Apr 29, 2017
Kitu Chenye Nguvu Kubwa Kuliko Pesa Ni Hiki Hapa.
Kwa
wengi wetu si rahisi sana kuweza kuamini kwamba kipo kitu chenye thamani kubwa
kuliko pesa. wengi huamini sana pesa ni kila kitu, kwamba ukiwa na pesa basi,
ndio mambo yote yameishia hapo.
Lakini
upo ukweli mwingine ambao pengine huujui. Mbali na thamani ya pesa yenyewe,
malengo ni kitu ambacho kinathamani kubwa sana hata kuliko pesa yenyewe ,malengo ninayoyazungumza hapa ni malengo yanayofanyiwa kazi.
Kama
una mashaka kidogo na hili, naomba uwangalie watu ambao kuna wakati wanaweza
kupata pesa huku wakiwa hawana malengo ni kitu gani kinawatokea. Najua utagundua
pesa zao zilipotea.
Unapokuwa
una malengo hata upate pesa nyingi sana, si rahisi sana kupotea, tofauti na mtu
ambaye anajiendea tu bila kuwa na malengo yoyote. Ni rahisi kuweza kufuata
malengo yako na kufanikiwa.
Ipo nguvu kubwa sana kwenye kufuata malengo yako. |
Kwa
hiyo mpaka hapo unaona kwamba kitu ambacho kinaweza kuwa na thamani kubwa hata
kuliko pesa ni malengo yenyewe. Hasa hili linakuja kutokana na nguvu ya malengo
katika kupata pesa.
Pesa
nyingi hazipo kwenye pesa yenyewe, pesa nyingi zipo kwa wale wanajiwekea
malengo na kuamua kuyafuata kila inapoitwa leo. Kama una malengo imara na
unayafuta pesa utapata tu.
Kwa
vyovyote maisha yako yalivyo, kwa vyovyote na hali yoyote uliyonayo hata iwe
mbaya vipi, hauwezi kutoka hapo na kufanikiwa hata upewe pesa nyingi. Pesa hizo
utazipoteza usipokuwa na mikakati imara.
Kwa
hiyo ili uweze kufanikiwa kipesa zaidi, hebu hakikisha una mipango imara,
hakikisha una malengo yaliyo sahihi. Hapo utatengeneza pesa nyingi na kupata
mafanikio.
Tunamalize
makala hii kwa kusema kwamba, kitu kingine chenye nguvu kuliko hata ya pesa
yenyewe ni yale malengo unayojiwekea. Hicho
ndicho kitu chenye nguvu kuliko malengo yenyewe.
Nikutakie
siku njema na endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.