Apr 27, 2017
Mambo Kumi Ya Kuimarisha Maisha Yako.
Maarifa
ni msingi mkubwa wa mafanikio kwa jambo lolote lile. Ndio maana kwa kadri jinsi
unavyozidi kuwa na maarifa bora na ndivyo maisha yako yanazidi kusimama na kuwa
ya mafanikio makubwa.
Hivyo
kwa mantiki hiyo ni muhimu sana kujifunza mambo yanayoimarisha maisha yako
karibu kila siku. Hebu leo katika makala haya, twende pamoja tujifunze mambo
kumi ya msingi yanayoweza kuimarisha maisha yako.
1. Washindi katika mafanikio hawafanyi
sana mambo tofauti na unayofanya wewe bali wanafanya mambo hayo kwa UTOFAUTI.
2.
Msingi mkubwa wa mafanikio unajengwa na mtazamo wako ulionao. Mtazamo ulionao
ndio unaokufanya ufanikiwe au ushindwe katika jambo unalolifanya.
3.
Mara nyingi fursa kubwa za mafanikio zinakuwa zipo miguuni petu au katika
maeneo yanayotuzunguka. Acha kutumia muda mwingi sana
kuangalia fursa zilizo mbali na wewe na kusahau pale ulipo.
Hapo
ulipo pia kuna fursa, kuwa makini na eneo ulilopo kuangalia fursa
zinazokuzunguka kufanikiwa. Unajua, ni rahisi sana kuona fursa zilizo upande
mwingine na kusahau fursa ulizonazo karibu yako.
4.
Fursa yoyote kubwa ikija kwako kama utaipoteza, sio rahisi fursa hiyo tena
kuweza kujitokeza kwako kwa namna nyingine.
Kwa hiyo kama kuna fursa imejitokeza kwako na una uwezo nayo itumie kwa
uhakika kukufanikisha.
5.
Mtazamo wowote ulionao uwe chanya au hasi, unajengwa na mambo makubwa matatu, Mazingira yanayokuzunguka, uzoefu katika
maisha na elimu. Hayo ndiyo mambo matatu yanayojenga mtazamo wako, Hakuna
mtazamo unaojengwa nje ya mambo hayo hapo.
6.
Faida za MAWAZO CHANYA katika maisha
yako.
Kuongeza ufanisi na ubora katika kazi.
Kuongeza faida kwa ukifanyacho.
Kutatua changamoto nyingi kwa urahisi.
Kupunguza msongo wa mawazo.
Kudumisha mahusiano bora na ya wengine.
7.
Hasara za MAWAZO HASI katika maisha
yako.
Msongo mkubwa wa mawazo.
Kupoteza afya.
Kuwa na hisia nyingi za maumivu.
Maisha yako kukosa maana.
Pamoja
na kwamba unajua hasara za mawazo hasi wengi wetu bado hawabadiliki unajua ni
kwa nini? ni kwa sababu ni asili ya binadamu kukataa mabadiliko, hapo unahitaji
nguvu nyingi ya kukutoa kwenye hali ya mazoea ili ufanikiwe kujenga mawazo
chanya.
8.
Hauhitaji elimu kubwa sana ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu
bora ambayo unaihitaji au unatakiwa
uipate ni elimu ya kubadilisha maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au
kukutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako
makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu inayotoa thamani ya maisha yako na sio
vinginevyo.
Kwa
hiyo kama kwa namna moja au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika
mahali unajilaumu kwamba ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea,
huu sio wakati wa kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani
itakayobadilisha maisha yako. na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani
darasani, inatafutwa mtaani kwa watu sahihi.
Ni
mzigo mkubwa sana kwako na kwa jamii kwa ujumla kuwa umesoma halafu hauna
mafanikio makubwa. Kama iko hivyo kwako, jiongeze kidogo tu, anza kuisaka elimu
sahihi, elimu ambayo itakupa thamani sahihi ya maisha yako na kukubadilisha na
kuwa mtu wa mafanikio. Maisha ya mafanikio hayaji kwa kusoma saana, bali ni kwa
kujifunza vitu sahihi ambavyo vina uwezo wa kubadilisha maisha yako.
9.
Kama vile ambavyo miili yetu ina hitaji chakula kizuri kila siku, pia akili
zetu zinahitaji maarifa bora kila siku ambayo yataweza kutubadilisha hapa
tulipo na kutupeleka eneo zuri zaidi kimafanikio.
10. Njia
mojawapo ya wewe kujisikia vizuri ni kufanya vitu ambavyo hutaweza kuhitaji
malipo yake kutoka kwa wengine. Unapojisikia vizuri ni rahisi sana kuweza
kufanya mambo makubwa na kwa msukumo mkubwa pia ulio ndani yako.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 628 929 816, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.