, 2017
Mambo Ya Kuzingatia Pale Unapoanzisha Biashara.
Njia
pekee itakuyokusaidia kuingiza kipato cha ziada na kukupeleka kwenye uhuru wa
kifedha ni kwa wewe kuamua kuanzisha biashara yako na utakayoamua kuisimamia
kikamilifu hadi ikuletee mafanikio.
Ili kuanzisha
biashara na ikafika mahali ukaanza kuona matunda ya biashara yako, kwa kawaida
huwa ipo misingi au mambo ambayo unatakiwa uzingatie sana ili biashara yako
iweze kudumu na kutoa faida uitakayo.
Yafuatayo Ni Mambo Ya Kuzingatia Pale
Unapoanzisha Biashara.
1. Elewa wateja wako wa mwanzo wanataka nini
na hapo utapata picha ya jinsi utavyoiendesha biashara na uzingativu juu ya
kazi. Ukijua wateja wako wanataka kitu gani, itakusaidia sana kuweza kuwapa
huduma hiyo.
2.
Kuwa mbunifu, hilo ndilo jambo kubwa
zaidi, biashara ni zilezile ila kinachofanya wateja wakimbilie biashara yako ni ubunifu wako. Kama usipokuwa mbunifu
na ukataka kufanikiwa kibiashara uwe na uhakika utakwama.
3.
Lugha nzuri kwa wateja na ukarimu, huweza kumasisha kuongezeka wa wateja wengi
katika biashara yako. hakua biashara ambayo italeta mafanikio makubwa kama wewe
mwenyewe una lugha mbovu na wateja wako.
4.
Epuka kutoa pesa ya mtaji kwa mahitaji binafsi utaua biashara. Hakikisha
mahitaji ya biashara na mahitaji yako binafsi unatenga kabisa. ni sumu kubwa sana
katika biashara kama eti huwezi kutofautisha matumizi binafsi na biashara yako.
5.
Jenga utaratibu wa kufanya tathimi ya
biashara yako wapi ulipotokana wapi ulipo na wap unaelekea,? Je, unasonga mbele
au unarudi nyuma, ukiona unarudi nyuma jiangalie upya, kujitathimini na ushituke
mapema kabla jahazi halijazama.
6.
Hifadhi kumbukumbu, hasa matumizi pamoja na mapato hata ya shilingi moja ya
sehem ya biashara. Jambo ambalo watu wengi hasa sisi weusi ni ngumu kwetu, na hii
ni kila siku unatakiwa kufanya. Huwezi kuendesha biashara na ikakua bila ‘documentation’. Hutajua ulikotoka, ulipo na unako enda kibiashara.
7.
Kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali wanaofanya biashara kama yako na
kufanikiwa pia usiwapuuze walioshindwa kwani nao wanacho cha kukufundisha.
Jifunze kwao kila siku hadi uweze kufanikiwa.
8.
Kuhakikisha biashara/duka haliishiwi bidhaa na kama likiishiwa bidhaa maana
yake uliowakopesha hawajarudisha, pia jitahidi kuweka mambo, mazingira ya
kuvutia wateja. Ukiweka mazingira hayo ujue ni lazima utaweza kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa.
9.
Kujitahidi kuweka aina ya bidhaa ambazo wateja wako watapata kwa urahisi na
jamii itakayo kuzunguka. Mteja anapenda sana duka ambalo kila akienda hakosi
bidhaa ambayo anaihitaji. Hapo ndipo mahali pake.
10.
Jitahidi na jifunze kukubali challenges/changamoto katika biashara yako na kutafuta njia
madhubuti ya kuzimaliza au kuzishughulikia. Ukiwa mtu wa kulia na hutaki
changamoto uwe na uhakika hutafika popote.
11.
Jitahidi kuangalia mbele kadri unavyona faida inaongezeka, jitahidi kuongeza
mtaji na kuzid kupanua biashara, hata kwa kufungua matawi zaidi pengine na
kuongeza ubora na ufanisi.
12. Usafi, ukarimu, kusoma nyakati, utafiti na
ubunifu na ni moja pia ya mambo ya kuzingatia. Eneo lako la biashara likiwa
safi na ukaongeza na ukarimu ni lazima utawavuta wateja wako katika biashara
kwa sehemu kubwa.
Kama
unataka kuanzisha biashara na ikakupa faida, hayo ndiyo mambo ya msingi sana
unatakiwa kuyazingatia na kuyatilia maanani kwa kiasi kikubwa ili kupata mafanikio
makubwa katika biashara yako.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa kibiashara.
Kama
unapenda kujifunza kwa ukaribu kabisa na sisi na kupata mafunzo mengi zaidi,
karibu kwenye kundi la Whats App,
kujiunga tuma neno THE UNIVESITY OF
WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35, ili kupata nafasi ya kuunganishwa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.