Apr 24, 2017
Tatizo Kubwa La Kutokutaka Kukosea Wakati Unatafuta Mafanikio Ni Hili Hapa.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza kuyapata bila kukosea, kama hutakosea na ukaweza
kufanikiwa basi wewe naweza kusema ni miongoni mwa watu ambao wana bahati sana.
Mafanikio ni matokeo ya kujifunza kutokana na makosa.
Tatizo
la watu wengi wanataka kufanikiwa lakini bila kukosea na wanasahau kwamba
hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana kwa namna hiyo. Mafanikio yanakuja kwa
kukosea na hilo si kosa, pengine kama unavyofikiri.
Unapotaka
kufanikiwa bila kukosea, kiuhalisa huwezi kufanikiwa sana kwa sababu, tatizo
kubwa la kutokukosea linakufanya ufanye mambo mengi kwa woga na mwisho wa siku
kujikuta ukipata mafanikio kidogo sana.
Kwa hiyo
ikiwa na maana kwamba kama unataka kufanikiwa, kukosea hakukwepeki, na wala
hilo sio suala la kuanza kujutia, ninaposema kukosea si maanishi kukosea kwa
makusudi bali naamanisha zile ‘mistake.’
Kama
kuna kitu umelenga kukifanya, hebu kifanye kwa moyo wote, acha kuwa na woga. Ikitokea
kama umekosea au umefanya makosa kwa bahati mbaya usisimame, endelea kusonga
mbele na kutafuta kilicho bora kwako.
Kushindwa
kwako kutakufanya ujirekebishe na kuwa na uwezo wa kufanikiwa kwa viwango vya
juu sana. Acha kuumizwa na kutokutaka kukosea kwako, kwani kumbuka kila wakati
tatizo kubwa la kutokutaka kukosea ni kushindwa kufanikiwa sana.
Unahitaji
sana kujifunza kutoka kwenye kukosea kwako kila wakati, fanya maisha yako yawe
shule bora ya kuweza kukusaidia kufanikiwa kwa viwango vya juu kabisa, hivyo
ndivyo mafanikio makubwa yanavyojengwa.
Makala hii imeandikwa na Imani
Ngwangwalu, DIRA YA MAFANIKIO.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.